Uchaguzi 2020 Tafakari ya Kina: Tundu Lissu akifuta kodi ataendeshaje nchi?

Uchaguzi 2020 Tafakari ya Kina: Tundu Lissu akifuta kodi ataendeshaje nchi?

NImependa sana usomaji na uchangiaji uliofanyika.Kuna eneo inabidi kama taifa tujsahihishe
 
ndugu yangu uko sawa kabisa mfa maji haishi kutapa tapa lissu anahangaika ili kuwafurahisha watu.aonekana mwema lkn misingi ya nchi yoyote dunia ni kodi sasa yeye anataka kutuletea wafadhili hapa ili tuwe kama nairobi sasa hiv wanahaha kukabilina na amri za bwana trumb
Mmeshajua anamaanisha kodi gani inayotakiwa kufutwa ? Msiropoke tu, njooni na detailed explanation sio kufuta kodi tu.
 
Mkuu mbona uchambuzi wako unakinzana na heading au Mods wame edit?
 
Hayo yote baadae kwa sasa mziki ni mmoja tu, kuiondoa CCM madarakani ili tupate uhuru ulio na Uhuru.

Yaani kila mkoa kila wilaya kutakuwa na kijiwe ,vitavyoruhusiwa kusema chochote kile juu ya nchi yako kama inaendeshwa vibaya vizuri vijiwe au viwanja hivyo vitakuwepo kisheria kabisa, utakalosema hapo huwezi kushitakiwa wala kuguswa, tutaviita viwanja vya demokrasia kwa ajili ya siasa za nchi yetu, wananchi kutoa joto lao dhidi ya serikali iliyopo madarakani.
Hii hoja yako kwa baadhi ya nchi inatekelezwa vizuri.

Kwa nchi kama Uingereza kwenye jiji la London kuna eneo linaitwa SPEAKERS' CORNER kwa ajili ya watu kukutana na kujadili au kutoa kero zao kwa serikali na wanapatiwa ulinzi kabisa na hoja zao kufikishwa sehemu husika bila wao kubughudhiwa.

Hili limesaidia kupunguza/kuondoa jazba na manung'uniko kwa wananchi yanayo tokana na kero zinazo wakabili.
 
unakinzanaje?fafanua na wengine waelewe.
Umeuliza kwenye heading kuwa Lissu akifuta kodi ataendeshaje nchi?

Kisha katika bandiko lako umeelezea namna atavyo badili mifumo ya kodi na ukusanyaji wake ili kuifanya iwe rafiki na kutekelezeka huku ikiacha tija na manufaa kwa walipaji ama wanufaikaji wa kodi.

Kwa nilivyo elewa pamoja na baadhi ya wachangiaji pia kupitia comments zao ni kuwa heading yako in the first place imemaanisha kuwa Lissu aliahidi kuwa hatatoza kodi akiwa rais ila maelezo yanaelezea namna atavyo boresha mifumo ya kodi na kuondoa kodi kandamizi.
 
Back
Top Bottom