Tafakari juu ya maisha ya watu mashuhuri kama Prof. Jay na uhalali wa kuomba michango ya matibabu

Mwandishi ana akili fupi sana. Fupi mno. Kwanza familia haijatoka na kusema wameshindwa kumtibu. Ni watu na mapenzi yao waliamua kufanya. Wale wa serikali wakaona wajipatie umaarufu kwa kujiingiza humo. Sasa unakuja na porojo za kukadiria mapato ya mtu hivi unajua majukumu yake? Unajua wanaomtegemea ni wangapi? Unajua hali za kiuchumi za watu wanaomzunguka? Wewe kama huwezi toa acha wanaochangia wachange. Kama tunamchangia mtu anayeoa au kuolewa kwa starehe yake iwe mgonjwa. Refusha hiyo akili angalau nusu inch uone mambo kwa maoana yake.
 
Nimepitia kiongozi, nzuri, kuna majibu yoyote legit kutoka kwa Mkapa?
mkapa sidhani kama amewahi kujibu chochote,kwanza i nasemwa hakuwahi kuhojiwa na mwandishi yeyote hapa nchini katika kipindi chote cha urais na hata baada
 
Sintamlaumu Kijana yyt atakaefilisika hata km alikuwa na Mtaji wa 200m TSHS
 
Wana hela ya kula tu, kugharamikia misiba na harusi lkn sio ugonjwa, 4mln kwa wiki sio mchezo.
 
Unamchangia mtu hata awe bilionea inategemea nae mchango wake wa ali na mali kwa jamii yake,kwa mfano mimi ni mchangie mtu kama polepole au bashiru au makonda au ali hapi au sirro ptyuuuu!!
 
Ni jambo la kustaajabisha sana
 
ni upumbavu kumchangia aliye nacho,
kama nina 100k, nawezachangia kadhaa walioshindwa na matibabu ya 20k ( ambayo serikali imewaignore ) kisha kupoteza maisha
Japo mi kiukweli sijawahi kuchangia watu km hao na sitachangia!
 
Hukujibu alichoandika mwandishi. Hata ukatae kinachosukuma serikali kuchangia ni siasa. Jay hakufuata taratibu za wizara kuimba kutibiwa na hatibiwi nje, serikali imebeba mzigo wa gharama zake. Kisiasa.
Ila ukweli unabaki ni kuwa watu wanapata hela lakini zinaishia kwenye matumizi. Umaarufu ni kitu kimoja, kuwa na hela ni kitu kingine.
 
kuna kipindi flan utawala wa jakaya kikwete, mzee King Majuto alishawahi kupatwa na maradhi hivyo Rais Kikwete akaamua kubeba jukumu la kumsaidia mzee Majuto sasa nakuuliza tena ndugu yangu zile nazo zilikuwa kick za kutafuta mtaji wa kisiasa? au utasema jamakaya alibeba lile jukumu kwa sababu ya kisiasa? sasa kwa mfano angesaidiwa na mtu kama MO au BAKHRESSA mngesemaje? au mngesema wamelichukulia hilo jambo kibiashara zaidi sababu wao ni wafanya biashara?
 
Hii hoja yako ndio msingi wa tafakuri ya mleta mada ila watu wengi wanamrushia matusi kana kwamba hataki Jay achangiwe.

Hoja namba mbili ni kwamba kwa umaarufu na utumishi wake kwenye mhimili wa bunge,Jay ni miongoni mwa watanzania wachache wanaovuta mpunga mrefu sana kibongo bongo. Bila kujali kama amekula bata au amewekeza,swali linabaki ni watanzania wangapi wanaopoteza maisha kwa kutokuwa na uwezo wa kupata huduma bora za afya endapo Jay ameshindwa pamoja na ukwasi wake wote huo?

Mleta mada hadhamilii kumponda Jay bali kuhoji uwezo wa umma mkubwa wa watanzania kumudu gharama za afya kulingana na ufinyu wa vipato vyetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…