TUSHIRIKISHANE TABORA: Timu ya JamiiForums yapata ajali maeneo ya Mbaoni - Urambo

Poleni sana, na ahsante Mungu kwa kuepusha maafa.
 
TAARIFA​

Tunasikitika kutangaza kutokea kwa ajali ya timu (2) ya wana Jamii Media, waliopo kwenye safari za mradi wa TUSHIRIKISHANE (JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane") iliyotokea hapo jana saa 5 asubuhi, maeneo ya Mbaoni - Urambo (Tabora). Timu hiyo ilikuwa na Meneja Uendeshaji na Mikakati wa Jamii Media, Bi Asha D. Abinallah na Afisa Miradi Bw. Ericus Kimasha.

Timu hiyo ilikuwa ikielekea Kigoma mjini ili kukutana na wenzao ambako walikuwa na ratiba Warsha, kwa ajili ya kuendeleza shughuli za Mradi wa TUSHIRIKISHANE mara baada ya kumaliza shughuli zake hizo jimboni Nzega.

Kwa sasa hali zao si mbaya sana na wapo njiani kurudi Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

JamiiForums tunatoa shukrani za dhati kwa wana Urambo kwa Ushirikiano, Matibabu, Ulinzi na Usalama uliyotolewa wakati na baada ya ajali hiyo.

View attachment 383076

View attachment 383075

View attachment 383077
View attachment 383135Jamii Media inawashukuru Sana Bw. na Bi. Banyanga, wamiliki wa Magole Pre & Primary School kwa kuwasaidia wafanyakazi wetu waliopata ajali
View attachment 383136
Jamii Media inawashukuru Afande Jonas na Afande Abdallah wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilayani Urambo kwa msaaada na huduma ya haraka kwa wafanyakazi wetu.

JamiiForums​
tunawashukuru sana kwa upendo na ushirikiano mlioonyesha kwa hao wadau wa JamiiForums, Mungu awajalie uzima pia
 
Poleni, ila nazani dereva alikuwa ni ADA.
Huwa anaendesha kwa kasi sana.
Mwambie apunguze kidogo.
 
TAARIFA​

Tunasikitika kutangaza kutokea kwa ajali ya timu (2) ya wana Jamii Media, waliopo kwenye safari za mradi wa TUSHIRIKISHANE (JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane") iliyotokea hapo jana saa 5 asubuhi, maeneo ya Mbaoni - Urambo (Tabora). Timu hiyo ilikuwa na Meneja Uendeshaji na Mikakati wa Jamii Media, Bi Asha D. Abinallah na Afisa Miradi Bw. Ericus Kimasha.

Timu hiyo ilikuwa ikielekea Kigoma mjini ili kukutana na wenzao ambako walikuwa na ratiba Warsha, kwa ajili ya kuendeleza shughuli za Mradi wa TUSHIRIKISHANE mara baada ya kumaliza shughuli zake hizo jimboni Nzega.

Kwa sasa hali zao si mbaya sana na wapo njiani kurudi Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

JamiiForums tunatoa shukrani za dhati kwa wana Urambo kwa Ushirikiano, Matibabu, Ulinzi na Usalama uliyotolewa wakati na baada ya ajali hiyo.

View attachment 383076

View attachment 383075

View attachment 383077
View attachment 383135Jamii Media inawashukuru Sana Bw. na Bi. Banyanga, wamiliki wa Magole Pre & Primary School kwa kuwasaidia wafanyakazi wetu waliopata ajali
View attachment 383136
Jamii Media inawashukuru Afande Jonas na Afande Abdallah wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilayani Urambo kwa msaaada na huduma ya haraka kwa wafanyakazi wetu.

JamiiForums​
Aaaamen God is good
 
Back
Top Bottom