Tabora: Nyoka Koboko amekunywa uji wa Moto, amkimbiza Mganga wa Kienyeji

Tabora: Nyoka Koboko amekunywa uji wa Moto, amkimbiza Mganga wa Kienyeji

images.jpeg

Hawa ndo kiboko ya nyoka
 
View attachment 2060887
Nyoka aina ya koboko anadaiwa kuweka kambi katika eneo la Mlimani City kata ya Ng'ambo manispaa ya Tabora ambapo amegeuka kuwa tishio la maisha kwa wananchi wa mtaa huo.

Katika jitihada za kumuondoa nyoka huyo wananchi walimleta mganga wa kienyeji ambaye alitamba kumuondoa nyoka huyo.

Mganga huyo Hassan Jumanne anasema alipanda juu ya mti wa muembe yalipo makazi ya nyoka huyo akiwa na chungu chenye uji wa moto ambao nyoka huyo alitoka na kuingiza kichwa kwenye uji kabla ya kumshambulia kwa kumgonga mara nne.

Mganga alizimia na kuanguka na alipopata fahamu alikimbia akiacha vifaa vyake vya uganga katika eneo hilo.

Uongozi wa kata hiyo umeanza jitihada za kuwasiliana na maliasili ili kumuondoa nyoka huyo.

Chanzo cha habari: CG FM Radio
🤣🤣🤣 Tanzania sihami
 
Mkuu Unamjua koboko wewe? Yule aking'ata haachi meno Bali sumu yeke hupita kwenye meno yake kwenda kwa mjeruhiwa,na anao uwezo wa kungata zaidi ya Mara kumi.
Basi hana madhara sana kama anavyopigiwa chapuo, kang'ata mtu mara nne na bado akawa na uwezo wa kukimbia baada ya kuzinduka?

Au kinga ya mtaalam na yenyewe haikua haba?
 
Back
Top Bottom