Tafsiri halisi ya neno Mswahili

Tafsiri halisi ya neno Mswahili

Mswahili ni yeyote mwenye asili ya pwani ya afrika mashariki, huwasiliana kwa lugha ya kiswahili, ni binadamu mwenye fikra sahihi, ni mdadisi, hughani mang'amuzi kwa lugha ya kiswahili!

Huyo ndiye mswahili halisi,japo wengi hapo juu wamepotosha na kudhihaki maana ya mswahili
 
Sifa kuu ya mswahili ni kucheka cheka na kupenda sana kupiga misele isiyo na maana!
 
Mswahili ni yeyote mwenye asili ya pwani ya afrika mashariki, huwasiliana kwa lugha ya kiswahili, ni binadamu mwenye fikra sahihi, ni mdadisi, hughani mang'amuzi kwa lugha ya kiswahili!

Huyo ndiye mswahili halisi,japo wengi hapo juu wamepotosha na kudhihaki maana ya mswahili

Nashukuru ndugu yangu.
 
Mswahili ni mtu ambae ana asili ya pwani, yaani kutokea mbwa maji yaani maeneno ya Gezaulole mpaka Pangani Tanga ukipitia Kigamboni (Tua moyo) hapa pana asili kubwa sana japo hapasikiki, Msasani, Kunduchi, Ununio, Bunju, Stahabu, Mlingotini (bwagamoyo ...mpaka huko Pangani mjini Tanga. watu wanaoishi au wenye asili ya maeneno hayo ndio waswahili.

Zaidi, Mswahili ana desturi zake za kipwani pwani, wengi wao wameloea asili za watu waliokuwa maeneno hayo yaani waarabu, na wengi wamechanganyika sana na waarabu wa enzi hizo. Ni watu wastaarabu, wenye kupenda watu yaani wageni, hawana makuu watu hawa na wenye ROHO ZA UKARIMU. na mengine mengi maani mie pia ni MSwahili.

Tofauti sana na watu wanavowafikiria waswahili.
 
Maana za mswahili
1:m2 yeyote anaye zungumza lugha ya kiswahili
2:mtu muongo/asiye mkweli
3:mtu mwenye utamaduni wa pwani anayezungumza kiswahili
4:chotara kati ya mbantu na mtu wa mbele
5:
 
Waswahili asilia.

Jamii ya watu ambao lugha yao kuu ni kiswahili (Hawana lugha nyingine za kienyeji). Hawa wanapatikana zaidi Kisiwa cha Zanzibar, Ukanda wa Pwani ya kaskazini mwa Tanzania (ukiondoa Wadigo). Vilevile, kuna makabila mengine ambayo hayana lugha yao ya asili, kama vile Wasegeju wa Tanga, na wenyewe ni Waswahili vilevile.

Na baadhi ya miji ya Tanzania, kuna jamii au kundi la watu, waliozaliwa na kukulia mjini kiasi kwamba lugha zao za asili zimewatoka. Mawasiliano yao ni Kiswahili tu. Hawa nao ni Waswahili. Mfano hai upo Arusha, mitaa ya Kaloleni na Bondeni.
 
Maana za mswahili
1:m2 yeyote anaye zungumza lugha ya kiswahili
2:mtu muongo/asiye mkweli
3:mtu mwenye utamaduni wa pwani anayezungumza kiswahili
4:chotara kati ya mbantu na mtu wa mbele
5:



..................welawela namba 2 nimeikubali, hamjasikia mtu anakwambia "wacha uswahili?" au ahadi za kiswahili......
1. siyo kuzungumza,hata wazungu,wahindi, wasomali na wachina wanazungumza kiswahili.
2. siyo kuishi hata wazungu,wahindi,wasomali waarabu na wachina wanaishi pwani au uswahilini
3. siyo utamaduni maana utamaduni unahusisha lugha,mavazi na taratibu zote za maisha e.g.arusi na misiba
4. siyo boko na bunju na bagamoyo wanakopatikana waswahili, pwani yetu inaanzia lamu-mombasa-tanga-dar-mtwara-mpka Beira msumbiji

LETE HOJA
 
wana jf naomba mnijuze maana ya neno mswahili n.b maana ziwe 5
 
Neno mswahili lina maana nyingi baadhi yake ni: Mzaliwa wa pwani ya Afr Mash,Mtu mjanja,mtu anaye zungumza kisw nk
 
mswahili maana ingine ni mshamba a.k.a muongeaji sanaaa lkn hajui chochote.......
 
wana jf naomba mnijuze maana ya neno mswahili n.b maana ziwe 5

Mswahili ni mtu muongo- muongo hivi, haaminiki ktk kauli zake, ahadi zake mara nyingi si zakweli! na hujitetea kwa maneno mengi sana ya kiswahili hasa wakati wa kuyeyusha mada fulani inayomlenga!!!
 
Ili upate jibu la huyu mswahili, embu vuta taswira ya mtu wa mwambao ambaye hajaathiriwa na mambo ya kimagharibi + shule hana, sasa lifestyle yake ni normal na ameadapt maisha ya hapohapo. Ndo ujue mazungumzo yake yakoje na uelewa wake utakuwa umeathiriwa na upeo wake
 
Mswahili ni mtu muongo- muongo hivi, haaminiki ktk kauli zake, ahadi zake mara nyingi si zakweli! na hujitetea kwa maneno mengi sana ya kiswahili hasa wakati wa kuyeyusha mada fulani inayomlenga!!!

Hii tafsiri ya kichina. Nimekulia mwambao ninachoweza kukusaidia hakuna mtu mkweli kama mswahili. Nahisi unamuona ni muongo labda umekutana na uelewa wake mdogo alafu anataka aonekane nayeye wamo hivyo lazima awe muongo, na hao wako wengi hata wazungu wapo
 
Mswahili ni mtu anayeishi pwani na daima hupenda kuva kanzu,kushika bakora na barakashee kichwani ndivyo mm ninavyomfahamu.
 
Mswahili maana yake;
1. Mzungumzaji wa Lugha ya Kiswahili hasa aliye MMILISI.
2. Mtu anayejitia ujuz wakat hajui kitu
 
Samahani wanaJF, hivi Mswahili ni nani?

Kwa nijuavyo, mswahili ni mtu anaejua kiswahili na anayeongea sana maneno mazuri mazuri yenye ahadi nzuri nzuri ambazo hazitekelezi, yaani ana uongo mwingi kuliko ukweli.

Baadhi ya wabara wakifika pwani hujaribu kuiga uswahili na wengine wanafanikiwa kuwa waswahili wazuri!!

Kwa jumla, waTZ wengi wana uswahili kuliko waKenya na waGanda. Ndiyo maana sisi waTZ tuna maneno mengi kuliko vitendo!! Siasa siasa tu zisizo tafsirika katika vitendo!! Matokeo yake tuko nyuma kimaendeleo licha ya juwa na raslimai nyingi majirani zetu!!

Tuache uswahili ili tuendelee!! Tuache kuongozwa na waswahili!!

SAMAHANI KWA NILIOWAKWAZA!!

Asubuhi njema!!
 
mswahili ni mtu kutoka kabila la waunguja,ambao lugha yao ni kiswahili,ambayo ni lugha pekee iliyochaguliwa na wakoloni itumike kwa mawasiliano katika ukanda wa afrika mashariki.
 
Back
Top Bottom