Tafsiri halisi ya neno Mswahili

Tafsiri halisi ya neno Mswahili

Bwana Nonda. Nakushukuru kwa majibu.
Next, ningependa tusaidiane, maana ya PWANI. Ni umbali gani kutoka baharini? Hivi ukichukua kisiwa kama Madagascar, kwa mfano, je chote kinakuwa ni sehemu ya pwani? au ni umbali kadhaa kutoka baharini? Na visiwa vya zanzibar? Ukiwa Zanzibar kwenye nchi kavu, unakuwa ndani ya pwani? au kunakuwa na kaeneo fulani kutoka baharini kanakoitwa pwani (within Zanzibar). Sitoki nje ya mada, nahitaji tu-define pwani maana yake nini, halafu tujue watu wa pwani ni watu gani, ili tuzidi kuelewa zaidi kuhusu mswahili.

Maana ya pwani. Bofya hapa Search Results for 'coast' | Matokeo ya Utafutaji kwa 'coast' | The Kamusi Project
Coast - Wikipedia, the free encyclopedia

Kimasafa sina utaalamu nalo kuwa ukomo uwe kilomita ngapi kutoka makutano ya bahari na ardhi. Lakini kwa visiwa vidogo kimantiki yaweza kutumika ni eneo la pwani.

Lakini hapa tusichanganye mgawanyo wa kijografia na utawala,kama mkoa wa Pwani au mikoa ya pwani. Lililo hakika ni kuwa Ukerewe si pwani.Mafia, Zanzibar vina mwambao wa pwani.
Kwa hiyo watu wa pwani ni watu walio karibu na bahari.
Rafiki zao ni samaki wa maji chumvi.

Kisiwa kama UK au Madagascar vimezungukwa na bahari, zina mwambao lakini kwa ukubwa wake kuna bara na mwambao. Hata Australia imezungukwa na bahari..lakini linaitwa sub-continent lakini ina miambao katika pande zake zote. aka sehemu za pwani.

Ndugu Namren..mimi Nonda si mtaalamu wa lolote, JF ndio shule yangu.Ninajifunza mengi humu.
Natumai watajitokeza wataalamu wa jiografia na kutusaidia hili la masafa.

Swahili people - Wikipedia, the free encyclopedia

YouTube - Utamaduni wa mswahili
 
Waswahili ni wale wenye kulijua beni (au waweza ita mbwa kachoka ukipenda), kidumbak, kibao kata, taarab, sumsumia,

Wale wenye kula wali wa asumini, vipopoo, bokoboko, mbatata za urojo, kaimati,

Wale wenye kuujua kuutumia udi, halawa, liwa, singo,....

ebana weee....bora niishie hapa kwa sasa
 
Vizuri umejitokeza, umfikishie ujumbe Mtu wa Pwani aje aokoe jahazi,kuhusu masafa ya eneo la Pwani.
 
Vizuri umejitokeza, umfikishie ujumbe Mtu wa Pwani aje aokoe jahazi,kuhusu masafa ya eneo la Pwani.

Itabidi tumuwekee hii link Mtu wa Pwani kwenye visitors page yake......aje atoe majibu ya kina
 
Nimeingia mtu wa pwani kwanza cha kwanza kinachofanya tuwe wa swahili tunasema tumeona mengi tumepokea mengi ndo maana waswahili wengi tunaamini tumestaharabika kwa 7bu majahazi ya wazungu , waarabu ndo tuloyapokea na kuwaelekeza bara wakachukue watumwa lkn pili uongeaji wetu tunapenda kutumia mafumbo, nahau, methali, tash tit , sitiara n.k na pia kuongea kiswahili ww co mswahili kuna waswahili wenyewe km unavyoongea kiengereza na ukawa co muingereza km kuna swali kuhusu waswahili niulizeni kwa 7bu lazima ukitaka kufundishwa pikipiki mwalimu akukalie nyuma ili ww ukae mbele ufundishwe
 
AWAU'ZA WASWAHILI

1

Risala enuka hima, sikae 'kataghafali
N'na jambo 'takutuma, ubalegheshe suali
Nipate jawabu njema, yenye amani na kweli
Nauliza Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

2
Lugha nyingi duniyani, zatamkwa mbalimbali
Na zote ulimwenguni, zina wenyewe mahali
Si Hindi Si Uzunguni, mewaumbia Jalali
Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani ?

3
Wakamba wana kikwao, lugha yao ya asili
Na Wazungu piya nao, wana zao mbalimbali
Na Wameru wana yao, wengine ni Wasomali
Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani ?

4
Wahindi wana Kihindi, kwa kabila mbalimbali
Na Wanandi ni Kinandi, ndizo zao akuwali
Wengine ni Wakilindi, wana yao ya asili
Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

5
Kuuliza Si ujinga, musinifanye jahili
Nautafuta niuwanga, tuzinduwane akili
Ndipo shairi hatunga, kubaleghesha suali
Nielezwe Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

6
Mara nyingi husikiya, kuwa hichi Kiswahili
Hakina mtu mmoya, ambaye ni chake kweli
Na wengine huteteya, kina wenyewe asili
Ndipo ha'mba Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

7
Masai ana kikwao, lugha ya tangu azali
Na Mahara wana yao, wengine Mashelisheli
Na Waluo lugha zao, Si sawa na Maragoli
Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

8
Na jamii wengineo, wana lugha mbalimbali
Na kujuwa ya wenzao, ni kujifunza ya pili
Lakini wana na zao, lugha za tangu asili
Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

9
Sasa ambalo nataka, kwa wenye kujuwa hili
Wa Kenya na Tanganyika, na walo kulla mahali
Nipani ilo hakika, tubalegheshe ukweli
Nambiyani Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

10
Miye mefikiri mno, kuamuwa jambo hili
Na huona lugha hino, lazima ina asili
Kwa sababu kulla neno, lina mwanzo wa usuli
Ndipo ha'mba Kiswahili, hi lugha ya watu gani?

11
Na iwapo hivi sivyo, niliyyoamuwa hili
Nionyeshani viliyyo, mubainishe ukweli
Nijuwe ambavyo ndivyo, tutowane mushkili
Kifunuke Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

12
Na iwapo atakuja, wa kunijibu suali
Namuomba jambo moja, twambiyane kiakili
Tusionyane miuja, jambo nisilo kubali
N'anambiye Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

13
Tamati ndio akhiri, na jina langu ni hili
Ahmadi wa Nasiri, na Bhalo ndilo Ia pili
Mtungaji mashuhuri, mpenda penye ukweli
Nambiyani Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

By Ahmad Nassir from Malenga wa Mvita
 
Vipi waarabu tunaongea na kupenda lugha ya kiswahili, nasi pia mtatuita waswahili?
 
Very educative links.
Thanks.

kuhusu definition ya PWANI (coast) Nimeipata hii hapa:

Coast Defined home

Jaribu pia kuipitia.

Inaonekana hakuna concrete definition. Nchi mbali mbali zinatumia criteria tofauti. Hata suala la umbali toka kwenye maji, zinatofautina. Kuna ambao wanatumia 200m (viwanja viwili vya soccer) na wengine 100km. Kwa ujumla naona ni vigumu sana kum-define mtu wa pwani ni nani. Ugumu huo huo unakuwepo pia kwenye kum-define mswahili.
 
Nanren,
Kwanza link haifanyi kazi,haifunguki.

Huu ugumu wa ku-define ni kwangu mimi na wewe. Lakini wenyewe watu wa pwani wanajijua, waswahili wanajitambua, kwao hakuna ugumu kujijua.
Au ugumu pia uko katika kum-define nani mchaga, mzigua, mzanaki,mjaluo, mhaya?
 
Nimeingia mtu wa pwani kwanza cha kwanza kinachofanya tuwe wa swahili tunasema tumeona mengi tumepokea mengi ndo maana waswahili wengi tunaamini tumestaharabika km kuna swali kuhusu waswahili niulizeni kwa 7bu lazima ukitaka kufundishwa pikipiki mwalimu akukalie nyuma ili ww ukae mbele ufundishwe
Mkuu.
Unajua kuendesha pikipiki?
Ulijifunza wapi?
Ulikuwa na mwalimu? LOL
 
Maana ya pwani. Bofya hapa Search Results for 'coast' | Matokeo ya Utafutaji kwa 'coast' | The Kamusi Project
Coast - Wikipedia, the free encyclopedia

Kimasafa sina utaalamu nalo kuwa ukomo uwe kilomita ngapi kutoka makutano ya bahari na ardhi. Lakini kwa visiwa vidogo kimantiki yaweza kutumika ni eneo la pwani.

Lakini hapa tusichanganye mgawanyo wa kijografia na utawala,kama mkoa wa Pwani au mikoa ya pwani. Lililo hakika ni kuwa Ukerewe si pwani.Mafia, Zanzibar vina mwambao wa pwani.
Kwa hiyo watu wa pwani ni watu walio karibu na bahari.
Rafiki zao ni samaki wa maji chumvi.

Kisiwa kama UK au Madagascar vimezungukwa na bahari, zina mwambao lakini kwa ukubwa wake kuna bara na mwambao. Hata Australia imezungukwa na bahari..lakini linaitwa sub-continent lakini ina miambao katika pande zake zote. aka sehemu za pwani.

Ndugu Namren..mimi Nonda si mtaalamu wa lolote, JF ndio shule yangu.Ninajifunza mengi humu.
Natumai watajitokeza wataalamu wa jiografia na kutusaidia hili la masafa.

Swahili people - Wikipedia, the free encyclopedia

YouTube - Utamaduni wa mswahili

vidio imenukumbusha Barabara ya 20 Tangaaaaa.....!! Proud to be mswahili!....:biggrin1:
 
tuseme karibia watu wote wa Tz wanazungumza kiswahili , je ni sahihi kuwaita wote waswahili ? ama waswahili ni wale tu ambao wana asili ya mrima / mwambao ? naomba ufafanuzi ....

hakuna kabila linaloitwa waswahili bali wapo watu wanaozungumza kiswahili,kiswahili ni 'fusion' ya kibantu na kiarabu kwa kiasi kikubwa, na pia kwa uchache kuna muunganiko wa maneno mengine ndani yake yaliyotoholewa kutoka lugha nyingine kama vile kireno, kijerumani, kihindi, kiingereza n.k. watu wengi wanaozungumza kiswahili aidha wana lugha zao za asili au walikuwa na lugha zao za asili,na muunganiko wa kibantu na kiarabu kuzaa kiswahili kulitokana na ujio wa waarabu katika pwani ya Afrika Mashariki kwa ajili ya biashara ya watumwa na biashara nyingine na pia waarabu hawakuishia pwani tu bali waliingia ndani zaidi kama vile Tabora, Kigoma n.k kwa ajili ya biashara zao na hivyo 'medium of communication' kati yao ilikuwa ni mkoroganyo wa kibantu na kiarabu na ukizingatia kwamba kila mmoja alikuwa hajui lugha ya mwenzake, na hatimaye kiswahili kikaanza kuzaliwa taratibu. kwa hiyo kabla ya kufika waarabu kulikuwa na watu waliokuwa wakiishi kwenye mwambao wa pwani na walikuwa na lugha zao zilizokuwa zikishabihiana(kibantu) lakini walipoingia waarabu n.k kibantu hiki kikachanganyika na lugha ngeni na kuzaa kiswahili. Nasisitiza hakuna kabila la waswahili bali kuna lugha ya kiswahili iliyozaliwa kutokana na sababu nilizotoa hapo juu.
 
Habari wanalugha...

Naomba kusaidiwa maana au sifa walau zisipungue tano za MSWAHILI, ni swali ambalo niliulizwa nikambwela.
 
Kwanza nakusaidia jambo moja, Mswahili ni mtu yoyote ambaye akitaka kufikiri au kuwaza, basi anatumia Lugha ya Kiswahili.

Ili usiwe Mswahili basi fikra na mawazo yako yanayopita kichwani yanapaswa yawe kwa Lugha nyingine... i.e Lugha za makabila au hata kwa lugha za kigeni mfano Kifaransa, kitaliano au Kiingereza.

Mapaka hapo utakuwa umejielewa, Je wewe ni mmoja wapo? Kama jibu 'ndio' basi angalau unayo nafasi ya kutoa japo sifa moja ya Mswahili.
 
Mswahili ni mtu asiyeaminika kwa ahadi anazotoa
 
Mimi nafahamu kuwa mswahili ni mtu anaeongea lugha ya Kiswahili kwa ufasaha,
 
Mswahili ni mtu asiyeaminika kwa ahadi anazotoa

Inakera sana huu ni upotoshaji mkubwa sana, hapa JF kuna watu wanahitaji kujifunza na wako makini kwa hilo kwa hivyo mtu anapotoa tafsiri potofu kama hii anapoteza maana nzima ya jukwaa hili, kama hujui ni bora utulie tu ungoje wanaojua!

Kuongea kiswahili kwa ufasaha pekee haitoshi kumfanya mtu kuwa mswahili japo ni sifa mojawapo ya mswahili, kwa mtazamo wangu naamini kuwa mswahili ni lazima pamoja na kuongea na kufikiri kwa kiswahili, ili mtu awe msawhili napaswa kuishi kwa kufuata utamaduni wa kiswahili hii ikiwa ni pamoja na aina ya vyakula anavyokula, mavazi,nyimbo, matambiko na vitu kama hivyo!
 
Nashukuru sana mkuu, nimepata kitu hapa
 
Back
Top Bottom