Tabora: Rais Samia akishiriki mkutano wa hadhara uwanja wa Ali Hassan Mwinyi

Tabora: Rais Samia akishiriki mkutano wa hadhara uwanja wa Ali Hassan Mwinyi

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Mkoani Tabora leo tarehe 19 Mei, 2022.

Ria Samia yupo mkoani Tabora kwa Ziara ya kikazi kwa siku 3, tangu aanze ziara hii amefanya uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo zikiwemo barabara na pia amesisitiza katika kulinda na kutunza miundombinu, watu kuongeza thamani katika uzalishaji wa bidhaa zao na pia kuwa wabunifu na kuendeleza uchumi wa viwanda.



=======

MAKAMBA: HATUJAFANYA UWEKEZAJI, MIUNDOMBINU IMECHAKAA, GRIDI IMEZIDIWA
Changamoto kubwa ya umeme Nchini imetajwa kuwa ni kutofanyika kwa uwekezaji wa kuboresha miundombinu inayoendana na mahitaji, ndiyo maana gridi ya umeme imekuwa ikizidiwa uwezo wake wa kufanya kazi.

Waziri wa Nishati, January Makamba amesema hayo na kuongeza: “Miundombinu ni kama waya zenye urefu na unene sahihi, transfoma, vituo vya kupokea na kupoozea umeme.

“Changamoto ya umeme ipo kwa kuwa hatukufanya uwekezaji unaoendana na mahitaji kwa miaka mingi, matokeo yake mfumo wa gridi yetu umeelemewa kutokana na kuongezeka mahitaji na uchakavu.”


Hotuba ya Rais Samia uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora

Kwa kuwa leo ni siku yangu ya mwisho kwa ziara hii basi nianze kwa kushukurani kuwashukuru Mkuu wa Mkoa huu, Wakuu wa Wlaya na wananchii wa Mkoa huu wa maeneo niliyotembelea na hata ambayo sijatembelea ikiwemo viongozi wa dini kwa dua na sala na machifu wenzangu nawshukuru sana kwa kuniunga mkono tangu nimeingia hapa kwenye mkoa huu pamoja na madereva wote kwa kutuendesha kote tulipokwenda na kufika salama, pia wananchi wote wa mkoa huu nawashukuru sana kwa ukarimu mlionifanyia, wajasiliamali, wamachinga, wanawake nawashukuru kwa zawadi na ukarimu wenu.

Shughuli nilizofanya katika ziara hii zote zomeshasemwa na waziri hivyo hakuna tija ya kuzirudia ila mkoa huu wa Tabora umepiga hatua kubwa sana za kimaendeleo katika mkoa huu, nimefika maeneo mbalimbali hata kule sikonge ambako kuna barabara imejengwa na nyumba nzuri zimejengwa ambazo hazina tofauti na za mijini, hivyo hiyo ni hatua kubwa ya kimaendeleo.

Mawaziri msivunjwe maneno na watu Inawezekana kuna maneno mengi sana, lakini hampati maneno kama ninayopata mimi. Hayanivunji moyo, najenga Nchi

Mambo mengi yameshasemwa hivyo mimi nina mambo mawili, moja ni kuwa maendeleo haya ni kwa ajili yenu na hivyo ni lazima kutunza miundo mbinu hiyo, muitunze na kulinda.

Na la pili ni swala la Ajira, kwenye kila fursa ya miradi kuna kursa ya ajira hivyo mchangamkie fursa kwani mnaweza kuajiriwa kama vibarua au kujiajiri kwa kuuza maji nk, lakini pia kuna mambo mengi kama umeme nk ambayo yamesha fafanuliwa vizuri na mawaziri.

Katika ziara hii, zimebainishwa changamoto nyingi ambazo mawaziri wangu wameshazitolea ufafanuzi vizuri wameeleza kuhusu mipango ya baadaye, kwa hiyo changamoto hizo zitatatuliwa, lakini pia kuna fedha za halmashauri zinaletwa hapa nataka kusema kuwa simamieni hizo fedha zikafanye kazi vizuri kuna wanaotaka kunijaribu kuwa zipofanya kazi vizuri watapata nini sitasema hapa nini kitawakuta ila wanijaribu.

Tabora ni eneo la hifadhi, kuwepo na mipaka ya kijijini na shughuli za watu na kuwepo na hifadhi kwani tukisema tukate misitu ili kupanua maeneo ya watu tutakosa hifadhi hata kilimocha nyuki hakitakuwepo, hivyo tupunguze wingi wa mifugo isiyo na tija kwani hatutakata tena maeneo ya hifadhi hivi karibuni mpaka baadaye.

Pia kuna swalqa la mitaala kuwa haiwaandai vijana kujitegemea hivyo tunatakiwa kubadili mitaala ili vijana waweze kujitegemea na kujiajiri, nami nakubaliana na swala hili la kumtayarisha kijana aweze kukubalika kwenye ajira au kujiajiri mwenyewe na wizara inapita kuchukua maoni ya wananchi ili kuweza kukabiliana na swala hilo.

Kuna kiwanda kinajengwa Urambo cha Kuzalisha asali nami nipongeze juhudi za mkoa, na kuna fedha zinakuja hivyo asali hiyo iandikwe kuwa inazalishwa Tabora.

Swala la usalama wa chakula, niwaombe sana wana Tabora kuhifadhi sana chakula kilichopo, tumekosa mvua kwa misimu miwili hivyo tutunze chakula kilichopo maana kukosa mvua si matakwa ya mtu bali ni matakwa ya Mungu na tulivyo haribu mazingira, nimejionea kwa macho yangu njiani hali ya mazao hairidhishi ila naona viazi njiani tutunze chakula kilichopo.

Kuna hili la fedha kwenye halmashauri, fedha zinapokuja kwenyehalmashauri wananchi wajue kuwa kuna fedha zimeletwa na ni kiasi gani hakuna haja ya kuficha, matumizi chama kijue wananchi wajue ili waweze kufatilia lakini pia, waweze kujua fedha hizo zimetumikaje kama kwa kufata kanuni na sheria maana hakuna mtu anayeweza kusema fedha hizi ziende hapa zisiende hapa, kuna mabaraza ya madiwani nyinyi ndio mna mamlaka ya kuamua matumizi ya fedha maana sheria imekupeni mamlaka hivyo fedha zifuate kanuni na sheria ya jisni ya kutumia.

Kuna malalamiko ya machifu kuwa hawatambuliwi naomba muwatambue na muwashirikishe kwenye maendeleo kwani kila mtu anamila na desturi zake. Muwashirikishe katika maendeleo.

Kuna swala la Tabora Girls, kuwa nusu ya eneo lake lijengwe shule ya vipajai maalumu hilo naliacha kwenye uongozi wa hapa watajua nini cha kufanya, lakini kuna swala la mipaka ya majeshi na maeneo ya wananchi hili nalibeba nitalifanyia kazi.

Tunaposema tumeanza kukigeuza kilimo ni kwa kutoa ruzuku, na tumeanza kutoa ruzuku lakini mwaka jana hakukua na ruzuku ila mwaka huu kuna ruzuku.

Baada ya kusema haya niwashukuru wana Tabora na niseme nilikuwa na ziara nzuri sana na niwaahidi kuwa nitarudi niende kwenye wilaya ambazo sijafika, niwashukuru sana niwaage kwa kusema kazi iendelee.
 
Naona ameamua kwenda kuwasuta wana Tabora 🤣 🤣 . Rais ameamua kuanzisha ziara za kusutana siku hizi.
 
[emoji625]TABORA

[emoji414]MEI 19, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. SAMIA SULUHU HASSAN kuongea na Wananchi, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora.

#AwamuYaSitaKazini
#TunajengaTaifaLetu
#2022JiandaeKuhesabiwa
#KaziIendelee
IMG-20220519-WA0089.jpg
 
Nipo huku toka juzi, kilichonishangaza, wanafunzi wote hawakwenda shule kwa kuwa walitakiwa kwenda uwanjani wakiwa na nguo za nyumbani naona wengi hawakwenda hasa walio mbali na uwanja.Sijaelewa lengo hasa lilikuwa nini!
 
Nipo huku toka juzi, kilichonishangaza, wanafunzi wote hawakwenda shule kwa kuwa walitakiwa kwenda uwanjani wakiwa na nguo za nyumbani naona wengi hawakwenda hasa walio mbali na uwanja.Sijaelewa lengo hasa lilikuwa nini!
Nchi ngum Sana ,yani watoto wanahalisha masomo kwenda muona rais, sijui tunatengeneza taifa la namna GANI yani, nasikia siku izi naye anachopa juu,
 
Ila wamekosea kufunga baadhi ya shule leo sababu ya ziara. Raisi anapaswa kuongea na wananchi sio wanafunzi ambao hawajui chochote

Watu wazima hawaendi, na lengo ni kuonyesha kuwa rais anakubalika. Hizi siasa za kilaghai zina chembe chembe za kijamaa. Kwenye siasa za kijamaa viongozi hutengeneza Hadaa ya kujaza watu kwa shuruti kwenye gafla zao kupitia madaraka yao. Hapa wanatengeneza uhalali kuwa wako madarakani kwa ridhaa ya umma, ndio maana wananchi wamejitokeza kwa wingi, kumbe ubatili mtupu.
 
Nipo huku toka juzi, kilichonishangaza, wanafunzi wote hawakwenda shule kwa kuwa walitakiwa kwenda uwanjani wakiwa na nguo za nyumbani naona wengi hawakwenda hasa walio mbali na uwanja.Sijaelewa lengo hasa lilikuwa nini!
Mafuriko Theory😀
 
Ni vizuri Mama akifika kila Mkoa kujua shida za anaowaongoza
 
Hii Nchi imetawaliwa na Dikteta hatari kabisa kwa hiyo Mama hawatamuelewa ila Mama anakubalika na watu wenye kuelewa Nchi inakwenda wapi.
 
Ni jambo jema

Huo uwanja ulijengwa na CCM

ulijengwa kwa nguvu za wananchi enzi hizo tukiwa na chama kimoja cha siasa..

Walioujenga wengine leo hii ni CCM, CDM, ACT, Chauma nk....ULIPASWA KUWA MALI YA SERIKALI SIO MALI YA CHAMA..
 
Back
Top Bottom