Tabora: Askari TFS matatani kusababisha kifo cha mwanafunzi wa awali

Tabora: Askari TFS matatani kusababisha kifo cha mwanafunzi wa awali

Askari watatu wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) pamoja na mgambo wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Tabora kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Grace Mussa (4) katika Kijiji cha Mpanda Mlowoka wilayani Kaliua, mkoani Tabora.

Akizungumza na Mwananchi leo Desemba 2, 2024 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Bwao amesema askari hao wanadaiwa kuhusika na kifo cha mwanafunzi huyo wa Shule ya Awali ya Kalemela baada ya kufyatua risasi na kumpiga mtoto huyo.

“Desemba 2, 2024 maeneo ya Kijiji cha Mpanda Mlowoka, saa nane mchana askari wa uhifadhi wa misitu wakiwa kwenye doria Hifadhi ya Taifa ya Msitu wa Kigosi Muyowosi walikamata trekta lenye namba za usajili T.689 DCA mali ya Sandu Kate iliyokuwa inalima ndani ya hifadhi.

“Wakiwa njiani kurudi kambini kwao maeneo ya Igombambili Kitongoji cha Mpanda Mlowoka wananchi walijikusanya na kuwazuia askari hao wasiipeleke trekta hiyo kambini kwao na kuziba barabara na magogo, ndipo askari hao wakiwa na silaha mbili aina ya AKA 47 walifyatua risasi na kusababisha kifo cha Grace Mussa na kumjeruhi Zengo Sandu (27),”amesema.

View attachment 3168105
Hata hivyo siku hizi ,damu ya mlalahoi wa Tanzania haina thamani yoyote, tunasuburi tu kusikia mwingine tena ameuwa sijui na nani nani huko, Kisha tunasahau maisha yanaendelea, matamko makali makali mbele ya camera kwamba tunachunguza ndiyo inakuwa mwisho.
 
Aisee Nchi kama imelaaniwa hii yaani mtoto anauawa kwa risasi kirahisi tu wakilinda mbao ya mninga..
 
Hivi hata hii ya kuandika kuwa mtoto wa 4 yrs alikuwa analima imekaaje? Anyway Rest in heaven katoto 💔
 
Askari wa vyombo vyetu wanachangamoto ya jinsi ya kutuliza ghasia za raia wasiokua na silaha . Kila ghasia hata kama ni ndogo kiasi gani inaohusisha vyombo hivi na raia lazima kutokee vifo .Utasikii risasi ilipigwa juu ikampata bahati mbaya au katika harakati za kuokoa maisha yake akampiga risasi bahati mbaya .
 
Hata kama ndio umpige mtu risasi kumuua!?
Kwanini wasingemkamata na kumuwajibisha kwa namna inayofaa hadi akatishwe uhai!?
Nadhani wao uhisi kila aliyekoporini ni mnyama hatarishi.
 
Hivi hata hii ya kuandika kuwa mtoto wa 4 yrs alikuwa analima imekaaje? Anyway Rest in heaven katoto 💔
Wanatafuta namna ya kukwepa eti baadae ionekane alidhani ni mnyama hatari kumbe ni binafamu analima, sasa haya mtoto ni miaka 4
 
kifungo Cha maisha kitawatosha.
Askari hawajui sehemu na muda Gani wa kutumia bunduki ni shida hyo.
 
Will there be a trial for excessive use of force against unarmed civilian? What precautions must be taken by law enforcement officers in there prescribed duties? What are the protocol for trespassing a conserved area?

My wish is to see justice prevail for the loss of life of a child who's dreams were shattered too soon.
 
Will there be a trial for excessive use of force against unarmed civilian? What precautions must be taken by law enforcement officers in there prescribed duties? What are the protocol for trespassing a conserved area?

My wish is to see justice prevail for the loss of life of a child who's dreams were shattered too soon.
Huyu naye khee! Kumbe humu kuna wanaojifunza sheria kwa kutumia maoni yetu, eti wanakwepa ada.
 
Back
Top Bottom