Tafsiri halisi ya neno Mswahili

Tafsiri halisi ya neno Mswahili

Sasa hizo mbinu zinahusiana nini na Waswahili pekee?

Kwanza "Waswahili" ni nani?

Wasukuma waliozaliwa Kinyasini na kukulia huko tangu linajengwa Azania Front ni Waswahili au si Waswahili?

Na waliolowea tangu wamekuja chuo kikuu 1975 na kuoa visura wa Kizaramo?

Na watoto wao waliokulia Dar, lakini wakakimbilia kusoma Canada?

Wazanzibari waliolowea Tabora tangu wamemsindikiza Stanley, na waarabu wa Tabora kina Rostam Aziz na Mzee Said El-Maamry ni Waswahili au si Waswahili?

Uswahili unaanzia wapi na kuishia wapi?

Unatokana na kabila, ni utamaduni au ni nini?

Na kwa nini Uswahili uwe kama neno lingine la kumaanisha "ushenzi" wakati tuna hodhi tamaduni zenye tunu za Sheikh Amri Abeid na johari ziso uanagenzi za magwiji kama Shaaban Robert? To say nothing of Mathias Mnyampala.

Speaking of Mathiasi Mnyampala, alikuwa Mswahili au la?

Hata kumjua hawa wanaojifanya kukandia uswahili wanamjua?
 
Ze Great WaSwahili never die!! Tunasema mswahili mzuri yule alokufa....! ndo tulojaaliwa tena.
 
Uswahili unaanzia wapi na kuishia wapi?

Unatokana na kabila, ni utamaduni au ni nini?

Mimi mpaka leo sijapata jibu la kuridhisha kuhusu 'uswahili' au 'mambo ya kiswahili'.

Kwa sababu, kama ni tabia za mtu ambazo ndiyo hulengwa kwa kuitwa uswahili, mbona tabia hizo hata wengine wasio Waswahili wanazo? Sasa iweje ziwe tabia za Kiswahili wakati hata mu-Inca naye anaweza kuwa nazo?

Au labda ndiyo masalia ya ukoloni hayo?
 
Umeona eenh, hivi naomba muongozo, mswahili ni nani
Kwanza "Waswahili" ni nani?

Waswahili ni jina la kutaja wakazi wa miji ya pwani ya Bahari Hindi katika Afrika ya Mashariki, hasa na Kenya ambao ni wasemaji wa lugha ya Kiswahili kama lugha ya kwanza. Neno "Swahili" latokana na Kiarabu "sawahil" yaani pwani, kwa hiyo maana yake ni "watu wa pwani". Lakini si makabila yote ya pwani la Afrika ya Mashariki ambao ni Waswahili.

Sosi: Waswahili - Wikipedia, kamusi elezo huru

Wasifu hasi wa Mswahili ni zao la kihistoria ambapo Mswahili alitafsiriwa kama mtu ambaye hakuwa na 'ustaarabu' kamili wa Kiarabu na/au 'usasa' wa Kizungu.

Sosi: Yahoo! Groups
 
athante best ila ndo hivyo alivyotumia mtoa mada kwamba hayo yote yanawahusu wenyeji wa kanda ya pwani tuuuu au,
 
Labda atueleze walengwa walikuwa ni kina sisi au wengineo
 
Waswahili ni jina la kutaja wakazi wa miji ya pwani ya Bahari Hindi katika Afrika ya Mashariki, hasa na Kenya ambao ni wasemaji wa lugha ya Kiswahili kama lugha ya kwanza. Neno "Swahili" latokana na Kiarabu "sawahil" yaani pwani, kwa hiyo maana yake ni "watu wa pwani". Lakini si makabila yote ya pwani la Afrika ya Mashariki ambao ni Waswahili.

Sosi: Waswahili - Wikipedia, kamusi elezo huru

Wasifu hasi wa Mswahili ni zao la kihistoria ambapo Mswahili alitafsiriwa kama mtu ambaye hakuwa na 'ustaarabu' kamili wa Kiarabu na/au 'usasa' wa Kizungu.

Sosi: Yahoo! Groups

Hujatuambia nani Mswahili na nani si Mswahili bado.

Kuna watu wengi wa bara wamehamia pwani tangu enzi za upagazi kwa Wajerumani kabla ya mkutano wa Berlin, wakafanya vizazi pwani, lakini si wa makabila ya pwani, hawa ni Waswahili au la?
 
Mkuu sio kwamba nilikuwa najibu swali, bali nilikuwa nachagiza mjadala mliouibua kwa kutoa matamshi ambayo wengine wamejaribu kudadavua.

Ninaamini kama tukijua Mswahili ni nani basi walio kinyume na hapo si Waswahili
 
Ni vizuri tu, tunachepukia kwenye jibu lakini jibu linaonekana si rahisi kupatikana.

Na hili si kwa "mswahili" tu.

Hata "mzungu" is a vague term.
 
mswahili!
kiswahili
viswahili
uswahili
waswahili
uswahilini
kuna mjadala hapa!
 
Aaaargh tuacheni bana watoto wa uswahilini issue za kuja kusimuliana Isidingo wakati skani hata jiko la mchina hatuna mnakuwa kama mnatugogoa kiaina!!!!!!!

Kama kwenu kimeeleweka na unamiliki ndinga isiwe sababu ya kutusolola ooonh mtoto wa uswazi sijui mambo ya kiswazi na manenooooooo kibaoooooooo ya kuzinguana kisa umesoma kwenu kuna fensi na madirisha ya aluminiamu!!!!!!!!

Kama kwenu mna jokofu na sie tunanunua barafu ili kupoza maji mwisho wa siku si wote tunakunywa ya baridi?????!!!!!!!!

Acheni hiyo mambo bana ndo maana mkikatizaga kitaa mida mibovu huwa tunwakwala mazaga sababu ya kujishebedua na utinginjolo wenu

Kama vipi tupotezeeni tu mjue sio ishu wala nini kuongeleana kisa tofauti za kimaisha!!!!!!!!
 
Kwanza "Waswahili" ni nani?

Wasukuma waliozaliwa Kinyasini na kukulia huko tangu linajengwa Azania Front ni Waswahili au si Waswahili?

Na waliolowea tangu wamekuja chuo kikuu 1975 na kuoa visura wa Kizaramo?

Na watoto wao waliokulia Dar, lakini wakakimbilia kusoma Canada?

Wazanzibari waliolowea Tabora tangu wamemsindikiza Stanley, na waarabu wa Tabora kina Rostam Aziz na Mzee Said El-Maamry ni Waswahili au si Waswahili?

Uswahili unaanzia wapi na kuishia wapi?

Unatokana na kabila, ni utamaduni au ni nini?

Na kwa nini Uswahili uwe kama neno lingine la kumaanisha "ushenzi" wakati tuna hodhi tamaduni zenye tunu za Sheikh Amri Abeid na johari ziso uanagenzi za magwiji kama Shaaban Robert? To say nothing of Mathias Mnyampala.

Speaking of Mathiasi Mnyampala, alikuwa Mswahili au la?

Hata kumjua hawa wanaojifanya kukandia uswahili wanamjua?

Ulitazama TBC1 jana?
kulikuwa na kipindi cha kiswahili na waliwafanyia interview watoto wa Mnyampala na Sheikh Amri Abeid..
 
Woow, sikuweza kutazama, not sure kama inapatikana kwa mtandao huku antipode of the antipode.

Imekuwa nasibu tu.
 
Walihojiwa na kilichongaza ni jinsi walivyo point out
kuwa sio watu wa kawaida tu hawajui historia vizuri bali mpaka Waandishi wa habari
mfano waandishi wengi wanauita uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid ,
wana changanya na Karume
so inakuwa 'Sheikh Amri Abeid Karume'
watu wawili tofauti wanachanganywa....
Achilia mbali vitabu vya magwiji wa Lugha ya Kiswahili kama hao kuwa available Kenya zaidi
kuliko Tanzania...
 
mswahili ni mtu wa ajabu ajabu asiyejitambua. wivu wa kijinga. mbeya. mnoko. wengi wanaishi uswahilin.
uzunguni hakuna mswahili kila mtu anaishi kivyake bila kufatiliana kama waswahili.

asante kwa ujumbe mzuri uliotupa. tutakuwa makin na waswahili.
 
Back
Top Bottom