Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Very Simple,we njoo Unguja utapewa pesa bila tatizo.
Mbona pesa ndogo sana hizo,halafu utachagua gari ya kutumia na utapakiliwa mpaka bandarini na kuanza kutumia Dar ili wanaochonga wakukome muuza sura.
Halafu kila mwezi unakuja kuchukua mshahara bila hata kufanya kazi.Na ukitaka kuishi huku utapewa nyumba ya kuishi
Kuna watu kazi zao kuwalea watu wenye kutaka mkato wa maisha kama nyie
Naomba mnifundishe lugha ya kuongea ili uaminike kuwa unachoongea ni cha kweli. Mingetumia lugha ipi?
BAADA YA KUFANYA NINAVYOWEZA NIMEGUNDUA YAFUATAYO KWA HUYU JAMAA YETU:
1.HIYO NAMBA YA SIMU ALIYOIWEKA HAPO HATA HAIJASAJILIWA.
2.HAYUPO MKOANI MBEYA NA HAJAWAHI KUISHI NJE YA NCHI.
3.NAMBA HIZO HAZIWI HEWANI MARA KWA MARA ZINAKUWA ZINATUMIKA MARA NYINGI ANAPOWATAFUTA WATU WAKE ANAODHANI ANAWEZA KUWATAPELI.
4.ANAYO NAMBA NYINGINE YA MTANDAO MWINGINE NDIO ANAYOITUMIA NA IMESAJIRIWA.
5.NIMEFANIKIWA KUPATA IMEI YA SIMU YAKE ANAYOTUMIA KWA HIYO ANAFAHAMIKA ALIPO.
6.MFUMO RASMI WA AJIRA HAUMTAMBUI.
wakuu nitarudi kwa mengineyo.
Naomba mnifundishe lugha ya kuongea ili uaminike kuwa unachoongea ni cha kweli. Mingetumia lugha ipi?
Ungesema dhamana yako ni nini? Kama una nyumba? Kiwanja? Gari uliweke rehani. Haiwezekani ukawa huna kitu chochote kisichohamishika na uwe unataka pesa hizo kirahisi tu. Mtanzania wa kawaida asiye na uhusiano na wewe hatakuelewa, labda ndugu zako wa damu.
Kuna jamaa kule Morogoro (SUA) aliingia mkenge huu huu wa hawa matapeli, 2008. Alitakiwa alipie na alilipa Tshs million 21 kama gharama za kuhamisha pesa( dollar 3bn) kutoka benki moja kule South Africa kuja kwenye akaunti yake CRDB. Hadi leo hajapokea hela yoyote kutoka SA zaidi ya kulipa madeni (sababu pesa aliyowatumia alikopa benki) na kupata stroke. Jihadhari, chukua hatua!
Siwezi kuongea yote hayo kwa watu wasio na interest nimejieleza vema kwenye post yangu.
Kwanza pole kwa majukumu ya kila siku.Wana JF nina jukumu moja kubwa la kuhamisha hela kutoka benki moja kule Scotland UK ili nizihamishie benki ya hapa Tz tawi moja la NBC. Ni zoezi ambalo limepitia mchakato mrefu kiasi na sasa niko katika hatua ya mwisho ili hela zitumwe. Kinachonikwamisha kufikia sasa ni kwamba natakiwa kumtuma mwanaseria wangu ambaye ameshughulikia hilo suala toka mwanzo ili akasaini documents fulani zinazohusiana na uhamshaji wa hizo hela. Yaani hayo ni masharti ya benki husika kwa mujibu wa sheria za Uingereza. Kiasi cha hela ninachohitaji kwa sasa ni sh. 5m (zingine zipo).
Naomba ieleweke kwamba hiki ni kitu halisi sio utani na documents zote ninazo nasubiri tu kukamilisha kazi iliyobaki hela zituwe.Nilikuwa ninasita kuja hapa maana watu kuamini vitu kama hivi ni ngumu sana unless mnaongea ana kwa ana. Nimejaribu kitafuta hela huku Mbeya nilipo tangu novemba 2013 lakini sijafanikiwa kukamilisha na muda unaenda tu. Kifupi mimi ni mtumishi wa serikali na sina fursa yoyote ya kuomba mkopo maana nimeishatumia kiasi cha pesa kuprocess documents za kuniwezesha kumiliki hiyo hazina.
Naomba wakuu zingatia kwamba nikipata hiyo hela ni zoezi la ndani ya wiki 2 tu ili hela zitumwe. Atakayenisaidia atalipwa hela yake 5m na ziada.ya 5m jumla milioni 10. Zaidi ya hapo tutawasiliana nijue shughuli anazofanya kuna upungufu gani ili nimpe support. Kimsingi nitamfanya awe mdau wangu na kupeana ushauri wa mambo ya kibiashara.
Najua kuwa maelezo yangu yanaacha maswali fulani ya msingi sana lakini nitafafanua kwa yeyote ambaye yuko interested kunisaidia. Kinachotakiwa ni kuni PM ili tuongee biashara au nitafute kwa namba hii 0755144512. Details nitazitoa in private tafadhali. Nawasilisha
Nitaku inbox nilikuwa busy sana leo mambo yote kesho mkuu
Angalia PM mkuu, JIEPUSHE NA HAO JAMAA FASTER KABLA HAWAJAKUPIGA NYINGINE. Unajua iko hivi, zile emails zinakuwa zimeandikwa kitaalam kiasi kwamba wewe akili itakuwa inakuambia kwamba unapigwa, lakini moyo unakwambia tuma pesa, dawa ni kufutilia mbali kila kitu na kusahau. Naelewa nachokiongea.
Mmmm nahisi ni zile LOTTO za dollar million 250 ndo huwa ziko hivi kama ndio acha utajuta ndugu