Tabora: Nyoka Koboko amekunywa uji wa Moto, amkimbiza Mganga wa Kienyeji

Tabora: Nyoka Koboko amekunywa uji wa Moto, amkimbiza Mganga wa Kienyeji

Kawaida nyoka wa kawaida hagongi zaidi ya Mara moja kwasababu akigongo meno hubakia je huyu kapata wapi uwezo wa kugonga mara nne?
Koboko haachi jino ng'oo kama ulikuwa hujui, anaweza kuvamia zizi la ng'ombe akagonga wote na kuua. Hii sifa ndiyo inayomfanya awe nyoka hatari kuliko wote Afrika. Tena anaweza kugonga bila kuacha jeraha ila ukizubaa huponi
 
FB_IMG_1640713977491.jpg


ukikutana na hii kitu jaribu mbio labda ndio zinaweza kukuokoa tofauti na hapo ukianza kutafuta mawe au fimbo ni labda mfe wote au ufe wewe.
 
Koboko alipewa uji wa lishe.Hii ni zaidi ya joke.Il pia kwamba huyo mganga alizinduka na kukimbia baada ya kuangushwa na koboko hiyo ndiyo habari mhimu ya kufuatilia,aligongwa kweli au alitishiwa tu kwa hofu akaanguka chini.Koboko kweli jamaa anaweza kuendelea kuwa hai?
View attachment 2060887
Nyoka aina ya koboko anadaiwa kuweka kambi katika eneo la Mlimani City kata ya Ng'ambo manispaa ya Tabora ambapo amegeuka kuwa tishio la maisha kwa wananchi wa mtaa huo.

Katika jitihada za kumuondoa nyoka huyo wananchi walimleta mganga wa kienyeji ambaye alitamba kumuondoa nyoka huyo.

Mganga huyo Hassan Jumanne anasema alipanda juu ya mti wa muembe yalipo makazi ya nyoka huyo akiwa na chungu chenye uji wa moto ambao nyoka huyo alitoka na kuingiza kichwa kwenye uji kabla ya kumshambulia kwa kumgonga mara nne.

Mganga alizimia na kuanguka na alipopata fahamu alikimbia akiacha vifaa vyake vya uganga katika eneo hilo.

Uongozi wa kata hiyo umeanza jitihada za kuwasiliana na maliasili ili kumuondoa nyoka huyo.

Chanzo cha habari: CG FM Radio
 
Kawaida nyoka wa kawaida hagongi zaidi ya Mara moja kwasababu akigongo meno hubakia je huyu kapata wapi uwezo wa kugonga mara nne?

Sio kila wakati nyoka hubakiza fangs au meno kwenye mwili bali meno hubaki kama tu yalikuwa yamechoka au ugumu wa ngozi ya mnyama
Ila huwa yanaota tena na tena

Kuhusu black mamba huyu ni shetani na ana hasira za kipumbavu sana

Ana uwezo wa kugonga hata watu kumi kama wamelala mahali pamoja

Huyu katika nyoka wote namuheshimu sana
 
Koboko anapiga hata mara ishirini, na zote anatoa sumu


Huyo Koboko anaitwa "Shetani"---- ni nyoka mwenye kasi kubwa kuliko nyoka wote na sumu yake ni ile yenye mchanganyiko wa sumu mbili, huyo huwa na hasira kali hasa akiwa analinda kiota cha mayai yake, kisipite kiumbe chochote karibu ya hapo, atalala nacho mbeRE🤣.
 
Back
Top Bottom