Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,256
- 44,597
View: https://youtu.be/SqkZTbIqJ4kBado sijazungumza ninavyotaka kuzungumza kweli; bado natafuta maneno sahihi. Lakini itoshe kusema kuwa walioshinda kwa kushindwa wanataka bado kushindanisha kushindwa! Yaani, wamevuruga wao, wao wametengeneza mazingira ya uharibifu, wao wameruhusu mauaji, wao wameshiriki mauaji hayo, wao hao hao wanakwepa kuzungumzia mauaji hayo, na hao hao wanataka tuamulie tuzungumzie vitu vingine vyote isipokuwa mauaji yaliyofanyika chini, kwa uwezo, na kwa maagizo yao! Walioshinda kwa kushindwa wanashindaje?
Sasa wameunda tume wao, wao wahusika wakuu wa sakata hili lote, wao ndio wana damu mikononi mwao lakini ni wao hao hao wanataka kutugawia na sisi wengine damu hizo. Yaani, wamejipaka damu halafu wanataka kutushika mikono watuambie 'mbona na wewe mikono yako ina damu!". Sasa wameunda tume ungedhani watatulia, hawataki kutulia, wanatapatapa kama walivyosema wahenga.
Wanatafuta visingizio vya kuhalalisha mauaji yale, uzuri ni kuwa tumeyaona 'live'. Hawana maelezo ya kushawishi hata mwanasesere! Wanataka tukubali tuseme "tumekusikia mkuu". Wanataka tupige makofi na kusema "serikali imesema, hoja imefungwa". Hawataki tuwe na maswali ya ziada; maswali ambayo wao kwa majibu yao wanasababisha.
Wanafikiri saluti na ving'ora vinajibu hoja! Wanafikiri misafara ya mashangingi - nafikiri siku hizi haya tuyaite 'mashangazi' inatosha kujibu hoja! Wakiingia na mashangazi yao wanataka tusimame kwa heshima (ambayo hawana tena) na tuitikie tu kama kasuku! Lakini cha kuudhi zaidi ni kuwa hawataki kuwajibika hadi hivi sasa!!
Mwigulu, mnajaribu kutafuta kuhalalisha kwanini serikali yako iliua Watanzania kwa kisingizio cha kulinda miundo mbinu; kama hiyo ingekuwa kweli.. Magufuli aliwaachia magari zaidi ya 140 ya mwendo kazi, wakati haya sita yanapigwa kiberiti mlibakia na mabasi 30 sijui; yale mia walioaharibu watapigwa risasi lini?