Bwana Nonda. Nakushukuru kwa majibu.
Next, ningependa tusaidiane, maana ya PWANI. Ni umbali gani kutoka baharini? Hivi ukichukua kisiwa kama Madagascar, kwa mfano, je chote kinakuwa ni sehemu ya pwani? au ni umbali kadhaa kutoka baharini? Na visiwa vya zanzibar? Ukiwa Zanzibar kwenye nchi kavu, unakuwa ndani ya pwani? au kunakuwa na kaeneo fulani kutoka baharini kanakoitwa pwani (within Zanzibar). Sitoki nje ya mada, nahitaji tu-define pwani maana yake nini, halafu tujue watu wa pwani ni watu gani, ili tuzidi kuelewa zaidi kuhusu mswahili.
Maana ya pwani. Bofya hapa Search Results for 'coast' | Matokeo ya Utafutaji kwa 'coast' | The Kamusi Project
Coast - Wikipedia, the free encyclopedia
Kimasafa sina utaalamu nalo kuwa ukomo uwe kilomita ngapi kutoka makutano ya bahari na ardhi. Lakini kwa visiwa vidogo kimantiki yaweza kutumika ni eneo la pwani.
Lakini hapa tusichanganye mgawanyo wa kijografia na utawala,kama mkoa wa Pwani au mikoa ya pwani. Lililo hakika ni kuwa Ukerewe si pwani.Mafia, Zanzibar vina mwambao wa pwani.
Kwa hiyo watu wa pwani ni watu walio karibu na bahari.
Rafiki zao ni samaki wa maji chumvi.
Kisiwa kama UK au Madagascar vimezungukwa na bahari, zina mwambao lakini kwa ukubwa wake kuna bara na mwambao. Hata Australia imezungukwa na bahari..lakini linaitwa sub-continent lakini ina miambao katika pande zake zote. aka sehemu za pwani.
Ndugu Namren..mimi Nonda si mtaalamu wa lolote, JF ndio shule yangu.Ninajifunza mengi humu.
Natumai watajitokeza wataalamu wa jiografia na kutusaidia hili la masafa.
Swahili people - Wikipedia, the free encyclopedia
YouTube - Utamaduni wa mswahili