Watu watahamasishwa tu waone kulipa Kodi ni haki yao ya lazima km kuvuta hewa! kula chakula ili uishi, ni lazima. watajipeleka wenyewe, kazi hii ya uhamasishaji ifanywe na vijana wapole wazuri wa sura, ke'' kwa me'' wanao ongea kwa lafudhi tamu na rafiki. nasema vijana sababu kundi hili ndiyo zuri kwa biashara yeyote, km Bar, Ndege, Hotel nk!
watoe ushauri na msaada kwa wafanya biashara, siyo km sasa wanatembea na Mgambo, Police km ugomvi, kufunga maduka ya dawa. mtu akiona Mgambo tu hana amani moyoni.
Kodi ni gharama za maendeleo ya huduma ninayo patiwa mimi mwananchi. Badilini neno kuendesha huduma za serikali, sijui kodi ya kichwa no! ni maneno ambayo si rafiki! sema ''Afya yako mwanana yaja malangoni pako leo'' na kweli umpe hiyo Afya uzuri.
Kifupi watu wenyewe watamani yale sirikali inayowafanyia faster na kwa ufanisi, hata akikwama kuipata hiyo huduma usimzodoe ongea nae taatibu aseme alipo kwama!!!
watu Million 67 siyo wengi kuwapa huduma mpaka mlangoni. hata ukiwaambia nitakuwa nakuoshea viatu vyako kila siku, atatoa hela hiyo! siyo ukajenge uwanja wa ndege chato kibabe! walahi lazima wakuibie na wewe utumie nguvu kuwapata.