Tafiti zinaonyesha 80% ya Wahalifu ikiwemo Wajambazi, wabakaji, wauaji, mashoga wamelelewa na Single Mothers yaani Fatherless

Tafiti zinaonyesha 80% ya Wahalifu ikiwemo Wajambazi, wabakaji, wauaji, mashoga wamelelewa na Single Mothers yaani Fatherless

TAFITI ZINAONYESHA 80% YA WAHALIFU DUNIANI IKIWEMO MAJAMBAZI, WABAKAJI, WAUAJI, MASHOGA WAMELELEWA NA SINGLE MOTHERS YAANI FATHERLESS

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Andiko hili halipo kwaajili ya kuwakandia single mothers bali lipo kwaajili ya kuonyesha matatizo ya u-single mother ambayo yanatokea kwenye jamii yetu ili tujue nini chakufanya.
Yeyote atakayechukulia kwa mtazamo hasi ihesabike kama kushindwa kwake kuelewa.

Tafiti mbalimbali duniani pamoja na uchunguzi wangu vinaonyesha kuwa Asilimia zaidi ya 80% ya Wahalifu Wanatokea katika familia ambayo hakuna Baba(FATHERLESS) na wengi Wamelelewa na Mama pekee (Single mothers).

In 1996, 70% of inmates in state juvenile detention centers serving long sentences were raised by single mothers.7

The absence of the father increases the daughters’ vulnerability to exploitation by those outside the family. Girls from homes without fathers are 6 times more likely to become pregnant as teenagers.9

Tafiti zingine zimetoa majibu haya
  • 63% ya vijana wanaojiua Wamelelewa na Mama pekee
  • 90% ya Chokoraa(homeless) na wazururaji wametoka kwenye familia zisizokuwa na Baba
  • 85% ya watoto wote wenye behavior disorders wametoka kutoka fatherless homes.
  • 80% ya Wabakaji wametoka kwenye familia zisizokuwa na Baba na Wamelelewa na single mothers
  • 71% ya walioacha shule au kuishia njiani Wamelelewa na single mothers
  • 75% ya walioko sobber wenye wanaotumia Madawa ya kulevya Wamelelewa na single mothers .
  • 85% ya vijana walioko jela au mahabusu wametoka familia zisizokuwa na Baba.
  • 75% ya mabinti
Tafiti zinaonyesha pia Mabinti wengi waliolelewa na Single mothers wanapata mimba kabla ya kuolewa na hiyo kuongeza zaidi single mothers.

Tafiti zinaonyesha kuwa makahaba wanaojiuza kwenye madanguro na wengine kujiuza barabarani Wanatokea familia zisizokuwa na Baba.

Tafiti hizi na zingine nyingi zinatupa picha kuwa malezi ya watoto na jamii hayawezi kuwa na tija kama familia hazitakuwa na Baba na Mama.

Imethibitika pasi na shaka kuwa Mwanamke licha ya umuhimu wake kwenye dunia lakini kwa sehemu kubwa Pekeake hawezi kuwafanya watoto wawe na maadili.

Hata hivyo sababu kubwa iliyotajwa ni suala la umaskini kwa wanawake waliowengi ambao baada ya talaka au mume kufariki au kutiwa mimba pasipo kuolewa inapelekea wao kushindwa mahitaji ya kifamilia kwa watoto.

Aisha, Sababu nyingine tajwa ni kuwa Mwanamke hata awe na uwezo wa kiuchumi wengi wao Bado asili ya huruma na upendo uliopitiliza kwa watoto hupelekea kushindwa kuwalea vizuri na hiyo kusababisha watoto kutokuwa na maadili.

Nafahamu wapo watu waliolelewa na Mama pekee na wenye maadili lakini watu hao kwenye hii dunia ni wachache sana. Uwepo wa wachache hao haiondoi ukweli kuwa watoto kulelewa na Mama pekee humweka katika hatari ya kuingia katika uhalifu na uovu.

Wito, ni vizuri kama mtu anampango wa kuleta kiumbe duniani ahakikishe anafuata njia sahihi ya kuwa na familia ya Mune na Mke. Tena Mume na Mke sahihi.

Acha nipumzike Sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
Umeandika kila kitu! Naunga mkono hoja tena nikiwa na mifano hai niliyoona kwa macho yangu.

Kwa ufupi sana niseme;
Baba ndiye KICHWA cha familia. Familia bila baba ni sawa na kuku aliyekatwa kichwa halafu akaachwa akimbie huku na huko.

Wanaume na Wanawake tambueni kuwa Baba ana umuhimu mkubwa sana kwenye malezi ya watoto na mustakabali wa familia nzima.

Wanaume tuwe serious na familia zetu. Wanawake watiini Waume zenu na mtambue umuhimu wao mkubwa katika familia.

Pesa haiwezi kulea watoto. Pesa bila uwepo wa Baba ni majanga. Mwenye masikio na asikie!
 
Hao ni asilimia ngapi kwenye idadi ya watized?
Ndio maana ya 80%
Inamaanisha wapo 20% ambao Wamelèlewa na Single Mothers na wana maadili
Hao ndio wanaleta Ujambazi kwa kutunga sheria ngumu kwa Watanzania watu hawajui hata kusoma wanawezaje kutunga sheria za kodi na Nchi ikaendelea zaidi ya kupiga makofi tu vifaa vya Ujenzi kodi juu kama makazi nayo ni Anasa..
 
Malezi ya baba ni muhimu sana,mtoto atajisikia vibaya kutolelewa na mama lakini atajisikia vibaya zaidi kumkosa Baba ktk kukua kwake.Niko kwenye ndoa na mwanamke ambaye hakupata malezi ya baba na malezi ya mama nayo hakuyapata kikamilifu kwa sababu mama yake alienda kuolewa akamuacha kwa bibi.Mweee mweee mweee..! mwanamke haambiliki,akifanya kitu sio sahihi ukamwambia anaamsha ni kama vile unamuonea anaona yuko sahihi na kutobehave kama mwanamke ALIYEOLEWA.Nikafikiria nimuachie kila kitu niondoke nibaki kulea hapana haitakua sahihi coz tuna mtoto wa kike ko ntakua nimetengeneza mazingira ya binti yangu kuja kua singo maza kama mama yake.Tofauti na kumzibua makofi mara moja tu kibri kilipozidi ilibidi nmuweke sawa kwa kuongea nae kwa upole na kumwambia ukweli na akajua udhaifu aliokua nao ulikua sababu ya malezi aliyopitia,walau naweza kusema asilimia 75 ndoa inaweza kusurvive.
 
Acha kuandika utumbo,sasa nikuambie kitu hao watu ambao wamelelewa na single mothers Mungu kawabariki sana na ndio watu wenye bahati sana
 
Hii nimeikubali kwa maana msingi wa familia ni wazazi wote wawili, jambo hili linampa wakati mgumu Sana hata mh Rais. Anawaasa vijana wote wa kike na kiume kuoa ama kuolewa na kuiheshimu taasisi hii mhimu ya ndoa.
 
Back
Top Bottom