Tabu Ninayopata kutoka kwenye familia yangu -25
Tulivyorudi nyumbani nikamueleza baba mwanzo wa matatizo yote ,nikamwambia baba ngoja tu nitafute mwanamke mwingine nioe ,baba akaniambia ngoja ataongea nae
Basi baadae baba akamuita tukaanza kuongea basi akaonekana ameelewa ,baadae nikaingia ndani kunywa dawa akanipa dawa vizuri nikameza
Baadae akaniambia naomba uoe mwanamke mwingine ili akusaidie si unaona unaumwa , akaniambia kwani tokea nimekwambia hivi hujawahi kufanya maandalizi ya kutafuta mtu ,nikamwambia nilitafuta lakini bado hajanielewa ,basi akaniomba namba ya simu ya huyo Dada wakaongea kwamba ameruhusu Mimi nimuoe ,yeye atakuwa mke mkubwa halafu mwenga atakuwa mke mdogo
Baadae alivyomaliza kuongea nae akanisisitiza kwamba nihakikishe naoa ,kesho yake akawa ameondoka kurudi kazini
Baadae Mimi nikamwambia baba uyu mwanamke naona hanitaki Tena ,basi yule mke wangu alikuwa anakaa na mtoto wa shangazi yake ,Sasa uyo binti akanipigia simu akaniambia yule Dada yake siku hizi anamtu waga anakuja kulala pale nyumbani aise niliumia sana
Basi baadae baba aliondoka Mimi nikabaki pale na braza na wale watoto wa Dada yangu ,baadae nikafanya process ya kumuoa yule mwanamke ,niliona nichague mtu ambae hajasoma
Bado ndoa changa nikapata uhamisho wa kuhamia wilaya ingine uhamisho kutoka kwa RAs ,basi mke wangu alivyosikia nimeoa ndio ikawa tiketi ya kuniacha
Akawaambia kwao kwamba amenikuta nimeshaoa ndio maana ameamua kuniacha ,kumbe ile kunilazimisha kuoa alitaka apate sababu ya kuniacha
Unajua Kuna kipindi kaka yangu mtoto wa mama mkubwa alijiua kwa sababu mke wake ambae alizaa nae watoto wawili alimkataa ,japo nilikuwa nahuzunika lakini nilikuwa nishangaa ni kwa Nini braza ajiue wakati wanawake wapo wengi
Aise usiombe ikakukuta yaani hauoni another option Zaid ya hiyo ya kujiua ,
Yule mwanamke niliemuoa alikuwa single mother wa watoto watatu ,nae sijui alikuwa na mental trauma alikuwa ni mkorofi sana anapenda kugombana yaani ukimkosea kidogo tayari makofi
Sasa nikaona uyu tunaweza Kuna kuumizana tulibahatika kupata nae mtoto mmoja wa kike ,lakini baadae ilibid niachane nae
Mwaka huu nimeoa mke mwingine naomba mungu sana anijaalie nidumu na uyu,
Baadae yule mke wangu wa kwanza alinitafuta na kuniomba msamaha ilikuwa bado sijaoa uyu wa tatu lakini nikaona haina haja ya kuwa na mtu asie na msimamo
Ndio maana nikaona nioe tu mtu mwingine
Sasa tabu ninazopata kutoka kwenye familia yangu ni ;-
1 wazazi na ndugu hawaniongelei vizuri pindi ninapo oa ,mke wa kwanza waliongea Mambo mengi sana hasa mama
2-hata ukitoa msaada hawathamini siku ukiombwa na ukawa huna basi ni maneno mabaya mabaya wanakuongelea
3- mama Sasa hivi ameshazeeka lakini bado anang'ang'ania kufanya zile shughuli za uvuvi Kila siku ni kupoteza pesa ,anahitaji nimnunulie mashine lakini Mimi naona ameshachoka halafu Kuna wadogo zangu wapo chuo nikinunua hiyo mashine nitashindwa kuwasapoti
4 - nimeoa mke wa tatu ,mama alitoa maneno mabaya sana but Sina Cha kufanya Zaid ya kumshukuru mungu
Kule nilipohamishwa nilitengeneza mazingira mazuri sana lengo langu ni kufungua kampuni
Ambayo itakuwa ina deals with
1 .Agroproduction (kilimo na ufugaji )
Yaani na Lima nafuga pia nakuwa na mashine za kusanga na kukoboa halafu nafunga kwenye viroba nauza
2.viwanda vidogo vidogo kama mikate na mashine ya kuprocesa ngozi
3.usagirishaji (magari ya abiria
4.duka la dawa , zahanati na maabara
5.maduka ya jumla
6 .magari ya mizigo
Naamini nitafanikiwa kwa sababu naona kabis siwezi kubadili maisha yangu kwa kazi za kuajiriwa Tena humu serikalini kulivyo na changamoto
Ndio hivyo ndugu zangu ,naombeni ushauri wenu nifanye Nini ili niweze kufikia malengo yangu
Dunia tunayoenda nayo ni ngumu sana
Mwisho
Sent from my TECNO P703 using
JamiiForums mobile app