Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Watu wametumia na wameishi miaka 20+, ukiwa mwathirika acha kunywa dawa uzikwe siku chache zijazo au kunywa dawa uwe na uhakika wa 20+ years.Zinasababisha liver, kidney na heart failure, no research, no right to speak
Watu wasije wakaanza kupukutika kama mende tu.Mungu atunusuru kwa hili
Magonjwa nyemelezi kama yapi?mkuu cio arv. hizo bado ztaendelea kuletwa. walizokata ni za magonjwa nyemelez
Pneumonia na TBMagonjwa nyemelezi kama yapi?
unadhan wanafill gap kama unavyofill udongo kuziba shimo? hadi serkali ishushe matumizi waishi kawaida. kitu ambacho si rahis hivyo.Bora waende. Ni aibu kuendelea kupokea msaada wa ARVs pamoja na condoms. Magufuli na regime yake sasa wafill hili gap. Hakuna namna nyingine
Uhakika wa kufa kwa Liver failure, kidney failure na heartfailure, ndio uhakika huo?Watu wametumia na wameishi miaka 20+, ukiwa mwathirika acha kunywa dawa uzikwe siku chache zijazo au kunywa dawa uwe na uhakika wa 20+ years.
Kama zingekua hatari hivyo zisingetolewa. Wana sayansi walishapima faida na hasara zake ndiyo maana zinatolewa.Uhakika wa kufa kwa Liver failure, kidney failure na heartfailure, ndio uhakika huo?
Anaekupa ARV anakupa kwa sababu zipi? Na anaekunyima dawa za magonjwa nyemelezi anakunyima kwa sababu zipi? Hivi ni kwamba nchi hii watu wamejaza funza vichwani mwao kiasi kushindwa kutafakari concept rahisi kama hii, watz mna mtindio wa ubongo au? Shida ni nini hadi upeo wa kifikiri unakuanmdogo koasi hiki??!!!Pneumonia na TB
Unadhani lengo la hao wanaokupa ni lipi? Wanakupenda sana? Tena wanakupa bure...Kama zingekua hatari hivyo zisingetolewa. Wana sayansi walishapima faida na hasara zake ndiyo maana zinatolewa.
Tanzania ni nchi huru... 😀 🤣USITUTISHEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
Nimeamua kuchangia kwasababu ningepata vijana 10 kama ninyi mngekaa jela mpaka kifo! Hivi unajua ni nini strategy ya WHO na Dunia kwasasa kuhusu maambukizi? Na trend ikoje kwenye jamii? Hivi unahisi zikisitishwa wewe utasalimika (familia yako)Hizo ARV mbona hawajaacha kutoa? Waache kutoa na hizo uone kama kuna mtu atakufa, maana hizo ARV ndio zinaua watu kwa sasa
Mtaomba kila mwaka? Hizo hela zinaletwa kila mwaka.Kitakachofuatia ni serikali kuomba mkopo wa dharura WHO kushirikiana na World Bank ili kuokoa maisha ya waathirika.
Dawa zitakuwepo ila mtazinunua kwa bei halisi.Imagine unasoma ujumbe kama huu na hujawahi kabisa kucheck afya yako kujua upo upande upi...
Wafunge kabisa ofisi zao wasepe; siyo wasitishe huduma zao halafu waendelee kuitafuna nchi ya TanzaniaSummary
Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids) imesema wafadhili wa dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi ya Ukimwi wamejitoa.
![]()
By Janeth Joseph
Moshi. Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids) imesema wafadhili wa dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi ya Ukimwi wamejitoa.
Taarifa hiyo imetolewa jana na mkurugenzi mtendaji wa Tacaids, Leonard Maboko kwenye ufunguzi wa wiki ya Ukimwi duniani uliofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Mandela vilivyopo Kata ya Pasua, Moshi mjini.
Hata hivyo, alisema mfuko ulioanzishwa na tume hiyo (AIDS Trust Fund) ulioanzishwa mwaka 2015 utasaidia kuziba pengo litakalokuwepo kwa miaka miwili.
“Wafadhili wameendelea kupungua nchini lakini huu mfuko wa ndani utasaidia kupunguza haya mapengo,” alisema Maboko.
Sasa hivi, alisema wafadhili wanatoa dawa za ARV lakini dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi wamejitoa.
Alisema mfuko huo utawasaidia Watanzania wanaohitaji dawa zilizokuwa zinatolewa na wafadhili waliojitoa.
Kwa upande wake, mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira alisema takwimu zinaonyesha maambukizo ya Ukimwi yamepungua mkoani humo kutoka asilimia 7.2 mwaka 2004 mpaka asilimia 2.6 mwaka 2018.
Aidha aliwataka wananchi kujitokeza kupima afya zao kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kujua hali za afya zao na kupunguza maambukizi mapya ya vVirusi vya Ukimwi.
Kilele cha siku ya Ukimwi duniani ni Desemba mosi.
By gazeti la Mwananchi online
Acha zako wewe... kijana yupo sahihi huyo,Nimeamua kuchangia kwasababu ningepata vijana 10 kama ninyi mngekaa jela mpaka kifo! Hivi unajua ni nini strategy ya WHO na Dunia kwasasa kuhusu maambukizi? Na trend ikoje kwenye jamii? Hivi unahisi zikisitishwa wewe utasalimika (familia yako)
Ifike pahala tuache mizaha kwenye mambo ya msingi.....
Mungu ainusuru jamii yetu....
Good night [emoji35]