Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu

Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu

Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu -18
Kitu ambacho bosi hakujua ni kwamba jamaa walitaka aniondoe ili wapate nafasi ya kupiga pesa ,yaani sisi watanzania sijui tutaendelea lini yaani unakuta mtu kaajiliwa sehemu badala ya kufanya kazi kwa bidii yeye anaiba ,basi bana Mimi nikaondoka zangu kwa kuwa nilikuwa nafanya kazi sehemu ingine Wala sikutetereka na mke wangu pia alikuwa anafanya kazi na tulioana kabisa ndoa ya serikali

Basi Mimi niliendelea kupiga kazi kinondoni bosi alinikubali sana ,pia alikuwa mtu makini sana alikuwa sio mtu wa kukurupuka huwezi kumsinich mwenzio ukategemea atafukuzwa kazi sana sana akiona kutoelewana kumezidi anawaita pamoja suluhi inapatikana kazi zinaendelea

Basi ilipita kama miezi mitatu hivi Niko kwenye mishe zangu ubungo nikakutana na bosi wa mbezi ,nikamsalimia fresh tu sikuwa na chuki nae ,basi bosi akauliza siku hizi unafanya wapi kazi , nikamwambia nafanya kazi sehemu nyingi tu tofauti tofauti , akaniambia kwamba Nina maongezi na wewe tutafute siku tuongee kwa kirufu ,Mimi nikampanaga jumanne jioni siku hiyo ilikuwa alhamis

Siku ya jumanne ilifika bosi akanipigia simu akaniambia yupo makumbusho niende kuongea nae ,basi Mimi nikapanda zangu daladala zile zinazotoka mabibo zinaenda makumbusho

Nilivyofika makumbusho bosi alikuwa amebaki gali lake pembeni ,nikaingia ndani ya gali tukaelekea restaurant moja hivi nyuma kidogo ya makumbusho stend ,bosi akaniambia niagize chochote

Msosi ulivyofika nikaendelea na msosi uku tukipiga story na bosi ,bosi akaniambia ameshindwa kuendesha ile dispensary ,ameamua Mambo mawili kuifunga au kutafuta mwekezaji

Lengo la kuniita pale ili nimsaidie kutafuta mtu wa kubinafsisha ,basi Mimi nikamuuliza kwani wewe unahitaji malipo ya sh ngapi kwa mwezi ,akaniambia mil 3 ,hapo kila kitu ni chake kasoro dawa tu na vifaa tiba ndio utakuwa unanunua pembeni

Nikamwambia kwa Sasa hivi Nina uwezo huo kukilipa hiyo mil 3 kwa miezi mitatu mfululizo bila kutetereka kama vipi nibinafsishie Mimi

Mzee akasema hakuna shida ilimradi tu awe anapata malipo yake ,Mimi nikamwambia lakini inabidi tuandikishiane mkataba ,mzee akasema hakuna shida

Ukweli hiyo pesa sikuwa nayo ila nilitaka anibinafsishie nilijua pale siwezi kukosa hiyo pesa ,pia matatizo ya pale nilikuwa nayafahamu ,mzee alikuwa anawalipa watu mishahara mikubwa sana na bado wakawa wanaiba sana ,pia site ile ilikuwa nzuri sana yaani kulikuwa Kuna wateja sana

Mbinu ya kwanza pale nilipanga kuwaondoa wafanyakazi wote wenye mishahara mikubwa
Mbinu ya pili ni kwenda kwenye maduka ya wahindi kukopa dawa

Basi mzee akaniambia kesho kutwa niende akanikabidhi ,kesho kutwa ilivyofika mzee akaitisha kikao Cha wafanyakazi wote akawaambia ameamua kubinafsisha hospital kwa bwana assassin eagle ,hivyo mtafanya makubaliano mapya na bwana eagle

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Wakuu muda huu wa mwanzo wa mwezi ni muda wa kufunga report za mwezi uliopita hivyo nimebanana kidogo ,mungu akiijaalia jumatatu nitakuwa nimemaliza , tutaendelea na bandika bandua ,pia kesho nitajitahid nitume moja baada ya hapo ni bandika bandua

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
Ongeza japo moja
 
Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu -19
Ili kuweza kuwakamata vizuri nikawaambia naomba muandike barua za msombi upya ,walivyoondoka nikawaita watatu tuliokuwa tunaelewana nao kipindi kile kakini pia walikuwa hawana mishahara mikubwa ,kule nilipokuwa nafanyia kazi niliomba ruhusa ya wiki mbili
Baadae nikaenda kwenye barua za watu walizokuwa wanaomba ajira ,nikatafuta wale maatendant wa bei chee ,nikawaita kama 6 hivi ukijumlisha na wale 3 wanakuwa 9 na mimi mwenyewe wa kumi ,hao ndio wakawa watu wa permanet

Walivyofika wale sita nikawa nawafanyia interview ya uelewa wao kuna wawili niliwapenda sana hawa ndio nikawafanya mameneja

Baadae wale mabinti wote nikaanza kuwapiga msasa wa kazi ,kituo kilikuwa hakina dawa ,nilienda kwa wahindi kariakoo huko tulikuwa tunachukua dawa zamani kipindi kile bado niko hapo kazini ,jamaa wakakataa kunikopesha wakasema mzee aliacha kulipa deni la laki nane ,nikawaambia wakikubali kunikopesha hata hilo deni nitalipa

Basi nilichukua mzigo mkubwa sana ,ila sasa yule mzee akawa ananizungusha kusaini mkataba ,nikajua hapa ipo siku atanibadilika ila ngoja nicheze na muda tu

Aise mambo yangu yalinyooka sana madeni yote kwa wahindi nililipa nikawa na nunua keshi

Wale waliokufanyia figisu ukafukizwa uliendelea nao au uliwatema?
 
Aiseee hongera sana,we mpambanaji sana

Kuna maMD wakipita hapa wanaona wivu hadi wanaanza kusema ni chai,wanashangaa CO kuweza kufanya yote haya tena kwenye jiji la watu
 
Uendelezaji wako wa stori ni mzuri hauchukui mda kuleta vipande kuna watu humu miendelezo ya stori zao unaikuta baada ya kubonyeza next hata mara 6 huwa ni usufumbufu wa hali ya juu mno
 
Back
Top Bottom