Mara nyingi, watu hupenda kuiremba Marekani na barabara safi na majumba makubwa.
Marekani kuna maisha ya kitajiri na kuna maisha duni kama ya Afrika.
Hatuwezi kuifananisha Marekani na Tanzania. Maisha ni tofauti sana kutegemea na elimu ya mtu.
Mtoa mada, kama unategemea kuajiriwa, uwe na elimu inayohitajika na waajiri. Hata kama ni daktari Tanzania, huwezi kuanza kazi bila ya ukaguzi wa vyeti vyako na kama umesona nje ya Marekani, digrii yako huenda isiwe sawa na ya Marekani mpaka ufanye course kadhaa. Hii huchukua muda.
Nakushauri uende peke yako kwanza. Nakushauri usiende Michigan, nenda majimbo ambayo yana kazi zaidi na tajiri zaidi. Michigan ipo hoi kiuchumi. Kwa kuanza, New York, California, Texas.
Nakushauri utafute kazi katika mtandao au usome kazi ziliopo katika mtandao kabla ya kwenda na usome gharama za maisha katika majimbo tofauti yanayolingana na elimu na ujuzi wako.
Tafuta kazi ambazo ni nyingi na rahisi kupata kwa elimu yako. Jisomee mwenyewe.
Maisha kokote ni magumu lakini utafanikiwa mwisho.
Kila la kheri.
Hii pia ni Marekani.