Tafakari juu ya maisha ya watu mashuhuri kama Prof. Jay na uhalali wa kuomba michango ya matibabu

Tafakari juu ya maisha ya watu mashuhuri kama Prof. Jay na uhalali wa kuomba michango ya matibabu

Chura

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2009
Posts
1,385
Reaction score
2,402
Anaandika mdau kutoka Facebook, Sibezi upendo wa serikali yetu chini ya mh.@Samia Suluhu lakini hatua ya serikali kutangaza kugharamia matibabu ya ndugu Prof. Jay ni aibu kwa taifa.

Ndugu yetu Joseph Haule

1. Amekuwa msanii mkubwa hapa nchini kwa zaidi ya miaka 20 basi tuseme hakukosa 1DOM kwenye usanii wake na brand yake

2. Amekuwa mbunge kwa miaka 5 ambapo kila mwezi analipwa allowance na mshahara sawa na walau 11M kwa mwezi ambapo kwa mwaka ni 132M na kwa miaka 5 anakusanya 660M basi tuseme apate 400M.

3. Alipomaliza muda wa ubunge wake amelipwa gratitude ya takribani 200M

4. Anamiliki walau mradi wa hotel Lakini kalazwa Muhimbili hawezi kugharamia matibabu yake na serikali imeahidi kumlipia Je watanzania wangapi wanafia mahospitalini kwa kushindwa kumudu gharama za matibabu? Na hali hata wengi wao hawajawahi hata kumiliki 1M katika maisha yao yote?

Hii ni aibu kubwa kwa serikali yetu ni aibu kubwa. Hili suala limebebwa kisiasa zaidi kuliko kaliba ya utu wema.
 
Unapozungumzia hili suala limebebwa kisiasa mkuu utakuwa unakosea sababu wanaomchangia jay si wana siasa pekee kabla hata serikali haijabeba hilo jukum watu wenye mapenzi mema na jay walishaanza kumchangia ambao si wana siasa, pia serikali katika kusaidia matibabu kwa raia wake hata wewe inaweza ikakutibia tu kwa zile case kubwa kama ya jay kinachotakiwa ufuate tu zile taratibu za wizara ya afya kwani serikali kupitia wizara ya afya ndio yenye mamlaka ya kukusaidia wewe na ndio maana wapo baadhi ya wananchi husafirishwa na kwenda kutibiwa nje ya nchi kipitia wizara hii....!! kitu kingine unachopaswa kufaham kuwa Jay ni maarufu hivyo umaarufu wake ameweza kupanua wigo wa marafiki tofauti ilivyo kwa mimi na wewe, Jay anafahamika karibu na kila mtanzania kwaiyo ana nafas kubwa ya kusaidiwa tofauti na ilivyo kwangu na kwako , ameweza kuonekana hao wengine unaosema wapo wengi mpaka mtu aende akahakiki uko ma hospital lakin yeye kutokana na umaarufu wake ameweza kuonekana kwaiyo kilichofanyika kwa Jay sio kibaya sana kila mtu ana nafas yake katika jamii!
 
Wabunge wa Chadema wakistaafu wanakuwa maskini kwa sababu mishahara na posho zao zinaishia kwenye kuchangia chama.

Ndio maana Halima Mdee na wenzake wakachukua maamuzi magumu.
Kwa hiyo wabunge wa CCM wana pesa zaidi?

Ndo maana Mdee kaamua kurudi UVCCM?
 
kuna kitu kimoja naona akili zetu zina kasoro sana.

mfano na kupa :marehemu ruge familia yao inapesa na rafiki yake kusaga hapo ndo usiseme ila mbona alichangiwa na mpaka umahuti ukamkuta.

swala la mtu kuugua lisikie kwa mwenzako maana unakuta pesa inayotumika kama unazika kusiko kuwa na matumaini na kama unaroho nyepesi unaweza kukata msingi wote biashara hata kuuza vyoyote.

inafikia ukomo wa pesa umegota na kuangalia mbele maana utaweza kumudu
 
Anaandika mdau kutoka Facebook, Sibezi upendo wa serikali yetu chini ya mh.@Samia Suluhu lakini hatua ya serikali kutangaza kugharamia matibabu ya ndugu Prof. Jay ni aibu kwa taifa.
Ndugu yetu Joseph Haule
1. Amekuwa msanii mkubwa hapa nchini kwa zaidi ya miaka 20 basi tuseme hakukosa 1DOM kwenye usanii wake na brand yake

2.Amekuwa mbunge kwa miaka 5 ambapo kila mwezi analipwa allowance na mshahara sawa na walau 11M kwa mwezi ambapo kwa mwaka ni 132M na kwa miaka 5 anakusanya 660M basi tuseme apate 400M.

3.Alipomaliza muda wa ubunge wake amelipwa gratitude ya takribani 200M

4.Anamiliki walau mradi wa hotel Lakini kalazwa muhimbili hawezi kugharamia matibabu yake na serikali imeahidi kumlipia Je watanzania wangapi wanafla mahospitalini kwa kushindwa kumudu gharama za matibabu? Na hali hata wengi wao hawajawahi hata kumiliki 1M katika maisha yao yote?

Hii ni aibu kubwa kwa serikali yetu ni aibu kubwa. Hili suala limebebwa kisiasa zaidi kuliko kaliba ya utu wema.
Gharama za matibabu za Jay ni kubwa sana kiongozi kama ulimnukuu malisa anakwambia kwa week moja anatumia Milion 4 sasa huoni kama ni pesa mingi sana?

Sasa milion 4 kwa mwananchi wa kawaida ki matibabu ni pesa nyingi sana, umezungumzia kuhusu pesa alizokuwa akilipwa na hotel kimsingi bado sio point sana, unaweza ukawa na hoteli lakin watu wasile wala kulala kwenye hotel yako na usikute hizo pesa unazozisema nyingi amefanya uwekezaji kwenye hiyo hotel na hata kama hajafanya uwekezaji kwenye hiyo hoteli bado pesa zinahitaji kufanya matumizi ya kila siku au unahis hizo pesa alizokuwa akilipwa yeye alizichimbia tu kwenye kibubu?

Kwa maana ya kwamba hali yeye na familia yake, hawavai, hawapati huduma za afya, hasomeshi, hasaidii wazazi wa pande zote mbili, hamsaidii ndugu hata mmoja, hafanyi jambo lolote lile la maendelea kama vile kujenga hiyo hotel na furnuture za hotel, hajajenga, hama mradi mwingine yofauti na iyo hotel?

Kifupi kaka usim judge mtu kuhusu swala la pesa sababu kila mtu anahitaji pesa ili aweze pata mahitaji anayoyakusudia nina imani iyo pesa unayoona kama alipata itakuwa ndio inaelekea kuisha ! ni imani yangu kwamba hilo tatizo lililompata Jay ingekuwa mm na ww saa hz tungeshakufa sababu huenda iyo milion 4 ya week moja tu tungepitisha bakuli hatar kwa ndugu jamaa na marafiki na kama tungeweza kupata iyo ya week nina imani uko mbele tungekwama tu!
 
Wabunge wa Chadema wakistaafu wanakuwa maskini kwa sababu mishahara na posho zao zinaishia kwenye kuchangia chama.

Ndio maana Halima Mdee na wenzake wakachukua maamuzi magumu.
ukiongea hivyo unakosea kaka kwani mbunge analipwa tsh ngapi? na kwenye chama mtu anakatwa tsh ngapi? wapo watu wanaishi kwa mishahara mpaka ya laki 5 na hawawi maskini sasa uyo anayeishi kwa laki tano na pesa anayobakiwa nayo mbunge baada ya kukatwa na chama nani mwenye afadhali? ungezungumzia kwamba pesa inahitaji nidham kidogo point yako ingekuwa na mashiko, mi naishi moro na moro haijawahi kuongozwa na mbunge mpinzan wabunge wote walioongoza moro ni CCM sasa we fuatilia historia ya wabunge wote waliopita wengine hata sehem ya kulala hawana , wana maisha magumu hatar unakuta mbunge hata hata nyumba, mbunge hata baiskeli hana ... uyo nae utasema mbunge wa chadema? Jay ana hotel kali tu na vimiradi vingine uyo ambaye unamtolea mfano na kusema wabunge wa chadema maskini, sugu nae ana bonge la hotel mbeya town pale desdery hotel nadhan kati ya ghorofa 4 au 5 tena hotel ya kisasa uyo pia ni mbunge wa chadema , lakin maisha wanayoishi wabungu we CCM hapa moro baba ni aibu tupu sema tu sio vzr kuwataja majina lakin wanatia huruma " tena mwingine alishawahi kuwa wazir kabisa lakin leo hii ukimuona ukiambiwa huyu mzee alishawahi kuwa wazir huwez amini
 
Huo ni wivu na ni mawazo ya kimasikini sana.
Eti kwavile mtu anacheo flani ndio akipata matatizo asisaidiwe?

Watu waache wivu na roho mbaya, mtu yupo ICU anapigania maisha yake na familia yake ipo kwenye majonzi then wajinga wanahoji kuhusu hela? Pesa ni nini juu ya maisha ya mtu!
 
Kama ulishawahi kuuguza mgonjwa aliye kwenye hali kama ya Joseph Hauler utaona ni kwanini familia waliamua kuchua uamuzi wa kuchangisha.............

Jambo pekee na la msingi kwa sasa ni kuangalia mwenendo wa afya ya mpendwa wetu na sio vinginevyo.........

Malumbano na mabishano yanayoendelea sasa hayana tija zaidi ya kuonyesha kuwa ni masimango kwa mgonjwa wetu............

Joseph Haule anapigania pumzi yake chini ya uangalizi wa madaktari......tunapaswa kuvaa VIATU vyake na kumuombea na sio kubishana kuhusu malipo....na huo ndio uungwana.......
 
Prof Jay anawakilisha taifa, anapeperusha kiswahili duniani wewe unawakilisha nini.
 
gharama za matibabu za Jay ni kubwa sana kiongozi kama ulimnukuu malisa anakwambia kwa week moja anatumia Milion 4 sasa huoni kama ni pesa mingi sana? sasa milion 4 kwa mwananchi wa kawaida ki matibabu ni pesa nyingi sana, umezungumzia kuhusu pesa alizokuwa akilipwa na hotel kimsingi bado sio point sana, unaweza ukawa na hoteli lakin watu wasile wala kulala kwenye hotel yako na usikute hizo pesa unazozisema nyingi amefanya uwekezaji kwenye hiyo hotel na hata kama hajafanya uwekezaji kwenye hiyo hoteli bado pesa zinahitaji kufanya matumizi ya kila siku au unahis hizo pesa alizokuwa akilipwa yeye alizichimbia tu kwenye kibubu? kwa maana ya kwamba hali yeye na familia yake, hawavai, hawapati huduma za afya, hasomeshi, hasaidii wazazi wa pande zote mbili, hamsaidii ndugu hata mmoja, hafanyi jambo lolote lile la maendelea kama vile kujenga hiyo hotel na furnuture za hotel, hajajenga, hama mradi mwingine yofauti na iyo hotel? kifupi kaka usim judge mtu kuhusu swala la pesa sababu kila mtu anahitaji pesa ili aweze pata mahitaji anayoyakusudia nina imani iyo pesa unayoona kama alipata itakuwa ndio inaelekea kuisha ! ni imani yangu kwamba hilo tatizo lililompata Jay ingekuwa mm na ww saa hz tungeshakufa sababu huenda iyo milion 4 ya week moja tu tungepitisha bakuli hatar kwa ndugu jamaa na marafiki na kama tungeweza kupata iyo ya week nina imani uko mbele tungekwama tu!

True.
Mungu ukuletea matatizo kulingana na uchumi wako.
Thus Tanzania hatuna vimbunga,mafuriko makubwa,matetemeko makubwa
 
Hoja sio matumizi ya pesa za matibabu, hoja ni kwamba inakuwaje mtu maarufu na mwenye brand kubwa anachangiwa kana kwamba hana hela za matibabu alizopata wakati wa shughuli zake za kisanii na kisiasa? Wakati mwingine inashangaza na ni aibu watu maarufu kuchangiwa wakati inaaminika wana fedha za kutosha
 
Wabunge wa Chadema wakistaafu wanakuwa maskini kwa sababu mishahara na posho zao zinaishia kwenye kuchangia chama.

Ndio maana Halima Mdee na wenzake wakachukua maamuzi magumu.

Bwashee, acha umbeya. Hao Chadema wakija kukuvalisha dera utakubali, utakataa?

Au ulitaka hicho chama chao kijengwe na ccm? Au unadhani na wenyewe walikwapua majengo ya serikali, viwanja vya wazi na vile vya michezo kama ccm?
 
Anaandika mdau kutoka Facebook, Sibezi upendo wa serikali yetu chini ya mh.@Samia Suluhu lakini hatua ya serikali kutangaza kugharamia matibabu ya ndugu Prof. Jay ni aibu kwa taifa.
Ndugu yetu Joseph Haule
1. Amekuwa msanii mkubwa hapa nchini kwa zaidi ya miaka 20 basi tuseme hakukosa 1DOM kwenye usanii wake na brand yake

2.Amekuwa mbunge kwa miaka 5 ambapo kila mwezi analipwa allowance na mshahara sawa na walau 11M kwa mwezi ambapo kwa mwaka ni 132M na kwa miaka 5 anakusanya 660M basi tuseme apate 400M.

3.Alipomaliza muda wa ubunge wake amelipwa gratitude ya takribani 200M

4.Anamiliki walau mradi wa hotel Lakini kalazwa muhimbili hawezi kugharamia matibabu yake na serikali imeahidi kumlipia Je watanzania wangapi wanafla mahospitalini kwa kushindwa kumudu gharama za matibabu? Na hali hata wengi wao hawajawahi hata kumiliki 1M katika maisha yao yote?

Hii ni aibu kubwa kwa serikali yetu ni aibu kubwa. Hili suala limebebwa kisiasa zaidi kuliko kaliba ya utu wema.
Harafu Kuna kenge serikalini wanatoka mapovu kuhimiza vijana wakitoka vyuoni wajiajiri,wakati huyu Mbunge amekuwa kwenye ajira(ubunge)kwa miaka mitano lakini na pesa yote aliyolipwa ameshindwa kujijengea mifumo imara ya uchumi,mpaka anakuwa omba omba Ili atibiwe
 
Back
Top Bottom