Tabau ninayopata kutoka kwenye familia yangu -14
Niliendelea kutafuta kazi baadae nikajikuta Niko bunju ,ngoja nielezee hapa vizuri yaani hizi direction nilikuwa nazipata hivi ,ukienda kwenye zahanati Dr wa pale anakwambia jaribu sehemu fulani nilisikia wanatafuta mtu ,hivyo nilifika tegeta ndio nikaelekezwa kufika bunju zahanati sitoitaja , nikaelekezwa nikifika pale wanahitaji mtu ,basi nilivyofika nikakutanishwa na bosi akaniuliza uliza vimaswali pale baadae nilifanikiwa kupata kazi pale ,Dr aliyekuwepo pale alikuwa anafanya kazi muda wote alikuwa Hana mtu wa kubadilishana nae hivyo tukaelewana tuwe tunabadilishana baada ya siku tatu
Basi mm nilirudi mkuranga kujipanga nione ni namna gani naweza kufanya kazi yangu vizuri ,nilifika mkuranga usiku nikaenda kwa juma ,jamaa nikamkuta yupo fresh akanieleza kuhusu vitu vyangu alivyochukua ,alisema kwamba amevipenda atanirudishia pesa niliyonunulia ,mm nikanyamaza Wala sikumjibu kimoyo moyo nikasema Sasa wewe aliyekwambia Mimi nauza ni nani ,na Mimi nikamueleza jamaa kwamba na Mimi nimepata kazi sehemu fulani ambapo nitakuwa naenda Kila baada ya siku 3
Basi baada ya siku 3 ,niliamka saa kumi na moja alfajir na kuwahi stendi ,nilifika mbagala kwenye saa 1 hivi ,gali za makumbusho ni za kugombania yaani gali hamna nilisubiri mpaka muda wa saa 3 ,yule Dr alishapiga simu kama zote sababu nilitakiwa kumtoa kwenye saa 2 hivi mpaka muda huyo saa tatu bado sijatoka mbagara
Baadae nilipata gali la makumbusho kufika makumbusho mwendo ni uleule gali za kugombania ,basi nilifika kazini kwenye mida ya saa 7 kasoro ,jamaa nilikuta amenuna hatari ,basi Mimi nikamuelezea changamoto zangu na ninapo kaa,jamaa akanishauri kwa Nini nisihamie karibu , nikamuelekeza hata pesa niliyokuwa nayo ya akiba ilikuwa imekata hivyo kupanga sehemu ya karibu mpaka nipate mshahara,jamaa akaniuliza siku yangu uliyoipoteza unaifidia vipi nikamwambia Mimi nitakufidishia siku nzima
Basi nilipiga kazi kwa kujituma sana ,bosi alitokea kunikubali sana na hii ilitokana na wateja kunipenda ,basi baada ya kupiga kazi pale, siku moja nikapigiwa simu kutoka tandika kwamba muda wa kuajiri umefika kama sijapata kazi niende ,basi nikaangalia maslahi nikaona sitoweza kufanya kazi sehemu mbili sababu kule tandika ilikuwa ni mwendo wa shift Sasa nisingeweza kwa sababu huku nakaa siku 3 ndio natoka ,basi ikabidi nimuunganishe jamaa yangu Dr Michael ,jamaa alienda kweli alipata kazi
Nilifanya kazi japo kulikuwa Kuna changamoto za migogoro na wale manesi ila ndio hivyo hakuna kilicho chepesi
Wakati napiga kazi pale niliendelea kutafuta kazi sehemu nyingine pia ,nilibahatisha kinondoni ,hapa nilipata lakini ilikuwa inatakiwa kuingia wikiend ,basi nikampanga jamaa yangu ikawa siku za ijumaa naelekea zangu kinondoni kupiga kazi
Siku moja kule bunju bosi akaniita ,kuingia kwenye ofisi yake nikakuta Kuna jamaa pia kakaa pembeni basi nikavuta kiti
Bosi akatoa utambulisho pale ,...
Sent from my TECNO P703 using
JamiiForums mobile app