Tafadhali Mwigulu: Acha Ufyatu - Kuharibu Muharibu Nyie, Kuwalaumu Muwalaumu Wale!

Tafadhali Mwigulu: Acha Ufyatu - Kuharibu Muharibu Nyie, Kuwalaumu Muwalaumu Wale!

Nani wa kumuamini Mwigulu huyu?? Aliwahi kusimama Bungeni na kuapa kuwa " ana ushahidi wa Duniani na bunguni kuwa Lwakatare ni gaidi"

Maelezo yake ni ya kimkakatikujaribu kumtengenezea njia ya kutoka magic honing Mhalifu mkuu aliyetufikisha hapa. Watz siyo wajinga.
Huo ulikua ushahidi wa DUMILA na BUNGONI. Kahuni kalikokubuhu hako.
 
Hawa washenzi hawachelewi kuja kutuambia walikufa watu 12.

Kwanza hizo takwimu za uharibifu hazi make sense na zina udanganyifu mkubwa. Wame-exaggerate hizo takwimu za uharibifu ili ziendane na idadi yoyote itakayokuja kutajwa ya vifo.

Gorbachev, miaka mingi baada ya kuondoka madarakani aliwahi kusema “Sometimes, I thought, ‘maybe now is the time to use force without paying attention to blood?’ I thank – I don’t know who, myself, or God – that I never did that.”
Wanajiandaa kupiga mkwanja hawa...si watatenga hela za "matengenezo".... watapiga kama wana akili mbovu
 

View: https://youtu.be/SqkZTbIqJ4kBado sijazungumza ninavyotaka kuzungumza kweli; bado natafuta maneno sahihi. Lakini itoshe kusema kuwa walioshinda kwa kushindwa wanataka bado kushindanisha kushindwa! Yaani, wamevuruga wao, wao wametengeneza mazingira ya uharibifu, wao wameruhusu mauaji, wao wameshiriki mauaji hayo, wao hao hao wanakwepa kuzungumzia mauaji hayo, na hao hao wanataka tuamulie tuzungumzie vitu vingine vyote isipokuwa mauaji yaliyofanyika chini, kwa uwezo, na kwa maagizo yao! Walioshinda kwa kushindwa wanashindaje?

Sasa wameunda tume wao, wao wahusika wakuu wa sakata hili lote, wao ndio wana damu mikononi mwao lakini ni wao hao hao wanataka kutugawia na sisi wengine damu hizo. Yaani, wamejipaka damu halafu wanataka kutushika mikono watuambie 'mbona na wewe mikono yako ina damu!". Sasa wameunda tume ungedhani watatulia, hawataki kutulia, wanatapatapa kama walivyosema wahenga.

Wanatafuta visingizio vya kuhalalisha mauaji yale, uzuri ni kuwa tumeyaona 'live'. Hawana maelezo ya kushawishi hata mwanasesere! Wanataka tukubali tuseme "tumekusikia mkuu". Wanataka tupige makofi na kusema "serikali imesema, hoja imefungwa". Hawataki tuwe na maswali ya ziada; maswali ambayo wao kwa majibu yao wanasababisha.

Wanafikiri saluti na ving'ora vinajibu hoja! Wanafikiri misafara ya mashangingi - nafikiri siku hizi haya tuyaite 'mashangazi' inatosha kujibu hoja! Wakiingia na mashangazi yao wanataka tusimame kwa heshima (ambayo hawana tena) na tuitikie tu kama kasuku! Lakini cha kuudhi zaidi ni kuwa hawataki kuwajibika hadi hivi sasa!!

Mwigulu, mnajaribu kutafuta kuhalalisha kwanini serikali yako iliua Watanzania kwa kisingizio cha kulinda miundo mbinu; kama hiyo ingekuwa kweli.. Magufuli aliwaachia magari zaidi ya 140 ya mwendo kazi, wakati haya sita yanapigwa kiberiti mlibakia na mabasi 30 sijui; yale mia walioaharibu watapigwa risasi lini?

Mwigulu anakopy zile siasa za NAZI, na communists. Ukisema uongo mara 100 basi watu wataamini kuwa ukweli, anachojisahaulisha (ingawa anajua) ni kuwa watu wameona, maiti zipo mikononi mwao, makaburi yapo, ndugu wapo, na dunia imesikia na kuona. These are Modern times, wakati ule wa NAZI kulikuwa hakuna internet wala AI.
 
Mwigulu anakopy zile siasa za NAZI, na communists. Ukisema uongo mara 100 basi watu wataamini kuwa ukweli, anachojisahaulisha (ingawa anajua) ni kuwa watu wameona, maiti zipo mikononi mwao, makaburi yapo, ndugu wapo, na dunia imesikia na kuona. These are Modern times, wakati ule wa NAZI kulikuwa hakuna internet wala AI.
IO, wanajaribu kutumia nguvu kubwa sana kuaminisha uongo kuwa kweli..
 
Msimamo wa serikali ni kwamba "they have no part in what happenned"... kwa ufupi wanatushangaa kwanini hatuwapongezi.

Hata boss wake alisema chunguzeni kauli za vyama vya upinzani...

They are out of touch kabisa
 
Huyu kiazi mwigulu nilisha mu ignore hapa JF Kitambo

Ni waziri mkuu wa BURUNDI.
Anafoka ana hasira ya ma bus yake kupigwa kiberiti
Na bado!
 
Back
Top Bottom