Tabora: Nyoka Koboko amekunywa uji wa Moto, amkimbiza Mganga wa Kienyeji

Tabora: Nyoka Koboko amekunywa uji wa Moto, amkimbiza Mganga wa Kienyeji

Nimecheka kwa sauti, nimepata picha anavotoka nduki.

Yaani kazimia tu hajapata madhara ya sumu?

Bora walivoamua kuwaita wataalamu wa kisayansi....sasa wao wakaleta mganga ambaye akaamua kumuunguza kwa uji.....ha ha ha ha....nyoka hasira yake ikaishia kwake.
Yani nyoka kiboko, na uji kanywa bure na kutoka hajatoka. Yani ni mbishi zaidi ya nick
 
Kawaida nyoka wa kawaida hagongi zaidi ya Mara moja kwasababu akigongo meno hubakia je huyu kapata wapi uwezo wa kugonga mara nne?
Wapo nyoka wanaogonga meno yanabaki na anaweza kukugonga tena na tena, mojawapo ni Mamba's awe green/ black Mamba anaweza gonga zizi zima la ng'ombe
 
Ung'atwe na KOBOKO halafu uzimie !..halafu utoke nduki !..
labda ana ngozi ya nyegere.
 
Au labda ni artificial,maana kama nyoka amefikia kugida uji wa moto kama maji ya baridi huyo tutaamini ni wa kawaida mkuu??? [emoji1787][emoji1787][emoji1787]!
Mganga kawazidi akili yaani hivi baada koboko kuingiza kichwa kwenye uji wa moto sumu yake inakuwa haina nguvu kali tena kama awali japo mbinu ya mganga aliye mbwinu mbunu ilifeli maarifa tu.
 
View attachment 2060887
Nyoka aina ya koboko anadaiwa kuweka kambi katika eneo la Mlimani City kata ya Ng'ambo manispaa ya Tabora ambapo amegeuka kuwa tishio la maisha kwa wananchi wa mtaa huo.

Katika jitihada za kumuondoa nyoka huyo wananchi walimleta mganga wa kienyeji ambaye alitamba kumuondoa nyoka huyo.

Mganga huyo Hassan Jumanne anasema alipanda juu ya mti wa muembe yalipo makazi ya nyoka huyo akiwa na chungu chenye uji wa moto ambao nyoka huyo alitoka na kuingiza kichwa kwenye uji kabla ya kumshambulia kwa kumgonga mara nne.

Mganga alizimia na kuanguka na alipopata fahamu alikimbia akiacha vifaa vyake vya uganga katika eneo hilo.

Uongozi wa kata hiyo umeanza jitihada za kuwasiliana na maliasili ili kumuondoa nyoka huyo.

Chanzo cha habari: CG FM Radio
Piga picha anakimbia huku amefunga msuli
 
Kwanini waganga wote ni waislamu?
 
Back
Top Bottom