Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu -18
Kitu ambacho bosi hakujua ni kwamba jamaa walitaka aniondoe ili wapate nafasi ya kupiga pesa ,yaani sisi watanzania sijui tutaendelea lini yaani unakuta mtu kaajiliwa sehemu badala ya kufanya kazi kwa bidii yeye anaiba ,basi bana Mimi nikaondoka zangu kwa kuwa nilikuwa nafanya kazi sehemu ingine Wala sikutetereka na mke wangu pia alikuwa anafanya kazi na tulioana kabisa ndoa ya serikali
Basi Mimi niliendelea kupiga kazi kinondoni bosi alinikubali sana ,pia alikuwa mtu makini sana alikuwa sio mtu wa kukurupuka huwezi kumsinich mwenzio ukategemea atafukuzwa kazi sana sana akiona kutoelewana kumezidi anawaita pamoja suluhi inapatikana kazi zinaendelea
Basi ilipita kama miezi mitatu hivi Niko kwenye mishe zangu ubungo nikakutana na bosi wa mbezi ,nikamsalimia fresh tu sikuwa na chuki nae ,basi bosi akauliza siku hizi unafanya wapi kazi , nikamwambia nafanya kazi sehemu nyingi tu tofauti tofauti , akaniambia kwamba Nina maongezi na wewe tutafute siku tuongee kwa kirufu ,Mimi nikampanaga jumanne jioni siku hiyo ilikuwa alhamis
Siku ya jumanne ilifika bosi akanipigia simu akaniambia yupo makumbusho niende kuongea nae ,basi Mimi nikapanda zangu daladala zile zinazotoka mabibo zinaenda makumbusho
Nilivyofika makumbusho bosi alikuwa amebaki gali lake pembeni ,nikaingia ndani ya gali tukaelekea restaurant moja hivi nyuma kidogo ya makumbusho stend ,bosi akaniambia niagize chochote
Msosi ulivyofika nikaendelea na msosi uku tukipiga story na bosi ,bosi akaniambia ameshindwa kuendesha ile dispensary ,ameamua Mambo mawili kuifunga au kutafuta mwekezaji
Lengo la kuniita pale ili nimsaidie kutafuta mtu wa kubinafsisha ,basi Mimi nikamuuliza kwani wewe unahitaji malipo ya sh ngapi kwa mwezi ,akaniambia mil 3 ,hapo kila kitu ni chake kasoro dawa tu na vifaa tiba ndio utakuwa unanunua pembeni
Nikamwambia kwa Sasa hivi Nina uwezo huo kukilipa hiyo mil 3 kwa miezi mitatu mfululizo bila kutetereka kama vipi nibinafsishie Mimi
Mzee akasema hakuna shida ilimradi tu awe anapata malipo yake ,Mimi nikamwambia lakini inabidi tuandikishiane mkataba ,mzee akasema hakuna shida
Ukweli hiyo pesa sikuwa nayo ila nilitaka anibinafsishie nilijua pale siwezi kukosa hiyo pesa ,pia matatizo ya pale nilikuwa nayafahamu ,mzee alikuwa anawalipa watu mishahara mikubwa sana na bado wakawa wanaiba sana ,pia site ile ilikuwa nzuri sana yaani kulikuwa Kuna wateja sana
Mbinu ya kwanza pale nilipanga kuwaondoa wafanyakazi wote wenye mishahara mikubwa
Mbinu ya pili ni kwenda kwenye maduka ya wahindi kukopa dawa
Basi mzee akaniambia kesho kutwa niende akanikabidhi ,kesho kutwa ilivyofika mzee akaitisha kikao Cha wafanyakazi wote akawaambia ameamua kubinafsisha hospital kwa bwana assassin eagle ,hivyo mtafanya makubaliano mapya na bwana eagle
Sent from my TECNO P703 using
JamiiForums mobile app