Mswahili ni mtu ambae ana asili ya pwani, yaani kutokea mbwa maji yaani maeneno ya Gezaulole mpaka Pangani Tanga ukipitia Kigamboni (Tua moyo) hapa pana asili kubwa sana japo hapasikiki, Msasani, Kunduchi, Ununio, Bunju, Stahabu, Mlingotini (bwagamoyo ...mpaka huko Pangani mjini Tanga. watu wanaoishi au wenye asili ya maeneno hayo ndio waswahili.
Zaidi, Mswahili ana desturi zake za kipwani pwani, wengi wao wameloea asili za watu waliokuwa maeneno hayo yaani waarabu, na wengi wamechanganyika sana na waarabu wa enzi hizo. Ni watu wastaarabu, wenye kupenda watu yaani wageni, hawana makuu watu hawa na wenye ROHO ZA UKARIMU. na mengine mengi maani mie pia ni MSwahili.
Tofauti sana na watu wanavowafikiria waswahili.