Tabora: Nyoka Koboko amekunywa uji wa Moto, amkimbiza Mganga wa Kienyeji

Tabora: Nyoka Koboko amekunywa uji wa Moto, amkimbiza Mganga wa Kienyeji

Kawaida nyoka wa kawaida hagongi zaidi ya Mara moja kwasababu akigongo meno hubakia je huyu kapata wapi uwezo wa kugonga mara nne?

Koboko black mamba ana uwezo wa kugonga hadi mara 11 na mara zote atatoa fatal venom,
Meno ya koboko ni tofauti na nyoka wengine , ya koboko yama matumdu kama syringe ,sumu inapita humo, koboko mmojq ana uwezo wa kuuwa mbuzi kadhaa kwa mara moja
 
View attachment 2060887
Nyoka aina ya koboko anadaiwa kuweka kambi katika eneo la Mlimani City kata ya Ng'ambo manispaa ya Tabora ambapo amegeuka kuwa tishio la maisha kwa wananchi wa mtaa huo.

Katika jitihada za kumuondoa nyoka huyo wananchi walimleta mganga wa kienyeji ambaye alitamba kumuondoa nyoka huyo.

Mganga huyo Hassan Jumanne anasema alipanda juu ya mti wa muembe yalipo makazi ya nyoka huyo akiwa na chungu chenye uji wa moto ambao nyoka huyo alitoka na kuingiza kichwa kwenye uji kabla ya kumshambulia kwa kumgonga mara nne.

Mganga alizimia na kuanguka na alipopata fahamu alikimbia akiacha vifaa vyake vya uganga katika eneo hilo.

Uongozi wa kata hiyo umeanza jitihada za kuwasiliana na maliasili ili kumuondoa nyoka huyo.

Chanzo cha habari: CG FM Radio
Aiseehh Mkuu hongera sana Nimechakata na kupata jibu..kajamaa kanajiuguza maumivu ..Chezeya Koboko wewe....halafu hako kaganga kamekula pesa za buree kwa kina Herode...
 
Huyo koboko mzee wangu alipata kunihadithia kwamba aliwahi kufukuzwa na huyo nyoka barabarani akitokea Kasulu kwenda Kigoma mjini mzee akiwa na gari yake Landrover 109 in 70s. Na yeye huyo mzee wangu ndiye aliyeniambia kwamba huyo sio nyoka bali ni "Shetani" [emoji1787]

Umeona eee
Yaani hii story kama ya mjomba wangu aliwahi kufukuzwa akiwa na Land Rover Arusha miaka hiyo hiyo mkuu
Ni kweli kabisa na story zinafanana

Ila huyu kiumbe ni Shetani halafu ana mbio za ajabu na akikuona anaanza kukukimbiza
Kuna documentary niliiona jamaa anahadithia akatuonyesha Koboko amekuta Simba kafa kama jana ila koboko akamgonga mara mbili kuhakikisha anakufa mara tatu [emoji23][emoji23]
 
mzee wangu aliwahi wacha pikipiki honda akakimbia kwa miguu baada ya kukutana na hiki kifaa. tuliifuata pikipiki kama watu kumi na tano umbali usiozidi 1km na tukiwa na silaha zote na hapo mzee alikuwa ana "PEN" kamashine kanapakia risasi moja moja.

tulivyorudi hatukumkuta lkn kumbe alikuwa na mipango alisumbua eneo lile kwa karibu siku tano tukafanikiwa kumuua siku ya sita.

lkn balaa tulikuja kugundua yalikuwa mawili nadhani ni jike na dume maana usiku huo mbwa kadhaa mtaani walipata dozi yake ambapo hakuna mbwa alimaliza wiki alikuwa kama anaoza huku anatembea alafu ananuka hadi inabidi mfukuze hataka kama ni wako.

lakini alipouliwa wa pili amani ndio ikatawala.
 
Ngoja niwape mbinu ya kumkamata koboko,waende police kitengo cha mbwa au kwa yeyeto mwenye yale mavazi ya kufundishia mbwa unayavaa,plus buti, helmet.kisha unamfata alipo koboko au nyoka yeyeto mwenye sumu unamkamata Akigonga kichwa anakutana na helmet, Akigonga mwilini ukutana na nguo Akigonga mguuni ukutana na buti,akitema mate ukutana na kioo,mikononi umevaa gloves za boxing.
Kama meno ya mbwa ayapenyi kwenye suti hiyo sembuse ya snake
Mbinu ya ndoo na uji ya kizamani mtakula snake bites za kutosha.

View attachment 2061048
Mkuu imekaa vizuri sana
 
mzee wangu aliwahi wacha pikipiki honda akakimbia kwa miguu baada ya kukutana na hiki kifaa. tuliifuata pikipiki kama watu kumi na tano umbali usiozidi 1km na tukiwa na silaha zote na hapo mzee alikuwa ana "PEN" kamashine kanapakia risasi moja moja.

tulivyorudi hatukumkuta lkn kumbe alikuwa na mipango alisumbua eneo lile kwa karibu siku tano tukafanikiwa kumuua siku ya sita.

lkn balaa tulikuja kugundua yalikuwa mawili nadhani ni jike na dume maana usiku huo mbwa kadhaa mtaani walipata dozi yake ambapo hakuna mbwa alimaliza wiki alikuwa kama anaoza huku anatembea alafu ananuka hadi inabidi mfukuze hataka kama ni wako.

lakini alipouliwa wa pili amani ndio ikatawala.

Balaa lake sio dogo
Halafu sumu yake inauwa mda mchache sana
Kuna cameraman mmoja alipona kwa sumu yake unaweza kum google
Tena anashambuliwa huku anarekodi

Huyu mbabe kwenye matuta kwa speed huwa anapita juu kwa hiyo usijidanganye ukasema uruke matuta yeye anapita kama anapaa
 
Mzee kuna dawa huwezi amini.
Mimi nilishashudia jamaa amegongwa na huyo kiumbe ila alipona msela.
Dawa zipo ant- venom n.k kitaalam tatizo first aid... Na pia muda wa kufika hospital... Sasa dk kumi tayari unaweza potea...[emoji35][emoji2959]
 
Sorry bro.. kuna spice mbili kma sijakosea kuna meno yanaoondoka na kuna meno yanayo Baki.. reje black mamba kama sijakosea
If an attacker persists, the mamba will strike not once, but repeatedly, injecting large amounts of potent neuro- and cardiotoxin with each strike.

skfull

FYI.
 
Kabla sijafika mbali katika kusoma habari, nilipofika hapo kwenye jina nikamkumbuka chakulia lia Mohamed Said nikaanza kucheka

Ndugu zake Mohamed Said kwenye mambo ya ajabu ajabu kama hayo ya uganga au wizi wizi ni pichu na kota
Unamkosea Mwana Mzizima[emoji41]
 
Back
Top Bottom