Tabora: Nyoka Koboko amekunywa uji wa Moto, amkimbiza Mganga wa Kienyeji

Tabora: Nyoka Koboko amekunywa uji wa Moto, amkimbiza Mganga wa Kienyeji

View attachment 2060887
Nyoka aina ya koboko anadaiwa kuweka kambi katika eneo la Mlimani City kata ya Ng'ambo manispaa ya Tabora ambapo amegeuka kuwa tishio la maisha kwa wananchi wa mtaa huo.

Katika jitihada za kumuondoa nyoka huyo wananchi walimleta mganga wa kienyeji ambaye alitamba kumuondoa nyoka huyo.

Mganga huyo Hassan Jumanne anasema alipanda juu ya mti wa muembe yalipo makazi ya nyoka huyo akiwa na chungu chenye uji wa moto ambao nyoka huyo alitoka na kuingiza kichwa kwenye uji kabla ya kumshambulia kwa kumgonga mara nne.

Mganga alizimia na kuanguka na alipopata fahamu alikimbia akiacha vifaa vyake vya uganga katika eneo hilo.

Uongozi wa kata hiyo umeanza jitihada za kuwasiliana na maliasili ili kumuondoa nyoka huyo.

Chanzo cha habari: CG FM Radio
Huu ndio ujinga na umasikini wetu

Ushirikina

Hakuna jamii shirikina iliyoendelea

Tandikeni risasi
 
Hivi watu hamuelewi? Mbona Wa TZ mnakuwa majinga na mbumbumbu kiasi hiki? Hilo ni fumbo, na si stori kama mnavyodhani. That's a code, wachache mno wameelewa. Rudia kusoma kwa makini.

Sent from my A50s using JamiiForums mobile app

Do you have to swear
Hivi hata kama ni code anaongelewa mama yako kama wewe umeelewa kwanini usiliweke wazi
Unajiona mjanja kwa kutukana watu usiowajua au unatafuta beans humu anaejua kupiga maana hamchelewi kuanza kuomba mchapwe

Anyway endelea kutafuta bwana
 
Kawaida nyoka wa kawaida hagongi zaidi ya Mara moja kwasababu akigongo meno hubakia je huyu kapata wapi uwezo wa kugonga mara nne?
Mkuu huyu nyoka ni tofauti na wengine. Nyoka Walio wengi hugonga adui mara 1 lakini huyu anaweza kugonga adui Wake Hadi mara 100. Pia baadhi ya nyoka hupambana tu pale wanapochokozwa lakini huyu akikuona tu analianzisha timbwili la asha ngedele bila kujali una madhara kwake na huwezi kumtoroka kwani anasifika kwa Kasi ya kukimbia.
 
Daah umekosea kutukana! Ila anyway, acha inyeshe tuone panapovuja!

Sent from my A50s using JamiiForums mobile app
 
Kawaida nyoka wa kawaida hagongi zaidi ya Mara moja kwasababu akigongo meno hubakia je huyu kapata wapi uwezo wa kugonga mara nne?
aliekwambia koboko anakungata na meno ni nani hicho kifaa kinainject sumu kama sindano vile na kwa kukuhakikishia unaweza ukachezea bite kama 10 hivi za fasta fasta ndo ajiskie kuchoka..
 
Mkuu huyu nyoka ni tofauti na wengine. Nyoka Walio wengi hugonga adui mara 1 lakini huyu anaweza kugonga adui Wake Hadi mara 100. Pia baadhi ya nyoka hupambana tu pale wanapochokozwa lakini huyu akikuona tu analianzisha timbwili la asha ngedele bila kujali una madhara kwake na huwezi kumtoroka kwani anasifika kwa Kasi ya kukimbia.
Kwa hiyo kwa kifupi ni nyoko mwenye uadui na mwanadamu na pia ni nyoka mchokozi huyo hafai hata kufugwa kwa hali hiyo
 
Sio kila wakati nyoka hubakiza fangs au meno kwenye mwili bali meno hubaki kama tu yalikuwa yamechoka au ugumu wa ngozi ya mnyama
Ila huwa yanaota tena na tena

Kuhusu black mamba huyu ni shetani na ana hasira za kipumbavu sana

Ana uwezo wa kugonga hata watu kumi kama wamelala mahali pamoja

Huyu katika nyoka wote namuheshimu sana
Aisee yaani hata Kama watu wamelala yeye anagonga tu ajiulizi?
 
Hii story sio kweli, koboko ivi wanamjua vizuri ? Anaweza kukung'ata hata mara kumi na huwezi chukua dakika hata 15 unakuwa ushakwenda....bila huduma kwanza.
 
Back
Top Bottom