Tafiti: Ugumba kwa wanaume unakua kwa kasi sana

Tafiti: Ugumba kwa wanaume unakua kwa kasi sana

mshamba_hachekwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2023
Posts
20,704
Reaction score
66,337
Imegundulika kua katika kipindi cha takribani miaka 50 nyuma kufikia sasa, kumekua na upungufu wa zaidi ya 50% ya manii(sperm) kwa wanaume wote duniani, na kusababisha kukua kwa kasi, kwa tatizo la ugumba kwa wanaume.
50% decrease.jpg

mbaya zaidi, upungufu huu umeonekana kua mkubwa zaidi kwa wanaume wakiafrika, yaani 73% ndani ya kipindi hichohicho....
73% decrease.jpg


Sababu zilizobainishwa zimewekwa katika makundi makuu mawili;

1. Mitindo ya maisha;
Sababu hizi wengi mmekua mkizifahamu hivyo sitoziongelea sana. Kuna uvutaji wa sigara wa wanaume na wanawake wenye ujauzito wa kiume, unywaji wa pombe, ulaji wa mhusika, stress pamoja na unene wa kupita kiasi. Zinaeleweka.....

2. Kemikali
Kuna kemikali zinazoharibu mfumo wa hormone za binadamu( Endocrine Disrupting Chemicals). Kemikali hizi zinafanya kupunguza hormone ya testosterone na kuongeza hormone ya estrogen kwenye mwili wa mwanaume, hivyo kupelekea ugumba, matatizo ya nguvu za kiume, kukosa hamu ya tendo la ndoa, pamoja na kupungua kwa urefu wa uume. Kemikali hizi zinawekwa kwenye vitu tunavyovitumia kila siku.....

Kemikali hizi zinapatikana kwenye vitu vifuatavyo;

chupa laini na ngumu za maji na watoto, dawa za kuulia wadudu
sabuni za kufulia, vifungashio vya vyakula kama foil, plastic wraps
detergent za chooni, maziwa ya kopo
makopo ya bati ya vinywaji na vyakula, nyama za viwandani
makontena, zana za michezo kama viatu na mipira
vipodozi, risiti
marashi, nguo mpya na samani
vyomba vya kulia visivyopata kutu, vyakula vilivyosafirishwa kutoka nje
vifaa vya kielektroniki

na kadhalika......
perturbateurs-endocriniens-sante-1536x573.jpg

Kwakua kemikali hizi ni nyingi mno, kwa maisha ya sasa ni ngumu mno kuepuka athari zake kwasababu zipo kwenye vitu vingi tunavotumia kila siku. Hata hivyo unashauriwa kujielimisha kuhusu hatari hii.

Ushauri uliotolewa ni kwamba watu waangalie viashiria ambavyo wanaweza kukwepa au kupunguza mfano; kufanya mazoezi, kupunguza unywaji wa pombe na uvutaji sigara, kupunguza utumiaji wa maji ya chupa, n.k....
 
Back
Top Bottom