Tafsiri halisi ya neno Mswahili

Tafsiri halisi ya neno Mswahili

Ni kweli mswahili ni vigumu sana kwenda na muda, wengi wao wanachelewa mno
 
Wana Jamvi
Asalam aleikhoum, Bwana Yesu asifiwe.
Maishani mwetu sina shaka tuna maneno na vitu ambavyo si vigeni, mfano watu na Lugha.
Ukizungumzia Mtu (singular) au watu ( Plural ) kila mmoja wetu anaelewa.
Huyu mtu au mwanadam katika uhalisia wake alipewa uwezo au katika mazingira yake awe na Lugha.
Lugha moja wapo ikiwa kiswahili ambayo ilipatikana kwa mchanganyiko wa Lugha ya Kiarabu na makabila ya mwambao was Bahari ya Hindi kama kwenye karne ya 15.
Tuje kwenye kitovu cha nyuzi hii kwamba mzungumzaji wa Lugha ya kiswahili anaitwa mswahili.
Katika tafiti na uzoefu nimekuwa nikisikia kwamba mswahili halitumiki kwa maana ya mzungumzaji wa kiswahili tu neno hili huambatana na maana nyinhi tu maana kuna wakati utamsikia mtu akisema......yule mzungu ni mswahili!
Wakati mzungu Huyo kiswahili hakijui katika kulitafakari au kutafuta maana halisi ya neno Mswahili nimeamua kulileta mkekani tusikie wenzi wetu wana mawazo gani tofauti na tuliyo nayo wengi wetu.
Ahsanteni
 
Kwanza kabisa Uswahili ni kitu hasi, machukizo.

Hakuna binti duniani amewahi kusema nampenda sana yule kaka, ana mambo ya Kiswahili.

Mfano hai uliotumika kwenye habari za kitaifa wiki hii ni pale Sheikh Mkuu wa Rukwa, Bw. Rashid Akilimali, aliposema:

“Takbirrr... Allahu Akbar. Wametukatalia kujenga msikitiki kwa kibri tu, wanasema hawataki Uswahili.”
 
Kwanza kabisa Uswahili ni kitu hasi, machukizo.

Hakuna binti duniani amewahi kusema nampenda sana yule kaka, ana mambo ya Kiswahili.

Mfano hai uliotumika kwenye habari za kitaifa wiki hii ni pale Sheikh Mkuu wa Rukwa, Bw. Rashid Akilimali aliposema:

“Wametukatalia kujenga msikitiki kwa kibri tu, wanasema hawataki Uswahili. Tunawapa mpaka Jumatano! Takbirrrrr... Alahu Akbar.”
Mkuu
mambo ndio hayooo!
Machukizo hapa ni nini? Kosa kuzungumza kiswahili? Nimejiuliza mengi ndipo nikapenda kujumuisha mawazo mengine.
 
Mkuu
mambo ndio hayooo!
Machukizo hapa ni nini? Kosa kuzungumza kiswahili? Nimejiuliza mengi ndipo nikapenda kujumuisha mawazo mengine.

Baadhi ya tabia za Kiafrika, kwa mfano hatuna umuhimu na muda. Rais anatua airport hana haraka ya kwenda Ikulu, mitaa ishafungwa masaa tunamsubiri apite, yeye anaanza kuchezewa ngoma za Kiswahili.
 
Mimi ni mtanzania. Kabila yangu ni mswahili. Kama tunavyojua kiswahili ni lugha za asili kama kisukuma, kihaya, kizanaki. Nk na ni ukweli usiofichika kuwa eneo kubwa LA watanzania hawajui kiswahili.

Sifa kubwa na nzuri iliyoficha ni kuwa waswahili ndio watu pekee walionzisha harakati za kipigania Uhuru na kwa litambua hilo Mzee nyerere akawaenzi badala ya kuchagua kizanaki kuwa lugha ya taifa akachagua lugha ya kabila langu ya waswahili kuwa lugha ya taifa.

Hayo maneno ya mitaani hayatutii unyonge kwa sisi huwa tunayaweka kwenye kawa na khanga

Lkn mswahili ni nani? Pitia hapa

Hizo zote ngonjera tu,Mswahili ni mtu anayetokea katika pwani ya swahili na anaongea kiswahili..
 
Mswahili ni mzawa wa Pwani ya Afrika Mashariki mwenye kusema lugha ya kiswahili na kufuata tamaduni za kiswahili iwe ni lugha, ngoma, mila na desturi

Kiswahili ni lugha moja iliyotokana na mchanganyiko wa lugha za kibantu kwa asilimia 69, mchanganyiko wa lugha za kiarabu na nyinginezo (kiingereza, kijerumani,kihindi, kireno, kigiriki n.k) kwa asilimia zilizobaki
 
Mimi ni mtanzania. Kabila yangu ni mswahili. Kama tunavyojua kiswahili ni lugha za asili kama kisukuma, kihaya, kizanaki. Nk na ni ukweli usiofichika kuwa eneo kubwa LA watanzania hawajui kiswahili.

Sifa kubwa na nzuri iliyoficha ni kuwa waswahili ndio watu pekee walionzisha harakati za kipigania Uhuru na kwa litambua hilo Mzee nyerere akawaenzi badala ya kuchagua kizanaki kuwa lugha ya taifa akachagua lugha ya kabila langu ya waswahili kuwa lugha ya taifa.

Hayo maneno ya mitaani hayatutii unyonge kwa sisi huwa tunayaweka kwenye kawa na khanga

Lkn mswahili ni nani? Pitia hapa

Mkuu,
Ahsante sana kwa data collection yako.
Kwa kiasi kikubwa nimemjua mswahili ni mtu gani na alili yake nini kuweza kusimamisha mswahili kama sifa.
 
Hizo zote ngonjera tu,Mswahili ni mtu anayetokea katika pwani ya swahili na anaongea kiswahili..
Pwani ya Swahili ni ipi. Video ya mswahili ni nani imetoa historia kiufasaha nafikiri kwa mwelewa ameelew mswahili ni nani sasa Hutu anatuambia nini?
 
Pwani ya Swahili ni ipi. Video ya mswahili ni nani imetoa historia kiufasaha nafikiri kwa mwelewa ameelew mswahili ni nani sasa Hutu anatuambia nini?
Pwani ya swahili ni pwani ya bahari ya hindi kutoka Sofala msumbiji mpaka Mogadishu Somalia.
 
Mshwahili ni mtu wa blabla nyingi plus ujuaji mwingi mvivu mbea na tapeli
 
Mshwahili ni mtu wa blabla nyingi plus ujuaji mwingi mvivu mbea na tapeli
Asante Boss kwa mchango wako.
Hii yote mkuu inaletwa na nini?
Kwa vitu ulivyovitaja ndio vinaharibu profile ya mswahili.
 
Pwani ya swahili ni pwani ya bahari ya hindi kutoka Sofala msumbiji mpaka Mogadishu Somalia.
Asante mkuu kwa taarifa yako, lakini hii Swahili coast nimeisikia kwako, naomba utupe reference umeitoa vitabu gani.
 
Wataalam wa lugha naomba kujua maana tano za neno mswahili ni mtu wa namba gani?
IMG_-yq4cls.jpeg
IMG_-q3a1q.jpeg
IMG_20181104_202731_276.jpeg
 
1.Ni mtu mwenye ngozi nyeusi
2.mtu aliyezaliwa ukanda wa Afrika mashariki
3.mtu mwenye maneno mengi ya uongo,ulaghai,mjanja nk
4.mtu ambaye lugha yake ya kwanza ni kiswahili
5.
 
Back
Top Bottom