Tabia zilizojificha: Chanzo cha migogoro kwenye mahusiano

Tabia zilizojificha: Chanzo cha migogoro kwenye mahusiano

Mimi tabia yangu sijaficha, nime post... Kilevi aka kimea ni tatizo kubwa sana kwangu
 
Mimi tabia yangu sijaficha, nime post... Kilevi aka kimea ni tatizo kubwa sana kwangu
[emoji23] [emoji23] [emoji23] hii inazungumzika kuna zile inborn...! Kwa mfano hivi kweli unaweza kumwambia shem kwamba una kaugonjwa kakupenda kupiga chabo? [emoji15] [emoji15] [emoji23] [emoji23]
 
d987097e8c8575a51ef34a66fc0ba71e.jpg
Binadamu ana hulka ya kutosema ukweli....hulka ya kutosema mabaya/madhaifu yake
Wengi wetu huvutiwa na lugha za watu hasa mnapoonana kwa mara ya kwanza
Mapenzi kabla ya ndoa si kipimo halisi cha tabia utakazokutana nazo ndani ya ndoa hasa mihemko na Masham sham vinapoisha
Uwe makini na kuwa tayari kukabiliana na ukweli mchungu kuwa yule kabla ya ndoa hawezi kwa asilimia mia kuwa huyu baada ya ndoa
Hizi tabia hazionekani mapema bali hujifunua taratibu kadiri muda na kuzoeana kunapoongezeka..na hii yaweza kuchukua hata miaka
Watu wengi sana wameshindiwa hapa kwamba yule mtu uliyempenda na kumwamini sana kumbe ni
Mlevi mbwa
Malaya kupindukia
Mnafiki sana
Muongo
Bahili
Ana roho mbaya
Mbinafsi
Mchonganishi
Kigeugeu nknk
Ndani ya mahusiano ya muda mrefu ndio tabia kama hizi hujifunua, ni ngumu kwa baadhi ya hizi tabia mtu kusema ukweli wake ni ngumu sana
Moyo wa mtu ni kiza kinene sana, wengi wetu humu tuko kwenye mahusiano ya kindoa au kimapenzi tu, wengine wameshatendwa na wanaugulia maumivu
Jiepushe na maumivu jiepushe na kuvunjika kwa mahusiano kwasababu kuna gharama zake kubwa tu...imagine una invest muda raslimali na hisia zako kwa mtu kwa zaidi ya miaka mitano halafu unaishia divorce...!!! Gharama na hasara si haba
Tambua kwamba kuna tabia za kuchukiza na pengine zisizovumilika.. jiandae kuzikabili na kuzikubali.. .. hakuna mkamilifu kila mwanadamu ana roho ya kishetani ikiwemo WEWE[emoji12] [emoji15] [emoji23]Asikudanganye mtu kuwa hizo tabia zinarekebishika, huko ni kujidanganya na kujitafutia maumivu zaidi
78d839dc3add7eb5673093f810dba387.jpg
Mkuu roho ya kishetani ndo ikoje na utaitambuje
 
Ila wewe Mnyanki mbishi kimtindo. Kwa hiyo am in...

Bora umechoka mapema ili upunguze competition hata.

Back to the topic,
Kwa kweli mimi haya nayaona kama vile ni hadithi tu kwangu, nikiamini kabisaaa kuwa kila mtu lazima awe na katabia fulani ambacho hukapendi, ila kama uliweza kuiona na ukaendelea naye hadi mkafikia ndoa basi hilo jaribu wewe unaweza kulishinda. si unaona hata umekuwa na ujasiri wa kusonga nalo mbele?
Hayo unayoyaona kama mapungufu utakuja kuona kama kumbe yalikuwa madogo tu ukimwachia akaondoka, utajikuta unatengeneza benchmark kila unapokutana na mwingine ukilinganisha na aliyetangulia unaona afadhali ya jana kuliko leo....

Shika sana ulichonacho, chondechonde tusitumie saaaana nguvu nyingu kutafuta mapungufu ya wenzetu. Bali tutafute zaidi mazuri yao, kwani mazuri yakiwa mengi yanaweza kuyashinda hayo mapungufu automatically

Pendaneni salama.
 
Ndo ujue watu wanamuhitaji Bwana Yesu awaokoe, awatakase na kuwafungua na vifungo hivyo kabla na baada ya ndoa, kwa akili ya kibinadamu huwezi kumjua mwenzi wako, bali kwa mafunuo ya Roho Mtakatifu utaweza, na ukishamjua utajua how to deal with their weaknesses positively badala ya kutumia madhaifu ya mwenzako kumtenga na kumsimanga na kumfanya apotee zaidi. Kama ukishindwa kumsaidia/ku deal na udhaifu wa mwenzako, HATA WEWE UTAKUWA NA MADHAIFU KIBAO ULIYOFICHA.
 
Back
Top Bottom