The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Askari watatu wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) pamoja na mgambo wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Tabora kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Grace Mussa (4) katika Kijiji cha Mpanda Mlowoka wilayani Kaliua, mkoani Tabora.
Akizungumza na Mwananchi leo Desemba 2, 2024 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Bwao amesema askari hao wanadaiwa kuhusika na kifo cha mwanafunzi huyo wa Shule ya Awali ya Kalemela baada ya kufyatua risasi na kumpiga mtoto huyo.
“Desemba 2, 2024 maeneo ya Kijiji cha Mpanda Mlowoka, saa nane mchana askari wa uhifadhi wa misitu wakiwa kwenye doria Hifadhi ya Taifa ya Msitu wa Kigosi Muyowosi walikamata trekta lenye namba za usajili T.689 DCA mali ya Sandu Kate iliyokuwa inalima ndani ya hifadhi.
“Wakiwa njiani kurudi kambini kwao maeneo ya Igombambili Kitongoji cha Mpanda Mlowoka wananchi walijikusanya na kuwazuia askari hao wasiipeleke trekta hiyo kambini kwao na kuziba barabara na magogo, ndipo askari hao wakiwa na silaha mbili aina ya AKA 47 walifyatua risasi na kusababisha kifo cha Grace Mussa na kumjeruhi Zengo Sandu (27),”amesema.