Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu-17
Nilianza safari kuelekea mwanza ,lengo ilikuwa niende kujitambulisha na ikiwezekana nilipe mahali kabisa ,nilifika mwanza mida ya usiku nikatafuta gesti kwa ajili ya kupumzika ,kesho yake nikaelekea ukweni ,tulivyofika tuliongea Mambo mengi na baba mkwe ,baba mkwe akaniambia kama upo tayari kutoa mahali tuma watu ili tuweze kuelewana nao mahali mkiweza kulipia ukiweza kulipia basi utaondoka na mke
Basi niliondoka ukweni na sikuona haja ya kurudi dar bila mke ,nikaona nimpigie baba simu, japo hakunilea nilikuwa Sina chuki nae ,pia alikuwa hanilaumu kwa kushindwa kumsaidia baadhi ya shida zake ,kesho yake ikabidi kina baba waje kwa ajili ya kuelewana mahali
Walifika mpaka ukweni ,wakaelewana kulipa ngombe na izo ng'ombe tukazibadilisha kwenda kwenye fedha ,nililipia kiasi na nyingine nikahahid kulipa taratibu ,basi nikapewa mke nikarudi nae dar kuendelea na kazi
Mke wangu pia nilimtafutia sehemu ya kufanya kazi hivyo maisha yalikuwa mazuri kwa upande wa kazi lakini kwa upande wa familia hatokuwa vizuri kwani tulikosa muda wa kuwa pamoja ,ila tulijiwekea malengo tulijiwekea malengo kwa muda
Sasa tatizo la pale mbezi wale jamaa tuliokuwa tunafanya nao kazi walikuwa ni wezi mno ila nilijitahid kusimamia nikanyoosha Mambo pesa ikaanza kupatikana
Siku moja siku ya sababa nilienda uwanja wa sababa kwenda kuosha macho ,basi katika kutembea kwangu nikakuta simu ya ofa kutoka Vodacom ,simu fulani hiv kubwa iPad zilikuwa zinauzwa laki moja na kumi basi nikanunua
Wale jamaa kule kazini mbezi walivyoniona na ile simu waka organized wakaenda kwa bosi wakamdanganya kwamba ile simu inauzwa Bei kubwa sana hivyo Mimi namwibia pesa ,basi Mimi nikaona bosi anaanza kunibadilika ,Mimi ndio nilikuwa meneja nashangaa naingia kazini nakuta Kuna meneja mwingine ,basi bana Mimi nikaona hakuna kibarua Tena
Nikaenda kwenye ofisi ya bosi kuongea nae yaani bosi amenuna tu akaniuliza unanidai sh ngapi ,basi akanipa pesa zangu Mimi nikaondoka zangu
Sent from my TECNO P703 using
JamiiForums mobile app