Tabora: Nyoka Koboko amekunywa uji wa Moto, amkimbiza Mganga wa Kienyeji

Tabora: Nyoka Koboko amekunywa uji wa Moto, amkimbiza Mganga wa Kienyeji

Hivi watu hamuelewi? Mbona Wa TZ mnakuwa majinga na mbumbumbu kiasi hiki? Hilo ni fumbo, na si stori kama mnavyodhani. That's a code, wachache mno wameelewa. Rudia kusoma kwa makini.

Sent from my A50s using JamiiForums mobile app
Mkuu mbona wanitusi ? Code zake zinaeleweka mbona unanikazia ? Tunaendeleza code tu kaa kwa pattern
 
Unampa heshima shetani??![emoji1787]

Huyu kwa kweli acha nimpe tu

Napenda sana nyoka na nimekutana nao wa aina nyingi
Kuna siku naelekea Horohoro njiani nilimuona Rock python urefu kama 4 meters hivi na mkubwa haswa
Nilisimamisha gari na haraka nilishuka kumuangalia akikatisha barabara taratibu baada ya kuona hatuna madhara nae

Cobra pia yupo Shambani na ni marufuku kumuua ana miaka mingi hapo na hana tatizo na mtu
All in all napenda sana nyoka ila huyu ukikutana nae sali sala za mwisho
 
Mlimani City kata ya ng'ambo![emoji848]
hapa dar nipo mahali fulani kuna siku nasikia vijana wanasema wanaenda mlimani city nikapata tabu kulingana na namna walivyo.

baada ya kuondoka nikamuuliza mtu jirani kuna duka kuwa hawa wanafanya nini mlimani city?

kumbe kuna eneo lina kapori kidogo ndio wanaliita hivyo hulitumia kwenda kupata weed wamelibariki kwa jina hilo.
 
View attachment 2060887
Nyoka aina ya koboko anadaiwa kuweka kambi katika eneo la Mlimani City kata ya Ng'ambo manispaa ya Tabora ambapo amegeuka kuwa tishio la maisha kwa wananchi wa mtaa huo.

Katika jitihada za kumuondoa nyoka huyo wananchi walimleta mganga wa kienyeji ambaye alitamba kumuondoa nyoka huyo.

Mganga huyo Hassan Jumanne anasema alipanda juu ya mti wa muembe yalipo makazi ya nyoka huyo akiwa na chungu chenye uji wa moto ambao nyoka huyo alitoka na kuingiza kichwa kwenye uji kabla ya kumshambulia kwa kumgonga mara nne.

Mganga alizimia na kuanguka na alipopata fahamu alikimbia akiacha vifaa vyake vya uganga katika eneo hilo.

Uongozi wa kata hiyo umeanza jitihada za kuwasiliana na maliasili ili kumuondoa nyoka huyo.

Chanzo cha habari: CG FM Radio
Fasihi simulizi
 
hapa dar nipo mahali fulani kuna siku nasikia vijana wanasema wanaenda mlimani city nikapata tabu kulingana na namna walivyo.

baada ya kuondoka nikamuuliza mtu jirani kuna duka kuwa hawa wanafanya nini mlimani city?

kumbe kuna eneo lina kapori kidogo ndio wanaliita hivyo hulitumia kwenda kupata weed wamelibariki kwa jina hilo.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom