Binadamu ana hulka ya kutosema ukweli....hulka ya kutosema mabaya/madhaifu yake
Wengi wetu huvutiwa na lugha za watu hasa mnapoonana kwa mara ya kwanza
Mapenzi kabla ya ndoa si kipimo halisi cha tabia utakazokutana nazo ndani ya ndoa hasa mihemko na Masham sham vinapoisha
Uwe makini na kuwa tayari kukabiliana na ukweli mchungu kuwa yule kabla ya ndoa hawezi kwa asilimia mia kuwa huyu baada ya ndoa
Hizi tabia hazionekani mapema bali hujifunua taratibu kadiri muda na kuzoeana kunapoongezeka..na hii yaweza kuchukua hata miaka
Watu wengi sana wameshindiwa hapa kwamba yule mtu uliyempenda na kumwamini sana kumbe ni
Mlevi mbwa
Malaya kupindukia
Mnafiki sana
Muongo
Bahili
Ana roho mbaya
Mbinafsi
Mchonganishi
Kigeugeu nknk
Ndani ya mahusiano ya muda mrefu ndio tabia kama hizi hujifunua, ni ngumu kwa baadhi ya hizi tabia mtu kusema ukweli wake ni ngumu sana
Moyo wa mtu ni kiza kinene sana, wengi wetu humu tuko kwenye mahusiano ya kindoa au kimapenzi tu, wengine wameshatendwa na wanaugulia maumivu
Jiepushe na maumivu jiepushe na kuvunjika kwa mahusiano kwasababu kuna gharama zake kubwa tu...imagine una invest muda raslimali na hisia zako kwa mtu kwa zaidi ya miaka mitano halafu unaishia divorce...!!! Gharama na hasara si haba
Tambua kwamba kuna tabia za kuchukiza na pengine zisizovumilika.. jiandae kuzikabili na kuzikubali.. .. hakuna mkamilifu kila mwanadamu ana roho ya kishetani ikiwemo WEWE[emoji12] [emoji15] [emoji23]Asikudanganye mtu kuwa hizo tabia zinarekebishika, huko ni kujidanganya na kujitafutia maumivu zaidi