kisumbusi
JF-Expert Member
- Nov 25, 2018
- 795
- 946
Mke sahihi, mume sahihiTAFITI ZINAONYESHA 80% YA WAHALIFU DUNIANI IKIWEMO MAJAMBAZI, WABAKAJI, WAUAJI, MASHOGA WAMELELEWA NA SINGLE MOTHERS YAANI FATHERLESS
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Andiko hili halipo kwaajili ya kuwakandia single mothers bali lipo kwaajili ya kuonyesha matatizo ya u-single mother ambayo yanatokea kwenye jamii yetu ili tujue nini chakufanya.
Yeyote atakayechukulia kwa mtazamo hasi ihesabike kama kushindwa kwake kuelewa.
Tafiti mbalimbali duniani pamoja na uchunguzi wangu vinaonyesha kuwa Asilimia zaidi ya 80% ya Wahalifu Wanatokea katika familia ambayo hakuna Baba(FATHERLESS) na wengi Wamelelewa na Mama pekee (Single mothers).
In 1996, 70% of inmates in state juvenile detention centers serving long sentences were raised by single mothers.7
The absence of the father increases the daughters’ vulnerability to exploitation by those outside the family. Girls from homes without fathers are 6 times more likely to become pregnant as teenagers.9
Tafiti zingine zimetoa majibu haya
Tafiti zinaonyesha pia Mabinti wengi waliolelewa na Single mothers wanapata mimba kabla ya kuolewa na hiyo kuongeza zaidi single mothers.
- 63% ya vijana wanaojiua Wamelelewa na Mama pekee
- 90% ya Chokoraa(homeless) na wazururaji wametoka kwenye familia zisizokuwa na Baba
- 85% ya watoto wote wenye behavior disorders wametoka kutoka fatherless homes.
- 80% ya Wabakaji wametoka kwenye familia zisizokuwa na Baba na Wamelelewa na single mothers
- 71% ya walioacha shule au kuishia njiani Wamelelewa na single mothers
- 75% ya walioko sobber wenye wanaotumia Madawa ya kulevya Wamelelewa na single mothers .
- 85% ya vijana walioko jela au mahabusu wametoka familia zisizokuwa na Baba.
- 75% ya mabinti
Tafiti zinaonyesha kuwa makahaba wanaojiuza kwenye madanguro na wengine kujiuza barabarani Wanatokea familia zisizokuwa na Baba.
Tafiti hizi na zingine nyingi zinatupa picha kuwa malezi ya watoto na jamii hayawezi kuwa na tija kama familia hazitakuwa na Baba na Mama.
Imethibitika pasi na shaka kuwa Mwanamke licha ya umuhimu wake kwenye dunia lakini kwa sehemu kubwa Pekeake hawezi kuwafanya watoto wawe na maadili.
Hata hivyo sababu kubwa iliyotajwa ni suala la umaskini kwa wanawake waliowengi ambao baada ya talaka au mume kufariki au kutiwa mimba pasipo kuolewa inapelekea wao kushindwa mahitaji ya kifamilia kwa watoto.
Aisha, Sababu nyingine tajwa ni kuwa Mwanamke hata awe na uwezo wa kiuchumi wengi wao Bado asili ya huruma na upendo uliopitiliza kwa watoto hupelekea kushindwa kuwalea vizuri na hiyo kusababisha watoto kutokuwa na maadili.
Nafahamu wapo watu waliolelewa na Mama pekee na wenye maadili lakini watu hao kwenye hii dunia ni wachache sana. Uwepo wa wachache hao haiondoi ukweli kuwa watoto kulelewa na Mama pekee humweka katika hatari ya kuingia katika uhalifu na uovu.
Wito, ni vizuri kama mtu anampango wa kuleta kiumbe duniani ahakikishe anafuata njia sahihi ya kuwa na familia ya Mune na Mke. Tena Mume na Mke sahihi.
Acha nipumzike Sasa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
Kumbe kuna wengine siyo sahihi?