Half american
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 38,283
- 97,793
Endelea mkuu assassin eagle
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tabia hiyo ya kuombaomba kwa ndugu mwenye kazi ilizaliwa Kigoma, ikakulia Tabora na kwa Sasa imejichimbia umakondeni.Watanzania wajinga sana wakati unatafuta wa kukusomesha kila mmoja kimya. Sasa umepata ajira kila mjinga anaejiita ndugu anakuja kuomba msaada. Nawe kiazi una saidia wakati wewe mwenyewe una shida kibao. Ndio maana hatuwezi kwenda mbele kwasababu tuna mizigo yetu na tunabeba na ya wenzetu pia.
Eagle assassin njoo malizia huko
Hayo matatizo itakua ni wajomba tu. Wajomba kwa kiherehere hawajambo.Leo nitaweka muendelezo ,bandika bandua nilipata matatizo kidogo
Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
Daaahhh,naweka kambi hapa mkuuu,inasikitisha sana!Mimi ni kijana nilizaliwa mwaka 88 Mwanza mjini, tuliishi kwenye nyumba ya familia ile nyumba tuliishi familia mbili babu alikuwa na wake watatu hivyo pale walekaa Bibi zangu wawili na watoto wao ambao Kila Bibi alikuwa na watoto Saba Kila mtoto alikuwa na watoto wake pia hivyo waligawana vyumba, Bibi mwingine yeye hakuzaa, japo babu alikuwa na nyumba nyingine tatu.
Kila Bibi alikuwa amepewa nyumba moja na nyumba hizi zilikuwa zimejengea mitaa tofauti, kwa kifupi maisha hayakuwa mazuri pale tuliishi kigumu gumu, uwezo wangu darasani pia haukuwa mzuri japo nilikuwa siwi wa mwisho mwaka 2000 walielewana wauze ile nyumba sisi tulienda kuishi na Bibi yetu ambae alikuwa ameacha chumba kimoja katika ile nyumba waliogawiwa, vyumba vingine walikuwa wamepangisha Kodi watoto ndio waliokuwa wanachukua yeye hakupewa kitu.
Bibi yangu alikuwa mpole sana, watoto wa kiume ndio walipanga pembeni watoto wa kike walikaa na mama yao pamoja na wajukuu wale wa kiume pia kula walikuwa wanakula pale kwa bibi ,Bibi yangu alikuwa anajishughulisha na biashara ndogo ndogo aliweza kutulisha wote na matumizi madogo madogo alikuwa anatupatia ,kwakweli maisha Yale yalikuwa yananiumiza sana yaani kulala ni tabu wajukuu wengi mna lala mpaka uvunguni nilijaribu kwenda kwa mzee wangu kukaa sababu yeye alikuwa na nyumba kubwa tu ,lakin yule mke wake akakataa Mimi kukaa pale yule mwanamke alisusia Kila kitu akasema kama Mimi nakaa pale basi yeye ataondoka.
Baba ikabidi anifukuze ila niligoma kuondoka baadae baba akaniita pembeni kwa upole akanieleza nirudi tu kwa mama yangu akaniambia hanichukii ila Sasa hivi ni ngumu kumuelewa ila nikiwa mkubwa nitakuja kumuelewa basi bwana ikabidi niondoke zangu niende kwa Bibi tuliishi hivyo hivyo kwa tabu aise ,mwaka 2002 nilimaliza darasa la Saba sikufanikiwa kufaulu Bibi nae alikuwa ameshachoka Kila siku anaumwa baadae Bibi alishindwa kabisa kuendelea kufanya biashara ikabidi apumzike huwezi amini watoto walishindwa kumtunza kabisa yule mzee.
Itaendelea
===
Muendelezo soma Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu
tunasubiri bandua bandikaBandika bandua