Tabora: Nyoka Koboko amekunywa uji wa Moto, amkimbiza Mganga wa Kienyeji

Tabora: Nyoka Koboko amekunywa uji wa Moto, amkimbiza Mganga wa Kienyeji

Watu wa zamani walikuwa wanamuwinda koboko kwa njia ya kubeba uji wa moto kwenye chungu kichwani, halafu wanapita chini ya mti ambao koboko anakaa. Koboko ana tabia ya kuwinda kichwa tena katikati ya utosi, hivyo akigonga anakutana na uji wa moto.

Sasa huyo mganga kapona kwa sababu sumu nyingi imepunguzwa baada ya koboko kukonga ule uji. Itakuwa sufuria au chungu cha uji kilimwagika baada ya kugongwa na koboko, ndi maana mganga naye akagongwa!

Taimingi ya mganga haikuwa nzuri

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kawaida nyoka wa kawaida hagongi zaidi ya Mara moja kwasababu akigongo meno hubakia je huyu kapata wapi uwezo wa kugonga mara nne?
Mada ni koboko.

Sasa wewe unazungumzia nyoka aina gani?

Koboko ulishasikia anauma na kung'oka meno?
 
Hii habari ni uongo, haiwezekani mtu agongwe na nyoka azimie afu azinduke
 
Mbinu ya tatu tumieni drone zile za kunyunyiza dawa zina tank la kuweka dawa jaza mafuta ya taa,msake kwa drone alipo weka dawa za kumvutia asogee karibu Ili umsspray mafuta taa.
Drones pia zinatumika kuwafukuza wanyama waharibifu mashambani mfano tembo,na walao nyasi pia majumbani mfano simba,chui,nk.
Pia unaweza zitumia kupambana na wafugaji walishao mifugo kwenye mashamba unawaspray pilipili au maji washa au upupu.
# Tumepewa akili tuwatawale wanyama na vyoote vikaavyo duniani ikiwemo majini yasiyoonekana.
Mbinu nzuri sana
 
Mbinu nzuri sana
Nzuri Sana kwa wafugaji wakorofi hasa wasukuma na masai walishao mashambani Mwa watu kwa kuwapiga wakulima unawaspray pilipili au upupu au maji washa au kuspray nyasi pilipili Ili ng'ombe au tembo wasisogelee mazao.
Pia nzuri pia kukimbizia panyaroad wakivamia mtaa unawaspray pilipili iliyochanganywa na upupu au maji washa.
 
Tembo ukimpelekea drones speed yake utoiweza ukimbia hatari.
Drones ufukuza nyani,tumbili, na wanyama wote waharibifu ikiwemo ndege waharibifu pia.
Hii ni fursa kwa vijana msio na ajira drones zimejaa tele China bei rahisi kuanzia laki 3 hadi Dar msimu wa kilimo unarudisha pesa yako na faida tele unakodiwa na wakulima kuwalindia mazao yao.
Unaiprogram sauti yeyeto uitakayo zipo sauti na vitisho vya kila namna kulingana na ndege au mnyama uwatakao kuwafukuza.
 
Koboko wa Next Generation. Sio wale wa kizazi kile waliokuwa wanakufa kwa uji. Eti unatumia mbinu za kizamaani kumkamata koboko wa 4G, utaishia mortuary 🏃‍♂️🏃‍♂️🤸‍♂️🤸‍♂️🈶🎶
 
Kawaida nyoka wa kawaida hagongi zaidi ya Mara moja kwasababu akigongo meno hubakia je huyu kapata wapi uwezo wa kugonga mara nne?
Nilikuaga na shamba tabora nikawa nimefuga kuku wa kienyeji,usiku akaja nyoka kagonga kuku kama 10 waliokua wanalalia mayai. Tulimsaka balaa kumbe tulikua tunajitafutia matatizo tu
 
Tembo ukimpelekea drones speed yake utoiweza ukimbia hatari.
Drones ufukuza nyani,tumbili, na wanyama wote waharibifu ikiwemo ndege waharibifu pia.
Hii ni fursa kwa vijana msio na ajira drones zimejaa tele China bei rahisi kuanzia laki 3 hadi Dar msimu wa kilimo unarudisha pesa yako na faida tele unakodiwa na wakulima kuwalindia mazao yao.
Unaiprogram sauti yeyeto uitakayo zipo sauti na vitisho vya kila namna kulingana na ndege au mnyama uwatakao kuwafukuza.
Wanakijiji wenyewe watakimbia drone
 
View attachment 2060887
Nyoka aina ya koboko anadaiwa kuweka kambi katika eneo la Mlimani City kata ya Ng'ambo manispaa ya Tabora ambapo amegeuka kuwa tishio la maisha kwa wananchi wa mtaa huo.

Katika jitihada za kumuondoa nyoka huyo wananchi walimleta mganga wa kienyeji ambaye alitamba kumuondoa nyoka huyo.

Mganga huyo Hassan Jumanne anasema alipanda juu ya mti wa muembe yalipo makazi ya nyoka huyo akiwa na chungu chenye uji wa moto ambao nyoka huyo alitoka na kuingiza kichwa kwenye uji kabla ya kumshambulia kwa kumgonga mara nne.

Mganga alizimia na kuanguka na alipopata fahamu alikimbia akiacha vifaa vyake vya uganga katika eneo hilo.

Uongozi wa kata hiyo umeanza jitihada za kuwasiliana na maliasili ili kumuondoa nyoka huyo.

Chanzo cha habari: CG FM Radio
Kuna watu wataiamini hii habar
 
Back
Top Bottom