Tabora: Nyoka Koboko amekunywa uji wa Moto, amkimbiza Mganga wa Kienyeji

Tabora: Nyoka Koboko amekunywa uji wa Moto, amkimbiza Mganga wa Kienyeji

Kwahiyo huo uji ndo silaha ya kupambana na nyoka? Tupe darasa kidogo tujue matumizi ya uji katika kukabiliana na majoka yenye sumu kali
Wakati huo hawa wazee wa kimilia au waganga, ilikua wakisikia tishio la uwepo wa nyoka wanajificha katika Miti.


Basi linachukuliwa Sufuria kubwa, unapikwa Uji , na Mzee au Mganga ,anajitwika hilo sufuria na Uji wamoto.


Kabla ya hapo anajipaka dawa mwili mzima ya kumvuta huyo nyoka ili amshambulie .


Basi baada yahapo anaenda kunako. Akipita maeneo Yale, yule nyoka mtini ,katika kuruka kumshambulia Mzee/Mganga, hujikuta katumbukia kwenye Sufuria la Uji mjizito wa moto.


Nyoka anakufa kwa kuunguzwa na Uji wa moto.
 
Kuhusu Hali za makazi na mazingira yetu kwa usalama wetu bila kusubiri Hawa strangers ni vema kuzingatia usafi wa mazingira na fumigation za mara kwa mara...
 
Mbinu ya tatu tumieni drone zile za kunyunyiza dawa zina tank la kuweka dawa jaza mafuta ya taa,msake kwa drone alipo weka dawa za kumvutia asogee karibu Ili umsspray mafuta taa.
Drones pia zinatumika kuwafukuza wanyama waharibifu mashambani mfano tembo,na walao nyasi pia majumbani mfano simba,chui,nk.
Pia unaweza zitumia kupambana na wafugaji walishao mifugo kwenye mashamba unawaspray pilipili au maji washa au upupu.
# Tumepewa akili tuwatawale wanyama na vyoote vikaavyo duniani ikiwemo majini yasiyoonekana.
 
Mzee kuna dawa huwezi amini.
Mimi nilishashudia jamaa amegongwa na huyo kiumbe ila alipona msela.
Yeah mkuu ni 100 kwa wawili wanaopata bahati hiyo but hata huyo aliyepona ukimtizama sana unakuta hayupo sawa upstairs,akimuuma victim wake haraka sana sumu husambaa kwenye damu,kwenye ubongo ikirudi kwenye lungs na moyo parapanda inalia.

Ndani ya 14 minutes mtu yupo mahututi hajiwezi dk 20 ndo nitolee.
 
View attachment 2060887
Nyoka aina ya koboko anadaiwa kuweka kambi katika eneo la Mlimani City kata ya Ng'ambo manispaa ya Tabora ambapo amegeuka kuwa tishio la maisha kwa wananchi wa mtaa huo.

Katika jitihada za kumuondoa nyoka huyo wananchi walimleta mganga wa kienyeji ambaye alitamba kumuondoa nyoka huyo.

Mganga huyo Hassan Jumanne anasema alipanda juu ya mti wa muembe yalipo makazi ya nyoka huyo akiwa na chungu chenye uji wa moto ambao nyoka huyo alitoka na kuingiza kichwa kwenye uji kabla ya kumshambulia kwa kumgonga mara nne.

Mganga alizimia na kuanguka na alipopata fahamu alikimbia akiacha vifaa vyake vya uganga katika eneo hilo.

Uongozi wa kata hiyo umeanza jitihada za kuwasiliana na maliasili ili kumuondoa nyoka huyo.

Chanzo cha habari: CG FM Radio
Mganga kaponaje kwa sumu ya koboko au ndiyo uchawi?
 
Back
Top Bottom