Wakili wa shetani
JF-Expert Member
- Nov 22, 2022
- 1,726
- 3,391
Juzi kati nilikuwa nazungumza na madogo fulani wawili kuhusu Jamiiforums. Wale madogo wakasema kuwa hawajawahi kuisikia Jamiiforums!! Nilishangaa sana, ni madogo wenye kazi na wako active kwenye mitandao ya kijamii. Yaani mtandao upo tokea mwaka 2006 hawajawahi kuusikia!!? Licha ya hayo, ukifanya search ya mambo mbalimbali ya kiswhili utakutana na links za JF. Inamaana hawajawahi kufanya hivyo!! Nikasema pengine JF si muhimu kama ambavyo members tunaichukulia.
Sasa juzi kukawa na habari ya watu kulizwa na upatu wa MTFE, nikakaa nikatafakari na kuona kuwa mtu wa JF hawezi kupigwa kirahisi na kitu kama hicho, members humu ni wasomi wanaochambua mambo kwa kina. Pia ni masikini wenye tahadhari na pesa zao na wanaopeana tahadhari hizo. Ni watu wanaoangalia mambo kwa uhalisia wake. Tafakari yangu ikanipeleka mpaka kwa madogo wale. Nikaona kuwa kwa kutoijua kwao JF wako vurnerable kwa mambo mengi sana. Kila siku tunajiuliza ponzi schemes zinapata wapi wajinga wa kuwapiga, nikagundua ni kama wale madogo.
Taarifa ni ulinzi dhidi ya mambo mengi sana. Tafakari ile ilinifanya nione kuwa JF ni muhimu kuliko tunavyoichukulia.