Tafakuri ya FaizaFoxy 6: Dar Es Salaam na Tanzania ya zamani, tukumbushane...

FaizaFoxy

Platinum Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
100,246
Reaction score
123,145
Tafakuri yangu leo imenikumbusha Sana Dar ya zamani 60s na 70s.

Wale wanaoikumbuka Dar na Tanzania ya zamani tukumbushane, si lazima iwe 60s na 70s, nimeweka kigezo hicho binafsi kwani ndipo zamani kwangu. Wengine mnaweza kuweka zamani yenu.

Nnaanza na Dar kwani ndipo makazi yetu miaka hiyo na sehemu zingine Tanzania ntagusia kumbukumbu zangu huko nilipopata fursa ya kupatembelea miaka hiyo.

Dar.
Nakumbuka , viwanja vya mnazi mmoja tulipoenda kutazama sinema za tarehe 3 (Aspro) kama sikosei na nyingine ilikuwa tarehe ngapi sikumbuki lakini nadhani ilikuwa ya sabuni za Omo.

Hao walikuwa wanavuta watu wengi sana wa viunga vya Kariakoo na jirani jirani miaka hiyo kujankutazam sinema za bure huku wakifanya matangazo ya biashara zao.

Hiyo ni fungua dimba nitaendelea na mengine uzi unavyoendelea.

Karibuni nanyi mlete kumbukumbu zenu za popote mlipokuwa.
 
Mi nakumbuka uwanja wa Karume ulikuwa wa ovyo sana. Tulikuwa tukitoka zetu shule Msimbazi Boys Primary tunazama uwanjani kwa kumpa askari mla rushwa sh 50 au 100.

Ukishaingia uwanjani unakimbia sana mgambo wasikukamate unaenda kujichanganya na watazamaji wengine. Hiyo ni miaka ya tisini ndiyo zamani yangu.
 
hivi enzi za usafiri wa chai maharage kuanza ilikua ni mwaka gani?
nakumbuka kuzikutia mwishoni mwishoni.....

Sent using Jamii Forums mobile app
Miaka ya 90,siku moja nimezurula we toka obay kupitia salendar Hadi town wakati wa kurudi nikaamua kupanda chai maharage pale kariakoo mpaka Morocco,nikataka kulipa hell ya mwanafunzi tulipofika ,asee konda alinikwida nusra Nile vibao ,Ni vile nilikua mdogo akaniachia,nilijieikia aibu kweli kukabwa mbele ya umati
 
Nnakumbuka kwa mara ya kwanza, kama sikosei, kuwaona Wachina, ilikuwa hapo kidongo chekundu, walijenga banda kubwa lilikuwa na maonesho ya bidhaa na tamaduni zao.

Kitu kilichovutia watu wengi, kwa muono wangu wa enzi hizo, ilikuwa ni Jogoo la kutengeneza (kubwa kiasi) lililokuwa linawika kila baadabya muda, kokorikooooo,lilikuwa kivutio kikubwa kwa watu na hususan sisi ambao umri wetu ulikuwa bado mdogo wa kuonea ajabu kila kipya.

Kingine tulichoonea ajabu ni macho ya Wachina, tulihisi kama mstari tu umechanwa panapotakiwa kuwa macho (nahisi kama Wachina wa enzi hizo walikuwa na macho madogo zaidi ya hawa tunaowaona sasa) au labda ndiyo ilikuwa mara ya mwanzo kuwaona ndiyo nikawa na kumbukumbu hiyo.

Hilo la Jogoo wa Wachina nimelikumbuka kwani miaka hiyo hiyo nikaanza kusikia mziki, sikumbuki wa bendi ipi, kwenye radio, ukipgwa Halafu anapigs mtu tarumbeta kama Jogoo linawika Kokorikooooo kooo.

Hahahaha, Wabongo kuiga tumeanza zamani sana, nadhani na wao Jogoo la kichina liliwavutia wakalipigia mziki.

Anaeikumbuka hiyo bendi anikumbushe.
 
Kulikoni umpe askari 50 au 100 wakati tiketi ziliuzwa shs 40?... noti mbili za shs 20 au noti nne za shs 10
 
Hahaha enzi hizo nadhani ulikuwa unaitwa uwanja wa Ilala.
 
Nakumbuka kupanda Basi za UDA 'hekalusi' za kibelgium kipindi hiko hata darasa la kwanza sijaanza. Around 1986's hio ndio zamani yangu
 
Wanafunzi wa Zanaki Primary School kula makoko ya wali wa Zanaki girl Secondary...

Mwalimu Ndosi Muhimbili Primary school maalufu kwa ukali na kuchapa fimbo zinazouma sana na nyingi.

Bonge la Organ Darasani Upanga Primary School.

Abdalah Mafishi mtemi wa Shule ya Olympio Primary School.

Bukaba jeba kubwa sana afu Blackiii kusoma primary school.

Raisi Mwinyi kufika Shule ya Muhimbili primary school na kumchapa bakora binti yake.

Shamba la Jela ya watoto watukutu baadae sijui walitapeliwa vipi kwa sasa ndio Hospital binafsi ya Regency hadi Leo sielewi walipata vipi ujasili .

Miaka ya 90's
 
Nakumbuka kupanda Basi za UDA 'hekalusi' za kibelgium kipindi hiko hata darasa la kwanza sijaanza. Around 1986's hio ndio zamani yangu
Nazikumbuka Ikarus, zile ndefu zikapewa jina kumbakumba.

Halafu vijana wa leo wanatuona hatujui hizi mwendokasi.

Binafsi nakumbuka kabla ya UDA ilikuwa DMT na kulikuwa na basi la ghorofa, hakuna ambae hajataka kulipanda hilo, sema enzi za hilo basi la ghorofa ilikuwa hakuna kuminyana, kama London tu.
 
Kama mtu anakumbuka mahandaki ya ardhini Mmnazi mmoja..

Na ile sauti ya tindo ikitangaza muda majira ya saa ukipiga simu za kuzungusha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…