Tabora: Ahukumiwa kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya ulawiti

Tabora: Ahukumiwa kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya ulawiti

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
MAHAKAMA ya Wilaya ya Tabora imemuhukumu mkazi wa Kidatu “B” kata ya Mtendeni Mkoani Tabora Husseni Mashibu (32) kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hati ya kumlawiti mtu mzima hadharani huku watu wakishuhudia kwa kumtuhumu kuwa ana mahusiano na mke wake.

Akitoa hukumu hiyo leo Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Tabora Sigwa Mzige mahakama imeona kifungo hicho kwa mshitakiwa kimstahili kwani alifanya unyama usiweze kuvumiliwa na jamii.

Alisema kifungo hicho kitakuwa fundisho kwa mshitakiwa huyo na wengine wenye nia ya kuwadhalilisha watu wengine kutokana na wivu wa mapenzi.

Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Wilaya Tabora Sigwa Mzige alìiambia Mahakama hiyo ushahidi uliotolewa ulitolewa mbele ya Mahakamani hiyo umeonyesha hauna shaka yoyote ukilinganisha na ushaidia uliotolewa na Mtuhumiwa Mwenyewe, Daktari ambae alithibitisha kutokana na Vipimo vya aliye lawitiwa alipata Michubuko na alipewa dawa ya Misuli.

“Mahakama zote Nchini zinafanyakazi vizuri kuhakikisha kila Mtuhumiwa analetwa hapa kwa Makosa mbalimbali kila kosa moja lina adhabu yake,” Mzige alisema.

Awali Wakili wa Serikali Robert Kumwembe aliiambia Mahakama hiyo kwamba Mshitakiwa ni Mkosaji wa Mara ya kwanza anapaswa kupata adhabu ya hiyo ya kwenda jela Maisha.

Wakili huyo aliambia mahakama hiyo kwamba Mtuhumiwa alipatikana na kosa la kumlawiti mtu Mzima ( Jina limehifadhiwa ) mnamo 30 January 2022 katika maeneo ya Kidatu “B” mkoani Tabora.

IPP Media
 
Duuuuuuh huko anako kwenda ataenda kua mke wa mtu, mtenda hutendwa 🚶🚶🚶🚶🚶
 
Nawaza tu hiyo Hadharanii kasimamisha mashine kaingiza kwenye tigo ya mwenzake.

Hio hadhara ilikuwa na watu wa aina gani? Walikuwa wanashangilia ama wanasikitika ?
Ingekua ni kweli basi picha na vdo clips zingesha sambaa mitandaoni.
 
Nawaza tu hiyo Hadharanii kasimamisha mashine kaingiza kwenye tigo ya mwenzake.

Hio hadhara ilikuwa na watu wa aina gani? Walikuwa wanashangilia ama wanasikitika ?
Sifa mtaani bila tahadhari kisheria ndo tokeo lake
 
Kwa ajili watu hawajui kuna dini nyingine ndio maana kila siku wanauliza,"Hii dunia imekuwa nini siku hizi?"
Watu hawajui kuhusu dini ya Shetani.
 
Kwa ajili watu hawajui kuna dini nyingine ndio maana kila siku wanauliza,"Hii dunia imekuwa nini siku hizi?"
Watu hawajui kuhusu dini ya Shetani.
Unaweza kuongea vizuri kidogo ili na sisi slow learners tukuelewe?!!!
 
Back
Top Bottom