Huu ndio uchochezi tusioutaka. Be responsible with your keyboard chief.
Mkuu kwa uzoefu wangu kuna ukweli kuhusu hayo matukio unayosema kutokana na kuangalia kwa haraka zako.
Nidhaniavyo mimi: kumbuka watu wanaosoma arts ni wengi kuliko watu wanaosoma sayansi katika shule nyingi na hata vyuoni, kutokana na wingi wao ukitafuta kujua ni kiasi gani wanafanya upuuzi ukilinganisha na watu wa sayansi utagundua makundi haya hayaachani sana,
ila arts wanaonekana kwa sana kwa sababu ni wengi kwa idadi ukilinganisha na watu wanaosoma sayansi.
Ukitaka kujua kama hakuna tofauti tafuta sample flani then fanya hesabu yako interms of percent.
Kwa mfano:
Shule ''A'' yenye jumla ya wanafunzi 100.
Kwa kawaida arts hua wengi labda tufanye 60, then sayansi wabaki 40.
Then assume nusu ya wanafunzi wa arts yaani 30 wanalewa pombe, na nusu ya wanafunzi wa sayansi yaan 20 nao wanalewa.
Kwa hivyo asilimia ya arts wanaolewa ni= 30/60*100%=50%
Kwa sayansi fanya 20/40*100%=50%.
Ukiangalia hapo interms of percent wako sawa kua 50% ya arts na 50% ya sayansi ni walevi.
Turudi kwenye observation ya kawaida bila kujua sample size ya kila kundi.
Chance kubwa ya kuwaona walevi ni wanafunzi wa arts 0.6 (yaani P=ne/ns= 60/100= 0.6)
Chance ya kuwaona wanafunzi walevi kwa sayansi ni 0.4 yaani 40/100 kwa kutumia kanuni hiyo ya probability.
Nawasilisha wakuu.