TACAIDS: Wafadhili wa dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi ya UKIMWI wamejitoa

TACAIDS: Wafadhili wa dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi ya UKIMWI wamejitoa

Status
Not open for further replies.

Moshi. Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (Tacaids) imesema wafadhili wa dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi ya Ukimwi wamejitoa.

Taarifa hiyo imetolewa jana na mkurugenzi mtendaji wa Tacaids, Leonard Maboko kwenye ufunguzi wa wiki ya Ukimwi duniani uliofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Mandela vilivyopo Kata ya Pasua, Moshi mjini.

Hata hivyo, alisema mfuko ulioanzishwa na tume hiyo (AIDS Trust Fund) ulioanzishwa mwaka 2015 utasaidia kuziba pengo litakalokuwepo kwa miaka miwili.

“Wafadhili wameendelea kupungua nchini lakini huu mfuko wa ndani utasaidia kupunguza haya mapengo,” alisema Maboko.

Sasa hivi, alisema wafadhili wanatoa dawa za ARV lakini dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi wamejitoa.

Alisema mfuko huo utawasaidia Watanzania wanaohitaji dawa zilizokuwa zinatolewa na wafadhili waliojitoa.

Kwa upande wake, mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira alisema takwimu zinaonyesha maambukizo ya Ukimwi yamepungua mkoani humo kutoka asilimia 7.2 mwaka 2004 mpaka asilimia 2.6 mwaka 2018.

Aidha aliwataka wananchi kujitokeza kupima afya zao kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kujua hali za afya zao na kupunguza maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.

Kilele cha siku ya Ukimwi duniani ni Desemba mosi.

Chanzo: Mwananchi
Kama anavyofanya kwa Corona

Muda si mrefu yule Mjinga Bichwa Kubwa atajitokeza kutangaza hakuna Ukimwi Tanzania...

Pumbavu sana yan
 
Bora waende. Ni aibu kuendelea kupokea msaada wa ARVs pamoja na condoms. Magufuli na regime yake sasa wafill hili gap. Hakuna namna nyingine
Yaani tuache kujenga standard geji na stigilazi goji kwa sababu ya ninyi mlioamua wenyewe kuingia uwanjani pekua pekua? [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]... Just joking....
 
Nasema hivi: hamuwezi kuwa mnagongana peku daily harafu mnasubiri beberu aje kuwapa condoms na ARVs bure. Kama mnaweza kununua ndege kwa cash money, mnaweza kulipia condoms ninyi[emoji846]
Acha ukatili jombaa, hiyo ni ajali kazini banaaaa... Si unajua tena mambo ya pale kati patamu?
 
Hahaaaa kmmk
Sisi ni matajiri hakuna shida, tunajenga SGR, Bwawa kubwa la kufua umeme wa megawati 2000+, tumenunua ndege 11, mbali na ujenzi wa vituo vya afya, nk hivi vyote ni fedha za ndani nini dawa za magonjwa nyemelezi!!

Maboko awe makini kusema ni miaka miwili tu
 
Kitakachofuatia ni serikali kuomba mkopo wa dharura WHO kushirikiana na World Bank ili kuokoa maisha ya waathirika.
Hahaaa hatuombi mikopo tutafanya maombi taifa litanusurika pia serikali itatoa agizo waathirika wote wapigwe nyungu
 
Hali ni njema ila sehemu kubwa ya Dawa hizi hupatikani kupitia mifuko ya wahisani kama hao USAIDS na UK AIDS na mashirika mengine. Sasa kama wahisani wanajitoa unadhani itakuwaje juu ya upatikanaji wa dawa Mkuu. Na kuna kipindi baadhi ya wagonjwa walikuwa wanakosa hizi za dawa za magonjwa nyemelezi na baadhi uwezo wao kifedha haukua mzuri kitu kilichopelekea baadhi ya wagonjwa kutoonekana tena kwenye vituo kuja kuchukua dawa ambayo inaacha maswali labda huyu mtu alivuta au alihama kituo.
Lakini hoja yangu hasa ni kwamba, wahisani hawa tunaowaita mabeberu wamekuwa msaada mkubwa sana kwa jamii yetu hasa watu wanao ishi na VVU. Sasa hizo dawa zikianza kukosekana kwa msaada maana yake anapaswa ajinunulie mwenyewe. Ni changamoto kubwa sana na ukizingatia watu hawa baadhi yao Afya zao zinakuwa zimedhoofika hata kazi za kujiingizia mia mbili mia tatu wengine wanakuwa hawawezi . Mungu aibariki Tanzania na viongozi wake.
Umeandika kizalendo sana mkuu.
 
Mungu aliyetuponya na CORONA hatatuacha!!!!
Walitutabiria mizoga kuzagaa!!! MUNGU amekuwa upande wetu!!!

bado MUNGU yuleyule tumtegemeaye YU HAI!!!

NB: wewe upingaye nguvu za Mungu kwa kejeli na kutamani mabaya yatupate nina neno moja kwako!! UTUBU
 
Mungu aliyetuponya na CORONA hatatuacha!!!!
Walitutabiria mizoga kuzagaa!!! MUNGU amekuwa upande wetu!!!

bado MUNGU yuleyule tumtegemeaye YU HAI!!!

NB: wewe upingaye nguvu za Mungu kwa kejeli na kutamani mabaya yatupate nina neno moja kwako!! UTUBU
Shida uzinifu dhambi hapo Mungu lazma akae mbali
 
UKIMWI,mbona kama unachukuliwa simple? Jamii imesahau adha za wagonjwa wa UKIMWI? Sasa kama dawa zitaadimika hali itakuwa mbaya,wagonjwa wengi watakufa mapema
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom