Tafadhali wadau naomba mnisaidie 5m Tshs nikakomboe hazina

Tafadhali wadau naomba mnisaidie 5m Tshs nikakomboe hazina

Status
Not open for further replies.
Very Simple,we njoo Unguja utapewa pesa bila tatizo.
Mbona pesa ndogo sana hizo,halafu utachagua gari ya kutumia na utapakiliwa mpaka bandarini na kuanza kutumia Dar ili wanaochonga wakukome muuza sura.
Halafu kila mwezi unakuja kuchukua mshahara bila hata kufanya kazi.Na ukitaka kuishi huku utapewa nyumba ya kuishi

Kuna watu kazi zao kuwalea watu wenye kutaka mkato wa maisha kama nyie

Kwenye msafara wa mamba.............hawakosekani!
 
Ama kweli;
dunia ya leo kuna mjinga tena kiasi hicho;

Hapa town tu jamaa anakuazima laki mbili
na anatokomea nazo sembuse milions.
 
Naomba mnifundishe lugha ya kuongea ili uaminike kuwa unachoongea ni cha kweli. Mingetumia lugha ipi?

Ungesema dhamana yako ni nini? Kama una nyumba? Kiwanja? Gari uliweke rehani. Haiwezekani ukawa huna kitu chochote kisichohamishika na uwe unataka pesa hizo kirahisi tu. Mtanzania wa kawaida asiye na uhusiano na wewe hatakuelewa, labda ndugu zako wa damu.
 
BAADA YA KUFANYA NINAVYOWEZA NIMEGUNDUA YAFUATAYO KWA HUYU JAMAA YETU:

1.HIYO NAMBA YA SIMU ALIYOIWEKA HAPO HATA HAIJASAJILIWA.

2.HAYUPO MKOANI MBEYA NA HAJAWAHI KUISHI NJE YA NCHI.

3.NAMBA HIZO HAZIWI HEWANI MARA KWA MARA ZINAKUWA ZINATUMIKA MARA NYINGI ANAPOWATAFUTA WATU WAKE ANAODHANI ANAWEZA KUWATAPELI.

4.ANAYO NAMBA NYINGINE YA MTANDAO MWINGINE NDIO ANAYOITUMIA NA IMESAJIRIWA.

5.NIMEFANIKIWA KUPATA IMEI YA SIMU YAKE ANAYOTUMIA KWA HIYO ANAFAHAMIKA ALIPO.

6.MFUMO RASMI WA AJIRA HAUMTAMBUI.

wakuu nitarudi kwa mengineyo.

Fungua kesi kwani mahakama na polisi hawapo?
 
mkuu achana na hizo ndoto hapo umeliwa kinachosubiriwa ni utume hizo 5m waingie bar kupongezana
 
Naomba mnifundishe lugha ya kuongea ili uaminike kuwa unachoongea ni cha kweli. Mingetumia lugha ipi?

Western union ndio njia kuu ya kuhamisha pesa kwa kiwango chochote world wide.labda hizo pesa zako chafu,labda zinatoka kwa magaidi.
Hivi kwa nin usikope pale NBC,Zikija uwalipe chao?
 
Western union ndio njia kuu ya kuhamisha pesa kwa kiwango chochote world wide.labda hizo pesa zako chafu,labda zinatoka kwa magaidi.
Hivi kwa nin usikope pale NBC,Zikija uwalipe chao?

Tatizo la kukariri hilo rudi shule.
 
Ungesema dhamana yako ni nini? Kama una nyumba? Kiwanja? Gari uliweke rehani. Haiwezekani ukawa huna kitu chochote kisichohamishika na uwe unataka pesa hizo kirahisi tu. Mtanzania wa kawaida asiye na uhusiano na wewe hatakuelewa, labda ndugu zako wa damu.

Siwezi kuongea yote hayo kwa watu wasio na interest nimejieleza vema kwenye post yangu.
 
hii hadithi inanikumbusha mbali kweli, waay back in 2005, achana na hizo hadithi ni michezo ya mitandaoni hakuna kitu kama hiki...cha ajabu ni kwamba pamoja na maendeleo yote haya bado kuna watu wanatapeliwa kila siku
 
Ha ha ha haa


Nicheke niondoke.

Ila ninaswali kwako ni hazina gani hiyo? Kumbe uko mbeya? Huko pesa za nje ilikuwaje? Usije ukawa unatapeliwa kupitia fb na email.

Hivi kuna mtumishi wa serikali hakopesheki?
 
Kuna jamaa kule Morogoro (SUA) aliingia mkenge huu huu wa hawa matapeli, 2008. Alitakiwa alipie na alilipa Tshs million 21 kama gharama za kuhamisha pesa( dollar 3bn) kutoka benki moja kule South Africa kuja kwenye akaunti yake CRDB. Hadi leo hajapokea hela yoyote kutoka SA zaidi ya kulipa madeni (sababu pesa aliyowatumia alikopa benki) na kupata stroke. Jihadhari, chukua hatua!


Yaani watu tunapenda vya bure sana. Hivi mtu toka Sa akupe wewe pesa asiyeyekujua hivi hana ndugu huko? Au ye hataki utajiri? Sijui huwa tunafikiria nini?
 
Siwezi kuongea yote hayo kwa watu wasio na interest nimejieleza vema kwenye post yangu.

Hiyo ni offer, na wala kwenye offer hakuna cha kuficha, atakayeridhika ndio atakufata kwenye msg. Haya badi ni PM mimi useme dhamana yako nini. Maana ungekuwa serious usingereply hapa, na direct ungenitumia PM. Unaonyesha ubabaifu. Inakuwa sio rahisi mtu kutapelika. Jifunze mbinu za ushawishi.
 
Ngoja tusubiri,mkuu ukifanikiwa tupe mrejesho
 
Wana JF nina jukumu moja kubwa la kuhamisha hela kutoka benki moja kule Scotland UK ili nizihamishie benki ya hapa Tz tawi moja la NBC. Ni zoezi ambalo limepitia mchakato mrefu kiasi na sasa niko katika hatua ya mwisho ili hela zitumwe. Kinachonikwamisha kufikia sasa ni kwamba natakiwa kumtuma mwanaseria wangu ambaye ameshughulikia hilo suala toka mwanzo ili akasaini documents fulani zinazohusiana na uhamshaji wa hizo hela. Yaani hayo ni masharti ya benki husika kwa mujibu wa sheria za Uingereza. Kiasi cha hela ninachohitaji kwa sasa ni sh. 5m (zingine zipo).
Naomba ieleweke kwamba hiki ni kitu halisi sio utani na documents zote ninazo nasubiri tu kukamilisha kazi iliyobaki hela zituwe.Nilikuwa ninasita kuja hapa maana watu kuamini vitu kama hivi ni ngumu sana unless mnaongea ana kwa ana. Nimejaribu kitafuta hela huku Mbeya nilipo tangu novemba 2013 lakini sijafanikiwa kukamilisha na muda unaenda tu. Kifupi mimi ni mtumishi wa serikali na sina fursa yoyote ya kuomba mkopo maana nimeishatumia kiasi cha pesa kuprocess documents za kuniwezesha kumiliki hiyo hazina.
Naomba wakuu zingatia kwamba nikipata hiyo hela ni zoezi la ndani ya wiki 2 tu ili hela zitumwe. Atakayenisaidia atalipwa hela yake 5m na ziada.ya 5m jumla milioni 10. Zaidi ya hapo tutawasiliana nijue shughuli anazofanya kuna upungufu gani ili nimpe support. Kimsingi nitamfanya awe mdau wangu na kupeana ushauri wa mambo ya kibiashara.
Najua kuwa maelezo yangu yanaacha maswali fulani ya msingi sana lakini nitafafanua kwa yeyote ambaye yuko interested kunisaidia. Kinachotakiwa ni kuni PM ili tuongee biashara au nitafute kwa namba hii 0755144512. Details nitazitoa in private tafadhali. Nawasilisha
Kwanza pole kwa majukumu ya kila siku.
Humo kwenye red nina mashaka napo sana.
Kwanza huko Scotland kuna matapeli wa ki nigeria,ghana na nk ambao kazi yao ni hiyo tuu ya utapeli uliopitiliza.
Kwanza nakushauri weka kila kitu wazi ili tukusaidie.
Jee hiyo pesa wewe --------- kwa misingi ipi?nani anayekutumia hiyo pesa?babako,mamako au nani?umeshatumia kiasi gani tangu kuanza mchakato?
Kuna jamaa alishawahi kuwapelekea pesa($11,000)jamaa wa hivyo kule S.Africa kwa madhumuni ya kupata $2.6m na akapigwa mpaka passport yake,na bro wangu ndiye aliyemuhifadhi kule J'berg kwa wiki3.
 
Nitaku inbox nilikuwa busy sana leo mambo yote kesho mkuu

Angalia PM mkuu, JIEPUSHE NA HAO JAMAA FASTER KABLA HAWAJAKUPIGA NYINGINE. Unajua iko hivi, zile emails zinakuwa zimeandikwa kitaalam kiasi kwamba wewe akili itakuwa inakuambia kwamba unapigwa, lakini moyo unakwambia tuma pesa, dawa ni kufutilia mbali kila kitu na kusahau. Naelewa nachokiongea.
 
Mmmm nahisi ni zile LOTTO za dollar million 250 ndo huwa ziko hivi kama ndio acha utajuta ndugu
Angalia PM mkuu, JIEPUSHE NA HAO JAMAA FASTER KABLA HAWAJAKUPIGA NYINGINE. Unajua iko hivi, zile emails zinakuwa zimeandikwa kitaalam kiasi kwamba wewe akili itakuwa inakuambia kwamba unapigwa, lakini moyo unakwambia tuma pesa, dawa ni kufutilia mbali kila kitu na kusahau. Naelewa nachokiongea.
 
Mmmm nahisi ni zile LOTTO za dollar million 250 ndo huwa ziko hivi kama ndio acha utajuta ndugu

Hahahaa, ni jamaa anamdanganya ni mkimbizi aliachiwa mapesa na baba yake sasa anataka kuyahamisha, ameona profile yake "fb" (!!!!!!), akamwamini (!!!), kwa hiyo kinachofanyika anampa mlolongo wa gharama ili waprocess hiyo transaction ya kutoka ziliko pesa kuja kwenye akaunti yake Africa, Tanzania, Mbeya, Mbalizi branch, kwa mtu wasiyemfahamu, na pesa zenyezwe ni dollar millioni kadhaa!!!!! Hiyo hata mtoto mdogo anajua anataka kutapeliwa, nashangaa jamaa amekomaa kuwa ana uhakika nao, sijui ameanza jana kuingia kwenye mitandao?!! Nashangaa hata Moderator ameiacha mpaka leo hii!:biggrin1:
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom