Tafakuri: Viongozi wanapoamuru jeshi kuua raia ni tangazo la vita? Nini hatima yake?

Tafakuri: Viongozi wanapoamuru jeshi kuua raia ni tangazo la vita? Nini hatima yake?

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
26,483
Reaction score
40,130
Narejea kusisitiza kwamba, CCM ndiyo watakaosababisha vita ya wenyewe kwa wenyewe Tanzania

Kitendo cha Hangaya kutangaza 2024 kuwa vyombo vyote vya ulinzi na usalama kujiandaa kijeshi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu 2025, lilikuwa ni tangazo la maandalizi ya vita dhidi ya raia.

Kitendo cha kutoa amri kuua raia na kuzima mitandao ilikuwa ni vita kamili ambayo inaendelea hadi sasa.

Majeshi yetu yameungana na watawala haramu katika haya
  1. Kushiriki wizi wa uchaguzi 2025
  2. Kulazimisha ushindi kwa asiyestahili
  3. Kumuapisha mhaini ndani ya kambi ya jeshi
  4. Kuua raia walioandamana na wasioandamana kwa kuwafuata majumbani kwao
  5. Kuendeleza kukamata, kutesa, kulawiti na kuua raia mpaka sasa ili kumsaidia mhaini aliyepora mamlaka ya wananchi kuchagua viongozi
  6. Kutishia na kuzuia raia kutimiza haki yao iliyowekwa na Ibara ya 18 ya Katiba
  7. Kushirikiana na kuwalinda majambazi waliojitwalia madaraka ambao wanaiba fedha na rasilimali zetu
  8. Kuratibu na kushiriki kuua majeruhi waliotokana na unyama wao wa 29 Oct+
  9. Kuratibu na kushiriki kuharibu miili za mrehemu waliowaua
  10. Kuratibu na kushiriki kuzika miili kwenye makaburi ya halaiki
  11. Na uovu mwingine mwingi....
Serikali haramu imevigeuza vyombo vyetu vya dola halali kufanya vita dhidi ya raia wa nchi hii.

Hii vita wanadhani ni lelemama, lakini watakachokiambulia ni fedheha, aibu na mwisho mbaya sana wa matendo yao.

Jeshi la polisi limegeuka kuwa la kigaidi kinyume na takwa la uanzishwaji wake.

Uzi tayari
 
Back
Top Bottom