Hyrax
JF-Expert Member
- May 20, 2023
- 964
- 2,675
Utu wa mtu unapimwa kwa kazi tena iliyo halali, kinyume na hapo wewe huna tofauti na wanyama waishio mwituni. Kwa muda mrefu sana nimejitahidi kufanya chunguzi mbalimbali, maana ni mambo ninayopenda hasa nikiwa sina vitu vingi vya kufanya.
Katika hili nililoandika kwenye kichwa cha uzi ninathibitisha kuwa, watu wenye tabia hizo tajwa wana hulka ya kuishi bila kiasi, tamaa na uvivu wa kufikiri na kutenda na tabia hizo zikikomaa ndani ya mtu zinamsukuma mtu kutafuta njia fupi za kufikia lengo analotaka. Jambo ambalo kiuhalisia hata akitimiza bado alichokifanya kitamwingiza kwenye hatia na majuto mengi kwa siku za usoni.
Nina mifano mingi ila mpaka naandika uzi huu kuna rafiki yangu sikuwa najua anafanya shughuli za ujambazi na utapeli, na sababu ya kutokujua kuwa anafanya shughuli hizo (dark hastle) ni kwasababu tulikuwa mikoa tofauti na yeye ni mwajiriwa wa serikali kama mimi.
Leo wenye nchi yao wamekuja kumkamata kama kuku aliyeko bandani, mke wake mrembo, mweupe analia sana, watoto wake wanne wa kike wazuri wanalia kwa huruma sana, jirani yake amenitumia footage za hilo tukio nimesikitika sana. Amefanya matukio zaidi ya 9, kati ya hayo matatu ni ya utapeli, sita ni ya wizi na ujambazi, na kati ya hayo ameua mara tatu.
Nyumba iliyotupu ni makao ya shetani, tufanye yaliyo haki, tufanye kazi halali, tuwe na kiasi ili mwisho wetu uwe mzuri.