Tabora: Nyoka Koboko amekunywa uji wa Moto, amkimbiza Mganga wa Kienyeji

Tabora: Nyoka Koboko amekunywa uji wa Moto, amkimbiza Mganga wa Kienyeji

Daah umekosea kutukana! Ila anyway, acha inyeshe tuone panapovuja!

Sent from my A50s using JamiiForums mobile app

Ume quote wengi humu na kutukosea heshima
Sio tabia yangu kutukana ila umetutukana wewe
Next time jaribu kuelewesha mambo bila kutumia maneno makavu
Wengine wajukuu zetu wamo humu eti [emoji23][emoji120]
 
View attachment 2060887
Nyoka aina ya koboko anadaiwa kuweka kambi katika eneo la Mlimani City kata ya Ng'ambo manispaa ya Tabora ambapo amegeuka kuwa tishio la maisha kwa wananchi wa mtaa huo.

Katika jitihada za kumuondoa nyoka huyo wananchi walimleta mganga wa kienyeji ambaye alitamba kumuondoa nyoka huyo.

Mganga huyo Hassan Jumanne anasema alipanda juu ya mti wa muembe yalipo makazi ya nyoka huyo akiwa na chungu chenye uji wa moto ambao nyoka huyo alitoka na kuingiza kichwa kwenye uji kabla ya kumshambulia kwa kumgonga mara nne.

Mganga alizimia na kuanguka na alipopata fahamu alikimbia akiacha vifaa vyake vya uganga katika eneo hilo.

Uongozi wa kata hiyo umeanza jitihada za kuwasiliana na maliasili ili kumuondoa nyoka huyo.

Chanzo cha habari: CG FM Radio
Ndiyo maana Subwoofer na Bi Tozo wanaparurana huku😀
 
Huyu kwa kweli acha nimpe tu

Napenda sana nyoka na nimekutana nao wa aina nyingi
Kuna siku naelekea Horohoro njiani nilimuona Rock python urefu kama 4 meters hivi na mkubwa haswa
Nilisimamisha gari na haraka nilishuka kumuangalia akikatisha barabara taratibu baada ya kuona hatuna madhara nae

Cobra pia yupo Shambani na ni marufuku kumuua ana miaka mingi hapo na hana tatizo na mtu
All in all napenda sana nyoka ila huyu ukikutana nae sali sala za mwisho


Huyo koboko mzee wangu alipata kunihadithia kwamba aliwahi kufukuzwa na huyo nyoka barabarani akitokea Kasulu kwenda Kigoma mjini mzee akiwa na gari yake Landrover 109 in 70s. Na yeye huyo mzee wangu ndiye aliyeniambia kwamba huyo sio nyoka bali ni "Shetani" 🤣
 
Nimecheka kwa sauti, nimepata picha anavotoka nduki.


Yaani kazimia tu hajapata madhara ya sumu?

Bora walivoamua kuwaita wataalamu wa kisayansi....sasa wao wakaleta mganga ambaye akaamua kumuunguza kwa uji.....ha ha ha ha....nyoka hasira yake ikaishia kwake.
Kwa mkoa wa Tabora, toka miaka ya zamani, hiyo Ndo ilikua mbinu ya kupambana na Nyoka .
 
Mkuu Unamjua koboko wewe? Yule aking'ata haachi meno Bali sumu yeke hupita kwenye meno yake kwenda kwa mjeruhiwa,na anao uwezo wa kungata zaidi ya Mara kumi.
mkuu kaboko ana mapigo 12 baada ya hapo ana uwezo tena wa kugonga
ila ili kujilinda ndio huleta sitofahamu ya mbwembwe za kufyokafyoka na kukimbiza kimbiza hovyo au anaweza akaondoka kabisa eneo hilo 7bu itamchukia tena muda mrefu kuwa na uwezo wa kugonga na kudhuru
ndo mana hata wanaoenda kumuwinda kaboko wanamlia timing hiyo
 
Ngoja niwape mbinu ya kumkamata koboko,waende police kitengo cha mbwa au kwa yeyeto mwenye yale mavazi ya kufundishia mbwa unayavaa,plus buti, helmet.kisha unamfata alipo koboko au nyoka yeyeto mwenye sumu unamkamata Akigonga kichwa anakutana na helmet, Akigonga mwilini ukutana na nguo Akigonga mguuni ukutana na buti,akitema mate ukutana na kioo,mikononi umevaa gloves za boxing.
Kama meno ya mbwa ayapenyi kwenye suti hiyo sembuse ya snake
Mbinu ya ndoo na uji ya kizamani mtakula snake bites za kutosha.

professional-dog-trainer-clothes-in-black-and-red-big(1).jpg
 
Ngoja niwape mbinu ya kumkamata koboko,waende police kitengo cha mbwa au kwa yeyeto mwenye yale mavazi ya kufundishia mbwa unayavaa,plus buti, helmet.kisha unamfata alipo koboko au nyoka yeyeto mwenye sumu unamkamata Akigonga kichwa anakutana na helmet, Akigonga mwilini ukutana na nguo Akigonga mguuni ukutana na buti,akitema mate ukutana na kioo,mikononi umevaa gloves za boxing.
Kama meno ya mbwa ayapenyi kwenye suti hiyo sembuse ya snake
Mbinu ya ndoo na uji ya kizamani mtakula snake bites za kutosha.

View attachment 2061048
Hii nimeielewa.. ikiwa applied inaweza kuwasaidia ndugu zetu wanyamwezi huko Tabora na hatimaye kumtia nguvuni bwana nyoka
 
Back
Top Bottom