Tafadhali Magufuli: Ambao Hukuwatuma, Wakikatwa Usiwabebe!

hili kweli likifanyika na wakaachwa wafanye kazi nyingine aka raia wa kawaida itasaidia Taifa huko baadaye kwa watu kuridhika na nyadhifa walizonazo...lakini pia ni vyema tukaacha kubeba watu kwenye chaguzi zote, tuache na kuheshimu maamuzi ya wananchi iwe chaguzi za ndani, chaguzi za Nec na hata uchaguzi wa Rais tuheshimu maamuzi ya wananchi na vyama vyote vipewe uwanja sawa, hapa ndipo tunaweza kupata viongozi kiasi fulani.
 
sema mkuu kitu anachonifurahisha, ni mtu wa principle, aliwataadharisha wateule wake tena kwa msisitizo, "ridhikeni na mlichonacho, acheni tamaa" ! wakamdhihaki na kujimwambafai kuacha vyeo vya uteule na kwenda kugombea.
 
Uchaguzi huru ndani ya chama

Breaking News !


Dr. Faustine Engelbert Ndugulile ashinda kura za maoni za ndani ya chama cha CCM jimbo la Kigamboni jijini Dar es Sakaam.

Kura za maoni za wajumbe halali zilikuwa 399 hakuna kura iliyoharibika na Dr. Faustine Engelbert Ndugulile amefanikiwa kupata kura 190 za wajumbe hao wa mkutano wa wilaya ya Kigamboni..

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kutumbuliwa kwa kilichoitwa 'tamaa' isiyokubalika ndani ya CCM Mpya Bw. Paul Christian Makonda amepata kura 122.
 
Mkuu
Hii panga pangua unaielewa kweli au sie ndio hatuelewi
Mkulu asiwe na visasi asiwe na upendeleo asibane uhuru wa wanachama kwa nini aabudiwe kiasi hiki?
Kuna mazuri amefanya lakini anavyojitutumua hivi kuna siku atakosa wa kumtetea
Kwani nikuulize Mkuu wewe unaona sawa kinachoendelea ndani ya Chama?! Nauliza tu Mkuu
Kazi njema!
 
Gambo na Mnyeti wameibuka kidedea, lakini Makonda kateleza kidogo mbele ya mtu mkweli, mwenye kuzingatia maadili, weledi na taaluma zake, yaani Ndugulile ambaye unaibu waziri wake ulisitishwa wakati wa sakata la kibabaishaji juu ya COVID-19. Ni lazima watu waelewe watatu hawa ni "special candidates" hata Polepole na Bashiru wanatambua hivyo.

Ni suala la muda tu, ili kusubiri na kuwapa nafasi zao, kwa kuwa mbele ya macho ya Mwenyekiti Taifa wamefanya mambo ya kutukuka.Matokeo haya yatapitia michakato mingine ya juu zaidi ikiwemo ya mwisho kabisa ndani KK ya Taifa ya CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…