TACAIDS: Wafadhili wa dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi ya UKIMWI wamejitoa

TACAIDS: Wafadhili wa dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi ya UKIMWI wamejitoa

Status
Not open for further replies.
Umeandika kizalendo sana mkuu.

Shukrani Mkuu .! Kwa asiyeifahamu hali halisi ya maisha ya ndugu zetu wanao ishi na VVU anaweza akasema au akashabikia au kushangilia usitishwaji wa DAWA. Huyu anayeshangilia akae akijua kuna siku yeye anaweza kuwa mmoja wa wahitaji wa hizo Dawa (Dunia duara)..!
Hizi dawa zimesaidia sana katika kuokoa maisha ya ndugu zetu, zikianza kuuzwa sijui itakuwaje yaani, watu wetu watakufa sana maana gharama ya kuzinunua iko juu sana.
Tutumie kondomu wakuu, UKIMWI upo.!
 
Jibu ni moja tu hizi dawa hazitibu ukimwi. Zinarefusha maisha. Kama zinarefusha maisha, tujiulize sisi waathirika hatuna nyege?. Kama tunanyege tunazimaliza vipi?, Je kwa kupiga nyeto au kwa kushiriki tendo?.

Tuache ujinga, narudia tena tuache ujinga.

Sent using Jamii Forums mobile app

Tuache ujinga, tuache kugongana peku peku tutumie kinga UKIMWI upo .!
 

Moshi. Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (Tacaids) imesema wafadhili wa dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi ya Ukimwi wamejitoa.

Taarifa hiyo imetolewa jana na mkurugenzi mtendaji wa Tacaids, Leonard Maboko kwenye ufunguzi wa wiki ya Ukimwi duniani uliofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Mandela vilivyopo Kata ya Pasua, Moshi mjini.

Hata hivyo, alisema mfuko ulioanzishwa na tume hiyo (AIDS Trust Fund) ulioanzishwa mwaka 2015 utasaidia kuziba pengo litakalokuwepo kwa miaka miwili.

“Wafadhili wameendelea kupungua nchini lakini huu mfuko wa ndani utasaidia kupunguza haya mapengo,” alisema Maboko.

Sasa hivi, alisema wafadhili wanatoa dawa za ARV lakini dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi wamejitoa.

Alisema mfuko huo utawasaidia Watanzania wanaohitaji dawa zilizokuwa zinatolewa na wafadhili waliojitoa.

Kwa upande wake, mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira alisema takwimu zinaonyesha maambukizo ya Ukimwi yamepungua mkoani humo kutoka asilimia 7.2 mwaka 2004 mpaka asilimia 2.6 mwaka 2018.

Aidha aliwataka wananchi kujitokeza kupima afya zao kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kujua hali za afya zao na kupunguza maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.

Kilele cha siku ya Ukimwi duniani ni Desemba mosi.

Chanzo: Mwananchi
Serikali ya Magufuli ina pesa nyingi sana, atawanunulia hizo dawa kiasi cha kutosha
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom