Tafadhali Mwigulu: Acha Ufyatu - Kuharibu Muharibu Nyie, Kuwalaumu Muwalaumu Wale!

Tafadhali Mwigulu: Acha Ufyatu - Kuharibu Muharibu Nyie, Kuwalaumu Muwalaumu Wale!

Mwigulu ni mtu wa kua jela mda mrefu sema tu nchi za Afrika toka kipindi kile anazamini wauaji kipindi cha Chadema Arusha na mabomu na ishu ya Rwakatare huyu nashangaa kua na Waziri Mkuu ambae amewahi kua na makundi ya mauaji
Mwigulu amekuwa akipata vyeo serekali kwa sababu ya kushiriki hiyo mipango miovu. Na hakuanza sasa ni toka alipoingia kwenge siasa. Na mtu mwingine wa aina yake ni Paul Makonda. Ni lazima turudi barabarani tarehe 9 kuhakikisha hawa wauaji tunawatoa na kuhakikisha tunapata katiba ambayo haitakaa itoe nafasi kwa mtu, bali taasisi. Maana kadiri ccm inavyopata madaraka kwa mabavu, ndio watu waovu wanavyozidi kukaa mbele.
 
Mwigulu anaongea kwa kufoka. Anamfokea nani? Kama hawataki kujirudi na kukiri uhusika wa serekali katika maafa ya uchaguzi ni bora wakae kimya. Wanavyoongea wanaharibu zaidi.
Yaani..wanazingua kwelikweli
 
Samahani naomba kujua, huyu jamaa anongea kama waziri mkuu ama kama katibu mwenezi na itikadi wa CCM AU L kama yule jamaa yao Tambwe hiza na cheo Cha propaganda?
Anazungumza kwa sababu gani wakati wao wameunda tume aya kujilindia
 
Tatizo kubwa wanafikiri sisi wajinga.
Tunawachora tu
Utasikia watakuja na press nyingine na viongozi wa dini.
Binafsi nahitaji haya majibu

Nani alitoa order ya kuzimwa mtandao
Nani alitoa oda ya polisi wasio na nguo kuingia mtaani
Nani aliruhusu wanajeshi kuwa mtaani
Nani aliruhusu miili itupwe

Kwanini hakuna aliyepisha uchunguzi?
wanajua hatuamini wanancho chunguza, kwanini wasilete wengine wachuguze ili tuamini uchunguzi?
 
Wanafikiri watu wanawaogopa na hawana akili kama wao, maandamano Dec 9 ni lazima na mabadiliko ya kweli kuanzia kwenye katiba, sheria za uchaguzi na waliohusika na mauaji watawajibika ni lazima
Ngoja kwanza niende zangu kwa hanil ndo mida yake hii ya live
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Bado sijazungumza ninavyotaka kuzungumza kweli; bado natafuta maneno sahihi. Lakini itoshe kusema kuwa walioshinda kwa kushindwa wanataka bado kushindanisha kushindwa! Yaani, wamevuruga wao, wao wametengeneza mazingira ya uharibifu, wao wameruhusu mauaji, wao wameshiriki mauaji hayo, wao hao hao wanakwepa kuzungumzia mauaji hayo, na hao hao wanataka tuamulie tuzungumzie vitu vingine vyote isipokuwa mauaji yaliyofanyika chini, kwa uwezo, na kwa maagizo yao! Walioshinda kwa kushindwa wanashindaje?

Sasa wameunda tume wao, wao wahusika wakuu wa sakata hili lote, wao ndio wana damu mikononi mwao lakini ni wao hao hao wanataka kutugawia na sisi wengine damu hizo. Yaani, wamejipaka damu halafu wanataka kutushika mikono watuambie 'mbona na wewe mikono yako ina damu!". Sasa wameunda tume ungedhani watatulia, hawataki kutulia, wanatapatapa kama walivyosema wahenga.

Wanatafuta visingizio vya kuhalalisha mauaji yale, uzuri ni kuwa tumeyaona 'live'. Hawana maelezo ya kushawishi hata mwanasesere! Wanataka tukubali tuseme "tumekusikia mkuu". Wanataka tupige makofi na kusema "serikali imesema, hoja imefungwa". Hawataki tuwe na maswali ya ziada; maswali ambayo wao kwa majibu yao wanasababisha.

Wanafikiri saluti na ving'ora vinajibu hoja! Wanafikiri misafara ya mashangingi - nafikiri siku hizi haya tuyaite 'mashangazi' inatosha kujibu hoja! Wakiingia na mashangazi yao wanataka tusimame kwa heshima (ambayo hawana tena) na tuitikie tu kama kasuku! Lakini cha kuudhi zaidi ni kuwa hawataki kuwajibika hadi hivi sasa!!

Mwigulu, mnajaribu kutafuta kuhalalisha kwanini serikali yako iliua Watanzania kwa kisingizio cha kulinda miundo mbinu; kama hiyo ingekuwa kweli.. Magufuli aliwaachia magari zaidi ya 140 ya mwendo kazi, wakati haya sita yanapigwa kiberiti mlibakia na mabasi 30 sijui; yale mia walioaharibu watapigwa risasi lini?
Wanatafuta pa kutokea..
 
Kila nilimuona niffa.Nna hasira na huyu mama basi tu.
Na ninamchukia najua simpunguzii chochote ila UKWELI utaniweka huru
 
Mwigulu, mnajaribu kutafuta kuhalalisha kwanini serikali yako iliua Watanzania kwa kisingizio cha kulinda miundo mbinu; kama hiyo ingekuwa kweli.. Magufuli aliwaachia magari zaidi ya 140 ya mwendo kazi, wakati haya sita yanapigwa kiberiti mlibakia na mabasi 30 sijui; yale mia walioaharibu watapigwa
Hii sindano yenyewe hasa
 
“Guys guys guys... watu wamepoteza wapendwa wao, watu wamepoteza maisha yao… I'm sorry am being emotional “

Hapa Mwigulu akijaribu kuonesha serikali iliyoua awa watu anaowazungumzia ndio imeguswa sana na hivi vifo ila wanaoulizia idadi ni watu wabaya sana.

Nafikiri tarehe 09 December kuna somo atajifunza zaidi kuhusu watanzania wa leo.
We acha tu. Huu ni unafiki level ya juu kabisa. Kama ni elimu nadhani huu ni unafiki wa Phd
 
Mwigulu ni mtu wa kua jela mda mrefu sema tu nchi za Afrika toka kipindi kile anazamini wauaji kipindi cha Chadema Arusha na mabomu na ishu ya Rwakatare huyu nashangaa kua na Waziri Mkuu ambae amewahi kua na makundi ya mauaji

Mwigulu amekuwa akipata vyeo serekali kwa sababu ya kushiriki hiyo mipango miovu. Na hakuanza sasa ni toka alipoingia kwenge siasa. Na mtu mwingine wa aina yake ni Paul Makonda. Ni lazima turudi barabarani tarehe 9 kuhakikisha hawa wauaji tunawatoa na kuhakikisha tunapata katiba ambayo haitakaa itoe nafasi kwa mtu, bali taasisi. Maana kadiri ccm inavyopata madaraka kwa mabavu, ndio watu waovu wanavyozidi kukaa mbele.
Na naona kabisa huyu ndiye wakisalimika wanaenda kumuachia madaraka aendeleze pale mwenzake alipoishia. Mbona tutakoma.
 
Hawa washenzi hawachelewi kuja kutuambia walikufa watu 12.

Kwanza hizo takwimu za uharibifu hazi make sense na zina udanganyifu mkubwa. Wame-exaggerate hizo takwimu za uharibifu ili ziendane na idadi yoyote itakayokuja kutajwa ya vifo.

Gorbachev, miaka mingi baada ya kuondoka madarakani aliwahi kusema “Sometimes, I thought, ‘maybe now is the time to use force without paying attention to blood?’ I thank – I don’t know who, myself, or God – that I never did that.”
 
Back
Top Bottom